China yaonya uhuru wa Taiwan 'unamaanisha vita' huku Marekani ikiahidi kuiunga mkono

A woman holds a Taiwanese flag

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, China inaiona Taiwan kama jimbo lililojitenga

China imeonya kwamba jaribio la Taiwan ya kupata uhuru wake ''inamaanisha vita''.

Onyo hilo linakuja siku kadhaa baada ya China kuanza harakati zake za kijeshi na kupitisha ndege zake karibu na kisiwa cha Taiwan.

Hii inakuja pia baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kuahidi tena ushirikiano wake na Taiwan, na kutangaza wazi msimamo wake katika Asia.

Marekani imetaja onyo la hivi karibuni la China kuwa '' bahati mbaya ", na kuongeza kuwa wasiwasi haupaswi kusababisha "kitu chochote kama makabiliano".

China inaona Taiwan yenye demokrasia kama jimbo lililojitenga, lakini Taiwan yenyewe inajiona kama taifa huru.

"Tunaviambia hivyo vikosi vya uhuru wa Taiwan: wale wanaocheza na moto watajichoma wenyewe, na uhuru wa Taiwan unamaanisha vita ," amesema waziri wa ulinzi wa Taiwan Wu Qian katika mkutano wa waandishi wa habari.

Pia ametetea shughuli za hivi karibuni za jeshi la China, akisema zilikuwa "hatua muhimu kutatua hali ya hivi.

FILE PHOTO: An honour guard consisting of members of the Chinese navy stand in formation during a welcoming ceremony in the Great Hall of the People in Beijing November 23, 2011

Chanzo cha picha, Reuters

Presentational grey line

Uhusiano wa China na Taiwan:

  • China na Taiwan zina serikali tofauti tangu vilipomalizika vita vya China vya mwaka 1949. Beijing imekuwa ikijaribu kwa muda mrefu kudhibiti shughuli za Taiwan za kimataifa na zote zina ushawishi katika kanda ya Pacifid.
  • Uhasama umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni na Bejing iliamua kutumia nguvu kurejesha tena kisiwa hicho.
  • Ingawa Taiwan inatambuliwa rasmi na mataifa mchache tu , serikali yake iliyochaguliwa kidemokrasia ina mahusiano thabiti ya kibiashara na nchi nyingi duniani.
  • Sawa na mataifa mengi, Marekani haina uhusiani rasmi wa kidiplomasia na Taiwan, lakini sheria ya Marekani haihitaji Taiwan ijieleza juu ya mbinu za kujilinda.
Presentational grey line

Marekani ilijibu Alhamisi "Tumeona kauli ya China ni ya kusikitisha ," afisa wa habari wa Pentagon John Kirby aliwaambia wandishi wa habari, katika taarifa ya kwanza ya utawala mpya kuhusu mahusiano baina ya China na Taiwan.

Bw Kirby aliongeza kuwa Pentagon "haioni sababu kwanini uhasama kuhusu Taiwan unahitaji kusababisha kitu chochote kama makabiliano ".

Chinese President Xi Jinping (R) shake hands with U.S Vice President Joe Biden (L) inside the Great Hall of the People on December 4, 2013 in Beijing, China

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtawala mpya wa Marekani unaoongozwa na Joe Biden, alionekana hapa mwaka 2013 katika picha na Kiongozi wa Wachina Xi Jinping, unatarajiwa kuendeleza shinikizo dhidi ya China

Utawala mpya wa Marekani unatarajiwa kuimarisha shinikizo dhidi ya China kuhusu mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na haki za binadamu, mizozo ya kibiashara, Hong Kong na Taiwan , huku uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu ukiendelea kuzorota.