Chad baada ya Idriss Déby: Muungano wa Afrika wataka utawala wa kijeshi uishe huku jeshi likiwa na mgawanyiko

Chanzo cha picha, AFP
Muungano wa Afrika umetoa wito wa kumalizika kwa utawala wa kijeshi nchini Chad, ambako rais wake aliuliwa na waasi.
Baada ya kifo chake mara moja jeshi lilitangaza kamba mwana wa kiume wa Idriss Déby ataongoza baraza la mpito kwa miezi 18 , kabla ya uchaguzi kufanyika.
Koloni la zamani la Chad, Ufaransa, ambalo lina ngome kubwa ya jeshi nchini Chad, lilionekana kuuunga mkono hatua ya mwanae Deby kunyakua mamlaka kama njia ya kuleta "utulivu" wakati wa "hali zisizo za kawaida".
Vyama vya upinzani pia vimelaani kile walichokiita "mapinduzi nasaba ".

Chanzo cha picha, Getty Images
Muungano wa wafanyakazi umeitisha maandamano ya watu wote , huku kundi la waasio likisema Chad "sio ufalme "
Baraza la amani na usalama la Muungano wa Afrika lilielezea "hofu ya hatari kubwa " kuhusu jeshi kuchukua mamlaka na kumuweka madarakani Jenerali Mahamat Déby Itno uongozini na kuvunjwa kwa bunge.
Wajumbe 15 wa baraza la usalama la AU walijadili hali nchini Chad Alhamisi lakini lilisubiri hadi kufanyika kwa mazishi ya Déby Ijumaa kutoa taarifa yake.
Lilisema yanapaswa kurejeshwa kwa raia "haraka".
Unaweza pia kusoma:
Kulingana na katiba, spika wa bunge anapaswa kuchukua mamlaka ya nchi inapotokea kwamba rais anafariki, na kuandaa uchaguzi..
Déby, aliyekuwa na umri wa miaka 68, alikuwa ndio tu amechaguliwa kuhudumu kwa muhula wa sita madarakani wakati jeshi lilipotangaza Jumanne kwamba alijeruhiwa vibaya katika mapigano na waasi wapiganaji wa Fact fkatika jimbo la kaskazini la Kanem.
Alikuwa mshirika muhimu wa Ufaransa katika mapigano dhidi ya makundi ya Jihadi kote Afrika Magharibi na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikuwa miongoni mwa viongozi wa kigeni na maelfu ya raia wa Chad waliotoa heshima zao za mwisho katika mazishi yake.

Chanzo cha picha, AFP
Akiwa amesimama kando ya jeneza la Déby's, Bw Macron alisema: "Uliishi kama mwanajeshi, , ulikufa kama mwanajeshi ukiwa na silaha mkononi mwako. Ulijitolea maisha yako kwa Chad ili kuyalinda maisha ya wananchi wake ."
Alipokuwa Chad, Bw Macron alifanya mazungumzo na Jenerali Mahamat Déby Itno, pamoja na viongozi wa Burkina Faso, Mali, Mauritania na Niger, ambao kwa pamoja wanapambana na makundi mbalimbali ya kiislamu, ambayo baadhi yana uhusiano na al-Qaeda na mengine yenye uhusiano na kikundi cha Islamic State.

'Mgawanyiko ndani ya jeshi unaashiria mwanzo wenye utata '
Rais wa Chad alikuwa ni mmoja wa viongozi waliotawala kwa muda mrefu zaidi Afrika na mshirika wa karibu wa mataifa yenye nguvu ya magharibi, hususan Ufaransa.
Usaidizi uliotolewa kwa rais Idriss Déby -rasmi ulilenga katika vita dhidi ya makundi ya wanamgambo wa kiislamu yaliyopo Magharibi na kati barani barani Afrika-ni pamoja na ujasusi kwa jeshi la Chad ,upelelezi wa anga, na hata makati wa ulinzi wa maeneo muhimu kwa jili ya jeshi la Chad.
Uwepo wa majeshi ya kigeni haukuwahi kupokelewa vyema na watu wa Chad, hususan kutokana na kwamba walikuwa ni askari kutoka nchi ambayo koloni la zamani.

Chanzo cha picha, Reuters
Wazo kwamba Ufaransa ilizidisha kwa makusudi vurugu fulani katika eneo hilo ili kulinda maslahi yake linaaminiwa na wengi.
Lakini mgawanyiko ndani ya jeshi la Chad-ambao sehemu yao ndogo ndio wanaomuunga mkono kiongozi mpya huku waasi wakimkataa kata kata-ni jambo linaloibua wasiwasi ya kuyumba kwa usalama huku kipindi cha mpito kikianza.












