Sulawesi Indonesia: Eneo la dunia linalotambua jinsia tano

Makassar, Indonesia.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu wa Bugis ni karibu milioni 6 wengi wao wakiwa wanaishi Makassar.

Watu wa Bugis kusini mwa Sulawesi ni jamii yenye nguvu na pia inajulikana kwa kutambua jinsia tano.

Kisiwa cha Indonesia cha Sulawesi kinachofahamika kwa pweza kinaendelea kupanuka magharibi mwa bahari ya Pasifiki maeneo ya bahari ya Celebe, Molucca and Flore.

Kusini magharibi ni bandari ya mji wa Macasar, kwa kipindi kirefu imekuwa kituo kikuu cha kibiashara duniani.

Nyakati za alfajiri katika eneo la majini kuna aina za boti maalum huko Indonesia zinazoelekea bandari ya Paotere kupakua mbilimbi bahari, ngisi, na viumbe wengine wa baharini.

Chombo aina hiyo cha baharini ni cha watu wa Bugis, jamii ya mabaharia inayojulikana kwa kutambua aina tano za kijinsia.

"Jamii ya Bugis ina maneno yanayowakilisha jinsia tano," ameelezea Sharyn Graham Davies, mwana anthropolojia katika chuo kikuu cha Monash huko Melbourne, Australia.

Jamii ya Bugis ndio kundi kubwa la kikabila Kusini mwa Sulawesi. Wapo sana eneo la Makassar kwenye mashamba ya mpunga kaskazini nwa mji huo lakini ustadi wao wa ubaharia na wafanyabiashara unaonesha ushawishi wao kote Indonesia na katika funguvisiwa vya Malay pia.

Watu wenye ushawishi mkubwa

Licha ya kuwakilisha karibu watu milioni 6 pekee katika nchi yenye idadi ya watu milioni 270, Bugis wana ushawishi mkubwa sana.

Los bugis son una sociedad marinera cuya influencia se ha extendido por Indonesia y el archipiélago malayo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bugis ni jamii ya mabaharia yenye ushaiwshi mkuwa kote Indonesia na funguvisiwa vya Malay.

"Bugis ni miongoni mwa jamii yenye watu wenye ushawishi mkubwa katika eneo hilo la funguvisiwa kisiasa, kiuchumi na kitamaduni," amesema Sudirman Nasir, wa jamii ya Bugis anayefanyakazi katika afya ya umma kusini mwa Sulawesi.

Mwanaanthropolojia Sharyn Graham Davies anaeleza kuwa katika jamii ya Bugis, jinsia ya Makkunrai na Oroani ni wale wanaotambua jinsia za mke na mume.

Kwa upande mwingine, kuna calalai wale wanaozaliwa kwa maumbile ya kike lakini wanafanya kazi zinazotambulika kuwa za wanaume; wanaweza pia kuvaa fulana na suruali, wanavuta sigara, wananyoa na kufanya kazi za dhorubu.

Calabai wanazaliwa na miili ya kiume lakini wanafanya kazi za kike, wanavaa magauni, wanajipaka vipodozi na kufuga nywele.

"Idadi kubwa ya Calabai wanafanya kazi katika saluni, " amesema Neni, Calabai kutoka mji wa Segiri, kaskazini mwa Makassar.

"Pia tunasaidia katika kupanga harusi na kufanya maonesho."

Jinsia ya tano

Calabai hawaigizi wanawake, Davies anaelezea, lakini wanaonesha sifa zao ambazo zinachukiwa na wanawake wa makkunrai kama vile kuvaa sketi fupi, kuvuta sigara na kuwa na tabia za kuvutia wanaume zaidi.

Ndani ya jamii ya Bugis, watu wa Calabai na Calalai wanaweza kuchukiwa na wengi lakini wanavumiliwa na hata kuchukuliwa kwamba wana jukumu muhimu katika jamii.

Kwa ujumla, huwa hawavamiwi au kuteswa na jamii yao.

Jinsia ya tano ya jamii ya Bugis ni bissu, ambayo inachukuliwa kuwa wao sio wanaume wala wanawake lakini wanawakilisha jinsia hizo zote.

Jinsia ya bissu, kama calabai na calalai wanaonesha utambulisho wao kupitia uvaaji wao: na mara nyingi huwa wanavaa maua, nembo ya kitamaduni inayoashiria wanawake lakini pia wanabeba upanga aina ya keris unaohusishwa na wanaume.

Nacidas en cuerpos masculinos, las calabai a menudo trabajan en salones de belleza o como planificadoras de boda

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Wakiwa wamezaliwa na miili ya kama mwanamume, calabai mara nyingi huwa wanafanyakazi katika saluni au kupanga harusi.

Jinsia ya Bissu wengi wao wanazaliwa wakiwa huntha, lakini jina hilo lina athari zake zaidi ya kibaolojia.

Wakati jinsia ya Bugis mara nyingi huelezwa kuwa ni pana, bissu wanachukuliwa kuwa zaidi ya kundi hili: wanachukuliwa kuwa watakatifu, sio tu binadamu tu ambao nusu ni wanawake, nusu ni wanaume lakini pia wenye sifa za wote kwa mara moja.

"Inasemekana kuwa chimbuko lao ni mbinguni, bissu sio wanaume wala wanawake kama wengine lakini walipoumbwa walisalia kuwa wasafi kwa jinsi zote," Davies anaeleza.

Wanachukuliwa kuwa kiunganishi kwa dunia hizo mbili na kuchukua jukumu la shamans yaani kitu kitakatifu katika dini ya Bugis.