Bill Gates: Wafahamu Mabilionea wengine waliotalakiana

Chanzo cha picha, Getty Images
Bill na Melinda Gates wametangaza kwamba wanatalakiana baada ya ndoa yao ya miaka 27 iliyowapa watoto watatu.
Kupitia ujumbe katika twitter wamesema: "Baada ya kufikiria sana na kufanya kazi nyingi juu ya uhusiano wetu, tumefanya uamuzi wa kumaliza ndoa yetu," wawili hao walisema katika ujumbe wa twitter .
Walikutana kwa mara ya kwanza miaka ya 1980 wakati Melinda alipojiunga na kampuni ya Bill ya Microsoft.
Wanandoa hao mabilionea wana watoto watatu na kwa pamoja wanaendesha Wakfu wa Bill & Melinda Gates.
Bill Gates ndiye mtu wa nne tajiri zaidi ulimwenguni, kulingana na Forbes, na ana mali ya thamani ya $ 124bn (£ 89bn).
Alipata pesa kupitia kampuni aliyoianzisha miaka ya 1970, Microsoft, kampuni kubwa ya programu ulimwenguni.
Wawili hao walichapisha taarifa hiyo wakitangaza talaka yao kwenye Twitter.
"Katika kipindi cha miaka 27 iliyopita, tumewalea watoto watatu wa ajabu na kujenga wakfu ambao unafanya kazi ulimwenguni kote kuwezesha watu wote kuishi maisha yenye afya, yenye tija," ujumbe huo ulisema
Lakini Bill na Melinda sio matajiri pekee ulimwenguni kutalakiana . wengine ambao waliachana baada na kugonga vichwa vya habari walipotoa tangazo hilo ni mabilionea hawa watano .
1. Jeff Bezos na Mackenzie Bezos, 2019
Bilionea mwingine aliyetangaza hivi karibuni kutalikiana na mke wake ni Mackenzie Bezos. Wakati taarifa ya talaka ya Bezos iliposambaa kwenye mitandao ya kijamii, mara moja vyombo vya habari vilianisha ni kwa jinsi gani watakavyogawana mali yeye na mkewe.

Chanzo cha picha, Reuters
Kiwango hicho kilikuwa ni cha asilimia 4% za hisa za kampuni yake ya mauzo ya mtandaoni -Amazon, ambayo kwa ina hisa ya dola bilioni 35 . Sio hiyo tu, wakati alipopokea kiasi hicho cha fedha, Mackenzie alikuwa mwanamke wa tatu tajiri zaidi duniani.
Hii ilimaanisha wakati huo kuwa , Jeff sio tajiri tu mwanaume mwenyewe tu bali ni ni mwanaume ambaye talaka yake ilimuwezesha mke wake kuwa mwanamke wa tatu tajiri zaidi duniani.
2. Alec Wildenstein na Jocelyn Wildenstein, mwaka 1999
Kabla dunia haijatangaziwa kuhusu talaka ya Bezos, talaka ya Wildenstein, iliyotokea mwaka 1999, ilikuwa ndio talaka kubwa zaidi ya bilionea kuwahi kushuhudiwa Alec Wildenstein, Mfanyabiashara Mfaransa- Mmarekani na muuzaji wa zana za usanii, alimtaliki mke wake wa miaka 21 , Jocelyn Wildenstein.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mgawanyo wa mali kutokana na talaka hiyo ulimpatia mke wake, mali ya thamani ya dola bilioni 2.8. Zaidi ya hayo, sheria ilisema pia kwamba atakuwa akilipwa dola milioni 100 kila mwaka kwa miaka 13 baada ya talaka. Kwa ujumla alipata dola bilioni 3.8
3. Bill na Sue Gross, 2016
Moja wapo ya talaka iliyokuwa mbaya sana katika orodha hii ni talaka ya Bill Gross, muasisi wa usimamizi wa mali -Pimco, ambayo ilikuacha katika hali inayoendelea kuwa mbaya ya kifedha na kiakili.

Chanzo cha picha, Forbes
Sue Gross, aliwasilisha kesi ya talaka mwaka 2016, na kuachana naye rasmi mwaka mmoja baadaye akiwa na utajiri mkubwa, ikiwemo nyumba ya kifahari ya ufukweni katika eneo la Laguna, ambayo ilikuwa na thamani ya dola milioni 36 million pamoja na mchoro wa "Le Repos", Picasso uliochorwa mwaka 1932, ambao aliuuza kwa kiwango hicho cha fedha.
Miongoni mwa mali alizotaka kuzitunza, Bill alitaka apewe haki ya kumtunza paka mmoja kati yap aka wao watatu , lakini hata huyo alipewa Sue. SMara moja , Bill alipoteza nafasi yake katika watu 400 tajiri zaidi katika orodha ya The Forbes mwaka 2018, baada ya kuwa katika orodha hiyo kwa miaka 14 mfulurizo.
4. Rupert Murdoch na Anna Torv, mwaka 1999
Tajiri wa vyombo vya habari Rupert Murdoch na mwandishi wa habari Anna Torv alikuwa ni mojawapo ya talaka 'zilizopangwa' vyema kuwahi kushuhudiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Walioana kwa miaka 31 na walikuwa na watoto watatu pamoja lakini waliamua kuachana baada ya kustaafu kwa Murcdoch katika ulimwengu wa dunia.
Wakati alipotangaza kustaafu kwake mwaka 1998, wawili hao walikubaliana kutalikiana katika mwaka uliofuata. Wakati taarifa hii ya kutalikiana kwao ilipoenea na kutoweka kwa taarifa kuhusu kugawana kwa mali zao, tetesi zilitokea kwamba Anna Torv alipokea dola bilioni 1.17.
Lakini kutokana na kwamba talaka hiyo ilikuwa imepangwa kwa haki, Murdoch alimuoa Wendy Denn, siku 17 baada ya talaka , na Torv nae akioana na William Mann miezi sita baadaye.
5. Harold Hamm na Sue Ann Arnall, mwaka 2015
Talaka ya bilionea huyu, ilizingirwa na kesi iliyogubikwa na machungu yaliyodumu kwa miaka mitatu (2012-2015).

Chanzo cha picha, Getty Images
Hatimaye, katika mwaka 2015, Harold Hamm alijaribu kumaliza kesi kwa kuandika hundi ya pesa alizomgawia Ann.
La kushangaza, Sue Ann alikubali . Hatahivyo, mwaka 2015, Sue aliwasilisha kesi ya rufaa na kudai apewe sehemu kubwa ya 75% ya umiliki wa vyanzo vya mali zao.
Rufaa hiyo ilikataliwa kwa misingi kuwa Sue Ann alikubali pesa alizopewa awali za hundi iliyowekwa mapema. Jambo la kushangaza, alitumia pesa zake katika kudhamini kamati ya siasa ambayo haikukaa kutoa hukumu juu ya kesi ya talaka.












