Washambuliaji wa mtandaoni wanasema ni dhambi kuasili mtoto mweusi Urusi

Ekaterina na mwanawe aliyemuasili

Chanzo cha picha, COURTESY EKATERINA FROLOVA

Maelezo ya picha, Ekaterina na mwanawe aliyemuasili

Hadithi ya kuasili mtoto wake ilianza kwa furaha , lakini ikazongwa na nyakati za kutisha kutokana na watumizi programu ya kutuma ujumbe ya Telegram walioanza kumtishia.

Ekaterina Frolova aliamua kuasili mtoto mdogo baada ya kumuona katika picha ndani ya nyumba moja ya mayatima.

''Nilijua kwamba mvulana huyo hakufaa kuishi katika nyumba hiyo, kwasababu wasingeelewa'', anasema.

Eketerina ni msusi katika rasi ya Kamchakta eneo lililo na milipuko mingi ya volcano mashariki mwa Urusi.

Alikuwa na hamu ya kuasili mtoto na hatimaye alifaulu , alipokutana na mtoto huyo na alihisi kana kwamba kuna uhusiano maalum kati yake na yeye.

''Mvulana huyo alinyoosha mkono na kujaribu kufanya kana kwamba amenijua kwa muda mrefu. Hilo lilifanyika muda tu baada ya mlipuko wa virusi vya corona kuzuka na kuanza kuathiri watu''.

Ekaterina alitaka kuigawa furaha yake , mbali na kutaka kuwa na mwenzake na ndiposa akaanzisha akaunti ya Instagram kwa niaba ya mwanawe mpya.

Lakini akaunti hiyo iliokuwa na picha nyingi za mvulana huyo ilimfanya kutafutwa na kushambuliwa vibaya na makundi ya mtandao wa Telegram.

''Sikujiandaa kukabiliana na chuki niliyokutana nayo mtandaoni. Ni 'dhambi' kulingana na washambuliaji wake kuasili mtoto mweusi.

Upendeleo na Chuki

Telegram ina zaidi ya wafuasi milioni 500 na inamilikiwa na raia wa Urusi Pavel Durov.

Ukurasa wa Instagram katika simu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ukurasa wa Instagram katika simu

Mbali na hayo, vitendo vyake vya kutuma ujumbe kati ya watu, ni mtandao unaoweza kuwafikia watu wengi zaidi.

Kwa sababu hiyo na kukataa kwake kugawa data ya watumiaji wake na serikali, Telegram imekuwa ikitumiwa kuandaa maandamano kama yale yalioonekana Belarus, Iran na Hong Kong.

Lakini, kampuni hiyo inashutumiwa kwa kutochukua hatua kali kukabiliana na mitandao ya watu wenye itikadi kali wanaohusishwa na kundi la Islamic aState au maandamano ya Capitol nchini Marekani mwezi Januari mwaka huu kwa mfano.

Nchini Urusi unyanyasaji uliosambaa miongoni mwa watumiaji wengi wa mtandao huo umeripotiwa kuhatarisha Maisha ya wanawake wengi.

Mwezi Januri 2021, Mtandao wa telegram ndio uliopakuliwa sana duniani kwa wiki chache.

Wasimamizi wa Telegram

"Walianiambia kwamba watu weusi hawaishi kwa muda mrefu nchini Urusi'', alisema Eketerina , akielezea jinsi wanachama wa mtandao mmoja wa Telegram kwa jina The Male State ulianza kampeni dhidi yake.

Anadai kwamba hupokea jumbe za kumtisha kila siku. Mbali na hilo, anadai kwamba walionya kumfunga na mwanawe katika farasi na kuwawacha katikati ya barabara.

Ekkaterina na mtoto wake

Chanzo cha picha, COURTESY EKATERINA FROLOVA

Pia walimwambia kwamba wawili hao wanafaa kufungwa katika magari mawili yanayoenda njia tofauti ili kuwaua.

"Lakini kitu cha kutisha zaidi ni wakati walipochapisha maelezo kuhusu mahali wanapofanya kazi kwa wanachama wote wa mtandao huo kuona''.

Eketerina anaelezea kwamba mwanzilishi wa kundi la Male State hutengeneza mabango ya wanawake walio katika uhusiano na watu weusi .

Ijapokuwa yeye huchapisha wazi machapisho yenye ubaguzi na unyanyasaji, mama huyo anasema kwamba hakuweza kupata majibu yoyote kuhusu hilo kutoka kwa wasimamizi wa Telegram.

Waanzilishi wa mtandao huo pia hawakujibu kuhusu mahojiano yalioitishwa na BBC.

Makundi ya wahalifu katika maeneo mbalimbali duniani yamekuwa yakitumia telegram kutekeleza uovu wao

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Makundi ya wahalifu katika maeneo mbalimbali duniani yamekuwa yakitumia telegram kutekeleza uovu wao

Eketerina sio mwanamke wa pekee anayedai kwamba makundi hayo ya Urusi yanayotumia Telegram humtumia ujumbe wa kumtisha.

Wanaharakati na wanamitindo ,pamoja na wanawake walio katika tabaka la chini pia wameripoti kuathiriwa na makundi hayo.