Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 01.05.2021:Messi, Haaland, Sterling, Grealish, Rabiot, Abraham, Torreira

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, atasaini mkataba mpya Barcelona ambao utakuwa na punguzo, ili kuwawezesha kufikia amlengo ya kumpata pia Erling Braut Haaland wa Borussia Dortmund. Barca wamemwambia Messi wako tayari kuanza kujadiliana kuhusu mshambuliaji huyo wa Norway, 20. (Eurosport)
Manchester City wako tayari kumuuza mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26,katika majira ya joto ili kusaidia fedha za kuwasajili Haaland wa Borussia Dortmund na kiungo wa kati wa England na Aston Villa Jack Grealish, 25.(Football Insider)
Wakala wa mchezaji Haaland, Mino Raiola amesema Real Madrid wanauwezo wa kumsajili mshambuliaji Erling Haaland katika msimu wa majira ya joto licha ya madai ya rais wa kilabu Florentino Perez hawawezi kumsajili mchezaji huyo (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Reuters
Barcelona wamefanya mawasiliano na Paris St-Germain ili wamrudishe Mbrazil Neymar, 29, kwenye uwanja wa Nou Camp. (RAC1, via Sport - in Spanish)
Chelsea wamepania kuikabili Barcelona kwa usajili wa Adrien Rabiot kutoka Juventus msimu huu wa joto, huku kiungo wa Ufaransa, 26, mchezaji huyu akipatikana kwa pauni milioni 17.(Calciomercato - in Italian )

Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham, Aston Villa na Newcastle ni miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa na mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 23, huku Chelsea ikiwa tayari kupokea pauni milioni 40 msimu huu wa joto.(ESPN)
Kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira, 25, hatarudi kwa msimu wa pili kuitumika Atletico Madrid kwa mkopo lakini angependa kujiunga na Boca Juniors. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Leicester, AC Milan na Wolfsburg wanamfuatilia wa Le Havre wa Guadeloupean Josue Casimir, 19. (Foot Mercato - in French)

Newcastle inaweza kufanya harakati za kusajili wa kiungo wa Huddersfield Lewis O'Brien, 22, ikiwa ni njia mbadala ya kuziba nafasi ya kiungo wa Arsenal Joe Willock, 21 anayecheza hapo kwa mkopo (Sun)
Wakati huo huo, Newcastle inataka kuipiku Celtic kwa kumsaini ya kiungo wa Crystal Palace na Jamhuri ya Ireland James McCarthy, 30. (Teamtalk)
Aston Villa itasajili beki mpya wa katikati msimu huu wa joto kama sehemu ya kujihami, na klabu hiyo inahitaji kumtoa beki Bjorn Engels, raia wa Ubelgiji (Football Insider)
Juventus inatarajia kufanya mazungumzo ya kumuuliza Massimiliano Allegri, 53, kurudi kuchukua nafasi ya kocha mwenzake wa Italia Andrea Pirlo, 41. (Gazzetta dello Sport - in Italian, subscription required)

Mahitaji ya mshahara wa Arturo Vidal yamekwamisha majadiliano juu ya uwezekano wa kuhama kutoka Inter Milan kwenda Marseille kwa kiungo huyo wa Chile, 33. (Calciomercato - in Italian)
Mshambuliaji wa Uhispania Lucas Vazquez anakaribia kukubali mkataba mpya na Real Madrid, licha ya Bayern Munich na Paris St-Germain kutoa ofa kwa mchezaji huyo wa miaka 29, ambaye amemaliza mkataba msimu huu wa joto.(AS - in Spanish)













