Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Volcano Congo:Sihami Mji wa Goma licha ya kuathiriwa na Volkano mara tatu
Kwa mtu wa kawaida ,kutokea kwa janga lolote katika sehemu unakoishi ni hatua itakayokufanya uake kuhama na kutafuta hifadhi katika eneo salama .
Mlipuko wa Volkano yam lima Nyaragongo huko Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni mkasa ambao ulisababisha vifo vya watu Zaidi ya 30 . Maelfu ya wakaazi waliachwa bila makao na uharobifu mkubwa kusababishwa na mtiririko wa Lava.
'Volkano mara tatu'
Lakini kwa Mchunganji Muherenywa ,Goma ni nyumbani na kamwe hana mpango wa kuhama na hajahama licha ya kwamba aliathiriwa na mlipuko wa Volkano kwa mara ya kwanza mwaka wa 1977 alipokuwa kijana mdogo .Wakati huo Volkano ililipuka wakati wa asubuhi na kudumu kwa siku moja pekee.
' Nilikuwa kijana mdogo na tulikimbilia Gisenyi nchini Rwanda .. tulirudi tukaingia nyumbani tukakatazwa tusitoke tena' anasema Muherenywa.
Alipokuwa mtu mzima ,alishuhudia tena na kuathiriwa na mlipuko wa pili wa Volkano ya mlima huo mwaka wa 2002 ambapo watu zaidi ya 250 walifariki . Licha ya mlipuko huo wa pili Muhereywa anasema hakuwahi kufirikia kuhama Goma kwani anasema mji huo ndio nyumbani .
'Katika mlipuko wa 2002 volkano ilianza kulipuka majira ya asubuhi na serikali ilikataza watu wasiende..kulikuwa ma mitetemeko kwanza kabla ya moto kuanza kuonekana' anaongeza .
Masaibu yake kuhusiana na milipuko ya Volkano Goma hayakuishia hapo na siku ya jumamosi ilikuwa mara ya tatu kwake kujipata akiponea janga kama hilo.
'Volkano ilipolipuka hapakuwa na habari kuhusu hatari.Serikali haikutoa tahadhari.. baadaye fujo zilizuka na watu walipopata habari , walishtuka na kuanza kukimbia wakielekea maeneo mengine' amesema Muherenywa
Muherenywa anasema wakaazi wengi wanalazimika kukaa katika eneo hilo hatari kwa sababu hawana pengine pa kwenda na wanaogopa kwamba mali yao na nyumba zitavunjwa na wezi iwapo watahamia maeneo mengine
Hatukujua Volkano italipuka
Katika mlipuko wa volkano siku ya jumamosi lava ilikomea katika wilaya ya Buhene, nje kidogo ya Goma, ikizika mamia ya nyumba na hata majengo makubwa. Jitihada za ujenzi zinaweza kuchukua miezi.
"Nyumba zote katika mtaa wa Buhene ziliteketezwa," Innocent Bahala Shamavu aliliambia shirika la habari la Associated Press.
Mahali pengine, lava ilivuka barabara ya N2 inayounganisha Goma na jiji la Beni, ikikata msaada muhimu na njia ya usambazaji. Walakini, uwanja wa ndege wa jiji hilo haukuguswa, licha ya ripoti za mapema kwamba ulikuwa umeathiriwa.
Volkano hiyo, iliyoko 10km (maili sita) kutoka Goma, ililipuka mara ya mwisho mnamo 2002, na kuua watu 250 na kuwafanya 120,000 kukosa makazi.
Wakazi walianza kuondoka katika nyumba zao hata kabla serikali haijatangaza mpango wa uokoaji. Usiku, umati wa watu ulionekana ukikimbia kwa miguu na magodoro na vitu vingine.
Mamlaka ya Rwanda ilisema zaidi ya watu 3,000 walikuwa wamevuka rasmi kutoka Goma. Wengine walianza kurudi Jumapili. Wengine walikwenda kwenye maeneo ya juu magharibi mwa jiji.
Mkazi mmoja wa Goma, Richard Bahati, alisema alikuwa nyumbani kwake aliposikia mayowe na alikuwa na wasiwasi mkubwa alipoona mbingu ikiwa nyekundu nje.
"Niliishi kupitia shida na volkano hii mnamo 2002. Volkano hiyo iliharibu nyumba zetu zote na mali," alisema.
Watu walitoroka bila kujua wanaenda wapi
Mfanyabiashara kwa jina , Kambere Ombeni, alikuwa miongoni mwa wale waliorudi katika eneo la tukio huku vifusi vikitapakaa.
''Tulitazama nyumba zote katika eneo la Nyarigongo likichomeka moto. Moto ulifika hadi hapa, hata sasa tunaweza kuona uji wa mlipuko wa volcano hiyo'', alisema.
Mkaazi mwengine , Irene Baula , alisema kwamba watu watahitaji usaidizi kutoka kwa serikali ili kujenga upya maisha yao.
''Kuna ardhi , watu, idadi ya watu ambayo imepoteza kila kitu, pengine pia kuna vifo, ni nani anayejua''?.
''Tunaiomba serikali kuwasaidia manusura wa mlipuko huu''.
Tom Peyra Costa, kutoka baraza la wakimbizi la Norway mjini Goma aliambia BBC kile kilichotokea.
"Uji uliokuwa ukitiririka ulikuwa polepole sana kama kilomita kwa saa, lakini haukusita… ulianza kuchoma nyumba'' , akiongezea kwamba mashirika ya kibinadamu yalikuwa tayari yameanza kuangazia mahitaji ya wakazi.
Mlima Nyiragongo ni moja ya milima inayolipuka Volkano lakini kulikuwa na wasiwasi kwamba vitendo vyake havikuchunguzwa vizuri na shirika la kuchunguza milipuko ya volcano mjini Goma tangu Benki ya dunia ilipositisha ufadhili kufuatia madai ya ufisadi.
Profesa Mike Burton, mtaalamu wa milipuko ya Volcano katika chuo kikuu cha Manchester nchini England , aliambia BBC kwamba uji wa volcano katika mlima Nyiragongo umekuwa na uwezo wa kutiririka kwa kasi .
Katika ripoti yake shirika hilo lilionya kwamba vitendo vya ardhini vya mlima huo vimeongezeka.
Mwaka uliopita , Mkurugenzi wa shirika hilo la Goma aliambia BBC kwamba ziwa la mlima huo wa Volkano limekuwa likijaa kwa haraka hatua ilioongezea uwezekano wa mlipuko katika miaka michache ijayo.
Lakini pia alionya kwamba tetemeko la ardhi linaweza kusababisha janga mapema.
Mlipuko mbaya zaidi wa volakano katika mlima huo ulitokea 1977 ambapo zaidi ya watu 600 walifariki.