Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Adolf Hitler: Kutoka ubabe wa kuitikisa dunia, kukaa mafichoni mpaka kujiua kwa risasi
Baada ya Aprili 25, 1945, lengo pekee la Hitler maishani mwake lilikuwa kutayarisha kifo chake.
Aprili 25, alimuita mlinzi wake, Heinz Linge, na kusema, "Nitajipiga risasi. Kisha uchukue mwili wangu na kuupeleka katika bustani ya ofisi na uuchome moto. Baada ya kifo changu. Hakuna ambaye anastahili kuniona au kunitambua. Na baada ya kufanya hivyo utarejea kwenye chumba changu." Chukua sare zangu, karatasi yangu na kila kitu ambacho nimekitumia na uvichome moto. Lakini usishike rangi ya mafuta ya Frederick Mkuu. Itamtoa dereva wangu salama Berlin baada ya kifo changu."
Akielekea mwisho wa maisha yake, Hitler aliishi katika handaki lililokuwa fiti 50 chini ya ardhi. Alikuwa akienda tu kwenye bustani ya ofisi akiwa anatembea na mbwa wake aliyempenda kweli, Blondie.
Hitler alikuwa nani?
Hitler alikuwa akilala saa kumi na moja au saa kumi na mbili asubuhi na kuamka mchana. Msaidizi binafsi wa Hitler, Troudy Junga, alikuwa akiishi chini ya handaki na Hitler hadi dakika za mwisho maishani mwake.
Akizungumza na BBC, kuna wakati alisema, "Siku 10 za mwisho zilikuwa mbaya zaidi kwetu. Tulikuwa tumejificha chini ya handaki na jeshi la Urusi lilikuwa linatukaribia. Tulikuwa tunasikia sauti za milio ya risasi, mabomu na bunduki. Hitler alikuwa chini ya handaki ameketi akiwasubiri lakini jambo moja lililokuwa limewekwa wazi ni kwamba ikiwa hawatoshinda vita, hawatawahi kuondoka Berlin na badala yake, watajipiga risasi kwa mikono yao wenyewe, kwahiyo, tulijua kile ambacho kingetokea."
"Aprili 22, 1945, Hitler alipotuambia kuwa tunaweza kuondoka Berlin kama tunataka, mchumba wake Eva Brown alikuwa wa kwanza kusema, 'Unajua kuwa siwezi kuondoka nikuache peke yako. Nitasalia hapa hapa.' Na maneno hayo hayo ndio yaliyonitoka mdomoni mwangu."
Hitler alibadilika
Albert Speer, Waziri wa Hitler aliyesimamia vita wakati huo, alikwenda chini ya handaki kukutana naye na kumuaga. Spear anasema wakati huo tabia za Hitler zilikuwa zimebadilika kabisa.
"Siku za mwisho za Hitler, hali yake ilivyokuwa hungetaka kumfanyia chochote zaidi ya kumpenda tu. Ungetamani umkumbatie tu. Mwili wake wote ulikuwa unatetemeka na mabega yake yalikuwa yamepinda. Nguo zake zilikuwa chafu lakini cha msingi zaidi majibu yake yalikuwa yamepoa. Sio Hitler yule. Nilikuwa nimeenda kumuaga. "Nilijua hiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa sisi kuonana lakini hawakusema lolote ambalo lingeniumiza moyo."
Robert Payne, mwandishi wa kitabu 'The Life and Death of Adolf Hitler', alielezea hali ya Hitler wakati huo. Aliandika, "Uso wa Hitler wote ulikuwa umefura, wenye makunyazi. Nuru ya maisha katika acho yake ilikuwa imefifia. Kile ambacho kinakumbukwa haswa kuhusu vile alivyokuwa, alikuwa akitembea huku anayuba yuba kama mlevi. Ndani ya mwezi mmoja, alikuwa I kama ameongeza miaka 10."
Siku ya mwisho chini ya handaki, Hitler aliamua kumuoa Eva Brown. Kipindi cha maisha na kifo cha Adolf Hitler, Robert Payne aliandika, "Swali likawa ni nani atakayefungisha ndoa hiyo?."
Goebbels akakumbuka aliyemuoza Walter Wagner. Tatizo likawa kumtafuta. Haikuwa rahisi. Lakini mwisho akapatikana ila kwa bahati baya, akawa amesahau kubeba cheti cha ndoa na kulazimika kukifuata."
Harusi ya Hitler
"Sherehe ya harusi ilikuwa karibu kuanza. Goebbels akatia saini kama shahidi wa Hitler huku Bormann akiwa shahidi wa Eva Brown. Tarehe katika cheti cha harusi ni Aprili 29. Lakini tarehe hiyo haikuwa sahihi kwasababu ilikuwa ni saa sita na dakika 25 usiku, kwahiyo tarehe hiyo ilitakiwa kuwa Aprili 30 "
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Bormann, Goebbels, Magda Goebbels, Jenerali Crabbs, Jenerali Bergdorf, wasaidizi wawili wa Hitler na mpishi wake wa mbogaboga.
Kila mmoja akatakia Eva Hitler afya njema. Evan alikunywa mvinyo mwingi lakini Hitler alikunywa kidogo tu a kujikumbusha. Pia alikuwa anakumbuka harusi ya Goebbels.
Lakini ghafla hali ya Hitler ikabadilika na akasema, "sasa sherehe imeisha. Kila mmoja aliingiwa na hofu."
