Mzozo wa Israel na Palestina: Uwezo na mapungufu ya silaha zinazotumiwa na Hamas dhidi ya Israel

Silaha ya kutungua makombora katika anga za Israel 'Irone Dome' zimefanikiwa kulipua asilimia 90 ya roketi zinazoingia nchini Israel kutoka Gaza.

Huku mauaji na uharibifu ukiathiri pande zote mbili za mzozo, - Wapiganaji wa Palestina waliopo ukanda wa Gaza dhidi ya vikosi vya Israel - inasemekana haijulikani ni lini mzozo huo utakwisha.

Israel imejikita katika mfumo wa kulinda anga yake kupitia ndege za kivita na zile zisizo na rubani ambazo zinaweza kutumika kushambulia Gaza wakati wowote ule.

Lakini licha ya kwamba Hamas na Islamic Jihad ndio wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa , wanamiliki silaha za kutosha kuishambulia Israel.

Msemaji wa wizara ya Ulinzi amesema kwamba''baadhi ya wapiganaji wa Hamas walitaka kuingilia kupitia handaki kutoka kusini mwa upande wa Gaza .

Inaonekana kwamba Israel ilipokea habari kuhusu shambulio hilo na kuliharibu handaki hilo.

Lakini silaha muhimu zinazomilikiwa na Wapalestina ni aina tofauti ya roketi ambazo zinaweza kurushwa kutoka ardhini hadi eneo lolote lile nchini Israel.

Baadhi ya roketi hizo zinadaiwa kusafirishwa kimagendo kutoka Misri kupitia mahandaki yanayounganisha Gaza na rasi ya Sinai.

Lakini idadi kubwa ya silaha hizo ziko katika ukanda wa Gaza , ambapo makundi ya Hamas na Islamic Jihad yana viwanda vinavyotengeneza silaha hizo.

Israel na wataalamu wa kigeni wanatarajia Iran kuhusika katika kuimarisha utaalamu wa makundi hayo ya Gaza.

Ni vigumu kubaini haswa ni silaha ngapi zinamilikiwa na Hamas.

Lakini inamiliki maelfu ya silaha tofauti . Ni wazi kwamba Israel inajua kuhusu suala hilo lakini haitaki kulizungumzia.

Kile ambacho msemaji wa wizara ya ulinzi anaweza kusema ni kwamba Hamas inaweza kuendelea kufanya mashambulizi kwa kipindi cha muda mrefu sana."

Hamas ina idadi kubwa ya roketi , kwa mfano ina kombora la masafa mafupi kama vile Qassam linaloweza kuruka umbali wa kilomita 10 na Quds 101 lenye uwezo wa kuruka kilomita 16 ,Grad linaloweza kuruka umbali wa kilomita 55.

Lakini Hamas lina roketi nyengine kama vile M-75 ambayo ina uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 75 na Fajr linaloweza kuruka umbali wa kilomita 100.

Pia wana roketi ya R-160 ambayo inaweza kuruka umbali wa kilomita 120 na M -302 ambayo inaweza kurushwa kwa umbali wa kilomita 200.

Ni wazi kwamba Hamas ina silaha ambazo zinaweza kushambulia mji wa Tel Aviv na Jerusalem na zinaweza kufika umbali wa pwani ya taifa hilo, eneo ambalo idadi kubwa ya Waisraeli huishi, mbali na majumba muhimu na ofisi za serikali.

Wizara ya ulinzi nchini Israel inasema kwamba zaidi ya roketi 1000 zilizorushwa nchini Israel katika kipindi cha siku tatu zilizopita , takribani roketi 200 zimeshindwa kupaa kutoka ukanda wa Gaza.

Wizara hiyo pia imesema kwamba silaha ya Iron Dome imefanikiwa kutungua asilimia 90 ya roketi ambazo zilifika Israel.

Lakini kumekuwa na uharibifu katika mji wa Ashkelon, ambapo roketi zimefanya uharibifu kwasababu silaha za Iron Dome hazifanyi kazi.

Mwanga mkubwa umekuwa ukionekana huku silaha ya Iron Dome ikitungua roketi zinazorushwa kutoka ukanda wa Gaza kuelekea Israel kama inavyoonekana katika eneo la Ashkelon Israel.

Vita hivi vya Israel na Palestina havitamfaidi mtu yoyote.

Lakini kutokana na kwamba mataifa ya Kiarabu yanajaribu kuweka makubaliano ya amani na Israel huku Wapalestina wakiwa wamegawanyika ni vigumu kupata suluhu ya mzozo huu katika siku za hivi karibuni.