Kimbunga Jobo chatoweka baada ya kuwasili pwani ya Tanzania

Chanzo cha picha, ACCUWEATHER
Hofu iliyokuwa imewakumba wakazi wa mikoa ya Kusini hasa iliyopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pamoja na mji wa Dar es salaam imepungua kwa kiasi kikubwa baada ya Kimbunga Jobo kiichotarajiwa kuwasili nchini Tanzania kutoweka.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imesema kwamba Kimbunga Jobo kilichotarajiwa kuathiri pwani ya Tanzania kimetoweka na hakipo tena.
Kulingana na taarifa ya mamlaka hiyo Kimbunga hicho kilichokuwa kikiendelea kupunguza nguvu zake kilififia wakati kilipowasili katika nchi kavu ya pwani ya Tanzania.
Taarifa ya mamlaka hiyo iliodai kuwa ya mwisho kuhusu kimbunga hicho, ilisema kwamba Jobo kilipoteza nguvu usiku wa kuamkia siku ya Jumapili tarehe 25 mwezi Aprili.
Hali hiyo ilisababishwa na kuendelea kuimarika kwa upepo kinzani wakati kimbunga hicho kilipokuwa kikielekea pwani ya Tanzania kutoka maeneo ya Mtwara na mji wa kibiashara wa Dar es Salaam.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Afisa aliyekuwa akitoa tangazo hilo alisema kwamba: Kwasasa Kimbunga hafifu Jobo hakipo katika nchi yetu na hakuna madhara ya moja kwa moja yanayotarajiwa.
Hatahivyo aliongezea kwamba mawingu ya mvua yaliokuwa pamoja na kimbunga hicho yameenea baharini karibu na kusini mwa pwani ya Tanzania na taifa la Msumbiji kwa jumla.

''Tunaweza kuona kwamba masalia ya kimbuga jobo bado yanaendelea kuleta hali ya mawingu katika maeneo ya ukanda wa pwani hali ambayo inaweza kusababisha mvua hususan katika mikoa hii ya upande wa pwani'', alisema
Aliongezea kwamba wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa .
Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho kilitarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutua Tanzania tangu mwaka 1952.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Ripoti zilizotolewa Alhamisi iliopita zilisema kimbunga hicho kilionekana kaskazini mwa Madagascar kikiwa na kasi ya kilomita 83 kwa saa.
Utabiri ulionyesha kuwa kimbunga hicho kilipitia Ushelisheli Aprili tarehe 22 kikiwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa na kilitarajiwa kutua Tanzania Aprili 24 au 25.