Siku ya mwisho ya maisha yake, Hitler alilala kwa saa kidogo tu na akaamka kuoga na kujiweka sawa. Inasemekana kuwa baada ya kujiweka safi, Hitler alikutana na wanajeshi wake na kusema inaonekana mwisho unakaribia.
Wanajeshi wa Muungano wa Usovieti wanakaribia kuvamia handaki lao muda wowote ule.
Hitler alijipiga risasi
Robert Payne anasema, "Hitler alimpigia simu Profesa Hussein na kumuuliza ikiwa vidongee vya kujitoa uhai vinapatikana. Hitler akamuagiza pia kumlisha mbwa wake vidonge vivyo hivyo akiwa anavifanyia majaribio. Baada ya kufanya majaribio, Hussein alimuarifu Hitler kuwa majaribio yamefanikiwa. Mbwa wake Blondie aliaga dunia ndani ya sekunde kadhaa."
"Hitler mwenyewe hakuweza kutazama tukio la mbwa wake kufariki. Na baada ya kifo chake, alimuweka Blondie na paka wake sita kwenye kasha ambalo lilipelekwa katika bustani ya ofisi. Paka wake walikuwa bado wanamshikilia mama yao.
Saa nane unusu mchana, Hitler aliketi na kula chakula chake cha mwisho. Otto Gwensche aliagizwa kupeleka lita 200 za petroli. Akajaza mitungi petroli na kuiweka mlango wa nje ya handaki.
Ian Kershaw, aiyeandika kuhusu sifa za Hitler: "Gwensch alimuita bingwa wa Hitler Eric Kampkana. Kampka akacheka. Alijua kuna kiwango gani cha petroli katika uwanja wa ofisi. "Huu sio muda wa kucheka," Gwenshe akasema. Kampaka alifanikiwa kuweka lita 180 pekee za petroli."
Na baada ya chakula chake cha mchana, hatimaye, Hitler aliamua kutembelea wanajeshi wake. Akasalimiana nao bila kuangalia nyuso zao. Wakati huo alikuwa ameandamana na mke wake, Eva Brown.
Eva alikuwa amevaa gauni la rangi ya buluu iliyokolea na viatu aina ya buti. Alikuwa amevaa saa ya platinamu mkononi mwake. Na kila mmoja wao akaenda kwenye chumba chake. Hapo ndipo msaidizi wake binafsi Magda Goebbels alipopiga kelele huku akisema Hitler hastahili kujitoa uhai. Akauliza ikiwa anaweza kuruhusiwa kuzungumza na Hitler, atafanikiwa kumshawishi.
Hitler hakuonana na yeyote yule
Gerhard Bolt ameandika kwenye kitabu chake cha 'In the Shelter with Hitler', "Msimamizi wa Hitler Gwenshe alikuwa na urefu wa fiti 6 na inchi 2 na alikuwa kama sokwe. Magda alilazimisha kumuona Hitler kiasi kwamba Gwenshe akaamua kufungua mlango.
Gwenshe akaamuliza Hitler, 'Je ungependa kumuona Magda?' Hitler akasema, 'Sitaki kumuona yeyote.' Eva hakuwepo eneo hilo. Pengine alikuwa bafu kwasababu kulikuwa na sauti ya maji kutoka ndani. Baada ya hapo, wakafunga mlango."
Heinz Linge, ambaye alikuwa amesimama nje ya mlango, hakujua kuwa Hitler alikuwa amejipiga risasi. Alihisi harufu ya ungaunga wa bunduki.
Roxas Mitch alikuwa mtengenezaji simu katika handaki la Hitler.
Akizungumza na BBC miaka michache iliyopita, alisema:"Ghafla nikasikia mtu anapiga mayowee, 'Linge akasema kwa sauti... Hitler hayupo tena duniani. Pengine walisikia milio ya risasi. Lakini sikusikia lolote.' Wakati huo huo, katibu binafsi wa Hitler Borman akawa amemuarifu kila mmoja.
Kila moja alikuwa ananong'ona na Borman akaashiria kufungua mlango wa chumba cha Hitler, na nikaona kichwa cha Hitler kikiwa kimelala juu ya meza.
Alivyokuwa, huenda alifariki dunia akiwa ananyoosha mkono wake, kopo lililokuwa na maua kando yake lilikuwa limeanguka na kupasuka. Siwezi kusahau nilichokishuhidia."
Mwili wa Hitler ulivyochomwa moto
Linge akaufunga mwili wa Hitler kwenye karatasi na kuutoa kutumia mlango wa dharura na kuupeleka bustani ya ofisi. Bormann akauleta mwili wa Eva Brown.
"Walipoubeba mwili wa Hitler na kuupitisha karibu na mimi, miguu yake ilikuwa inalewa lewa. Mtu moja akapiga kelele, 'Njooni huku juu, wanachoma mwili wa bosi.' Lakini mimi sikwenda ju
"Moto ulipokuwa unazima, miili yao ikanyunyiziwa petroli. Moto ulikuwa umewaka kwa saa mbili unusu. Na kufikia saa tano usiku, Gwensche aliwatuma wanajeshi kuzika miili hiyo iliyokuwa imechomeka. Siku chache baadaye, wanajeshi wa Muungano wa Usovieti walipofukua mabaki ya miili ya Hitler na mke wake, kila kitu kilikuwa kimeisha." Kukapatikana jino. Mtu aliyekuwa daktari wa meno wa Hitler tangu mwaka 1938 akathibitisha kwamba jino hilo ni la Hitler." u."