Jinsi Sabatier alivyokabiliana na umaskini hadi kustaafu akiwa na miaka 30

Akiwa na miaka 24, hakuwa na chochote kabisa. Akaunti yake benki ikiwa na dola 2.26 pekee na hakuwa na kazi, wakati huo ndipo alipoamua kurejea nyumbani kwa wazazi wake.

"Nilikuwa nalala kwenye kitanda kile kile nilichokuwa nakilalia nikiwa mdogo," Grant Sabatier, mwandishi wa kitabu cha Financial Freedom - ambacho kiliuzwa kwa wingi nchini Marekani - na mwanzilishi wa tovuti ya Millennial Money, amezungumza na BBC Mundo.

Mwaka 2010 wazazi wake walimpa miezi mitatu kuondoka kwenye nyumba yao. Akiwa amehitimu somo la falsafa na wakati hata hajaitwa katika mahojiano ya kutafuta kazi, akaanza kufikiria namna ya kutafuta pesa.

Na wakati huo ndipo alipojitoa kuanza kuchunguza namna kampeni za matangazo ya Google zinavyoendeshwa na kwa kipindi cha mwezi mmoja alijifunza akiwa nyumbani namna ya kuendesha matangazo hayo - kupitia mafunzo na miongozo iliyokuwa inapatikana katika tovuti na akaanza kutafuta kazi.

"Mara ya kwanza nilipotuma maombi kutafuta kazi hiyo ya uuzaji kupitia njia ya digitali, Nikaipata," anasema. Na kuanzia hapo maisha yangu yakabadilika. Akaondoka kwenye nyumba ya wazazi wake na kujiwekea lengo la kuweka akiba na kuwekeza kadiri ya uwezo wake.

Katika kipindi cha miaka mitano alikuwa na dola milioni 1.25 za Marekani, amesema Sabatier kutoka New York.

"Nilikuwa naishi kwenye nyumba duni, Gari yangu ilikuwa mbaya na muda wangu mwingi nilikuwa nautumia kufanya kazi na kuweka akiba."

Lakini bila shaka, peza zote hizo hakuzipata kwa kazi anayofanya. Muda wake wa ziada, alikuwa anaendesha kampeni zake za kibiashara mitandaoni akiwa na wateja kadhaa.

"Wakati fulani nilikuwa na vyanzo 13 tofauti vya kujipatia kipato."

Baada ya mwaka mmoja, alianzisha kampuni yake ya kuendesha matangazo kwa njia ya dijitali na miezi sita baadaye, akaanzisha kampuni ya pili.

"Nilistaafu nikiwa na miaka 30"

"Niliweka pesa nyingi kiasi kwamba nikaamua kustaafu nikiwa na miaka 30 na leo hii kazi ninayofanya nikuandika kwenye blogu," amesema Sabatier, ambaye sasa hivi ana miaka 34.

"Nilistaafu kufanya kazi katika kampuni kwasababu sihitaji tena pesa, naweza kuishi kwa kutumia pesa ambazo nimetengeneza katika kipindi changu chote cha maisha kilichosalia."

Sabatier anaitaja hali hiyo kama "uhuru wa kifedha, " kama jina la kitabu chake.

Kustaafu hakumaanishi kuwa mtu hawezi kufanya tena kazi, nikufanya kile unachopenda."

Ukweli ni kwamba, kufanya kazi yenye uhusiano na biashara mtandaoni haikuwa kile anachotaka maishani, lakaini alichukulia kazi hiyo kama njia moja ya kumpa kipato.

"Kuanzia mwanzo lengo langu lilikuwa kupata pesa za kununua uhuru wangu."

"Nilikuwa na shauku ya kupata pesa," Sabatier anasema.

Na mwisho wake dhamira iliyokuwepo ni kuweka akiba na kuwekeza akiwa bado na umri mdogo.

"Nilinunua uhuru wangu"

"Ilinichukua miaka mitano, miezi mitatu na siku sita," anasema. Na msingi wa kufikia lengo hilo ulitokana na sababu kadhaa.

"Kuna bahati ndani yake, kufanya kazi kwa bidii, kuwa na shauku na kuwekeza ulichoweka akiba kwa njia nzuri."

Sabatier alianza kuwekeza mwaka 2010, wakati soko lilipokuwa halifanyi vizuri na kupata faida kupitia alichopata katika njia zake zingine za uwekezaji.

"Nilifanikiwa kuweka asilimia 82 ya kipato changu. Bado naona uwekaji akiba kama fursa wala sio kujinyima," aliongeza.

Los ingresos entre los jóvenes noruegos aumentaron un 13% respecto a generaciones anteriores inmediatas. Una ten...

Unawezaje kufanikiwa?

Sabatier anasema kuwa kuna hatua tatu kufikia uhuru wa kifedha.

1- Kadiri unavyoendelea kuweka akiba ndivyo unavyoweza kufikia uhuru wa kifedha kwa haraka. Ikiwa utaweka akiba ya asilimia 5 au 10, hautawahi kufikia uhuru huu. Kiwango muafaka ni kuweka akiba ya asilimia 50.

Lakini kwa hilo kutokea, utalazimika kuishi katika nyumba ndogo pamoja na wengine kwa kipindi cha takriba miaka 5.

2- Tumia fursa zote unazopata kutafuta pesa. Utaanza na kazi ulioajariwa lakini tafuta vyanzo vingine vya kupata kipato kando na kutegemea shahara.

3- Wekeza kile ulichoweka akiba.

Sabatier aliwekeza katika nini?

Katika majengo na soko la hisa. "Kadiri unavyowekeza, utakuwa unapunguza muda wako unaotumia kutafuta pesa."

Na sasa hivi, Sabatier anaishi na mke wake mjini New York na licha ya kwamba ni moja ya miji ambayo gharama ya maisha iko juu zaidi nchini Marekani, anasema matumizi yake sio zaidi ya dola 50,000 za Marekani kwa mwaka.

"Naweza kutumia zaidi ya kiwango hicho cha pesa, lakini sitakuwa na furaha," anasema, na kueleza kuwa mengi anayopenda kufanya huwa ni bure kama vile kusikiliza muziki na marafiki au kutazama filamu na mke wake.

Na mwisho anaeleza kuwa, "kadiri unavyoendelea kufanya matumizi ndivyo utakavyolazimika kufanyakazi kwa miaka mingi."