China yalalamikia 'uchokozi' wa Marekani kuhusu ujumbe iliyotuma Taiwan

Chinese J-10 fighters were among the Chinese aircraft(File image)

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais wa Marekani Joe Biden ametuma ujumbe usio rasmi wa maafisa wa zamani wa ngazi ya juu kwenda Taiwan Jumatano katika ishara ya kuunga mkono kisiwa hicho cha kidemokrasia, ambacho China inadai kuwa ni sehemu yake .

Seneta wa zamani Chris Dodd na Manaibu Katibu wa zamani wa kigeni Richard Armitage na James Steinberg wanatarajiwa kuwasili Taiwan Jumatano alasiri, wakisafiri kwa ombi la Biden, kwa kile afisa wa Ikulu aliita "ishara ya kibinafsi" ya kujitolea kwa rais kukisaidia kisiwa hicho.

"Kwa mara nyingine ziara hii inaonyesha uhusiano thabiti kati ya Taiwan na Marekani," alisema Xavier Chang, msemaji wa Rais Tsai Ing-wen wa Taiwan.

Ujumbe huo utakutana na Tsai siku ya Alhamisi.

Watu milioni 23 wa Taiwan wanaishi na tishio la uvamizi kutoka kwa China, ambayo haijafutilia mbali uwezekano wa matumizi ya nguvu kudhibiti kisiwa hicho. Beijing pia imejaribu kuitenganisha Taiwan na ulimwengu na imekuwa ikilaani juhudi za nchi zingine kudumisha mawasiliano na kisiwa hicho.

Siku ya Jumatano, ilisema mazoezi ya kijeshi yanayoendelea karibu na Taiwan yalikuwa "mazoezi ya kupigana". Siku ya Jumatatu, ndege 25 za jeshi la anga la China ziliingia katika eneo la utambulisho wa angani (ADIZ), uvamizi mkubwa zaidi ulioripotiwa na Taipei tangu Uchina ilipozidisha vitendo vyake vya kibabe baada ya Tsai kuchaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo 2016.

Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Beijing ilidai serikali ya Taiwan na wanaodaiwa kutaka 'kujitenga' walikuwa "wakishirikiana na vikosi vya nje" na wakijaribu kuyumbisha amani na utulivu.

Jeshi la la ukombozi wa Watu linaanda mazoezi halisi ya mapigano katika Mlango wa Taiwan ni hatua muhimu kuchukuliwa ili kushughulikia hali ya usalama katika Mlango wa Taiwan na kulinda uhuru wa kitaifa," msemaji Ma Xiaoguang alisema.

Rais wa Marekani Joe Biden

Chanzo cha picha, Getty Images

Ujumbe wa Marekani unazuru Taiwan kwa maadhimisho ya miaka 42 ya Sheria ya Uhusiano ya Taiwan, ambayo Biden aliiunga mkono wakati alipokuwa seneta.

Afisa huyo aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba ujumbe huo ulikuwa ukifuata "desturi ya muda mrefu ya pande mbili" na kwamba ziara hiyo - ya watu watatu wanaojulikana kuwa karibu na rais - ilikuwa "ishara ya kibinafsi" kutoka kwa Biden, ambaye alichukua madaraka mnamo Januari.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliikasirisha China kwa kutuma maafisa wakuu kadhaa kwenda Taiwan na Katibu wake wa wa masuala ya kigeni Mike Pompeo alitangaza siku chache kabla ya urais wa Trump kumalizika mnamo Januari kuwa alikuwa akiondoa vizuizi kwa mawasiliano kati ya maafisa wa Marekani na wenzao wa Taiwan.

Taiwan ni suala zito zaidi kwa China na kiini kikuu cha ugomvi na Washington, ambayo inahitajika kwa mujibu wa sheria ya Marekani kukipa kisiwa hicho uwezo wa kujilinda.