Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je ukanda wa Afrika mashariki na kati utanufaika vipi na ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda
- Author, Walter Nguma
- Nafasi, Mchambuzi
Jumapili ya Aprili 12, 2021 mkataba wa utekelezwaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda ulisainiwa ambapo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Musseveni walihusika katika kusaini mkataba huo wamakubaliano ya ushirikiano wa nchi hizi mbili.
Mradi huu ambao utachukua takribani kilomita 1445 kutoka Uganda mpaka Tanzania unakadiriwa kugharimu kiasi cha dola bilioni 3.5 za kimarekani.
Makampuni yanayohusika na uwekezaji katika mradi huu ni pamoja na Total ya ufaranza pamoja CNOCC ya China.
Ambapo bomba hilo lenye sehemu ya asilimia 80 ya kilometa 1445 upande wa Tanzania litajengwa na kuendeshwa na kampuni ya Bomba la mafuta likiwa ni ubia wa kampuni ya mafuta ya Uganda (UNOC) shirika la maendeleo la pentrol la Tanzania (TPDC) na kampuni mbili za mafuta, Total na (CNOCC.)
Faidi za mradi huo wa bomba la mafuta
Katika kusainiwa kwa mkataba huo zipo faidi zinazoonekana katika mradi huu mkubwa baini ya nchi hizi mbili ambazo ni;
Ajira: Katika mradi huu mkubwa wa kihistoria unaeleza kuwa utasaidia katika upatikanaji wa ajira ambazo zimekadiriwa kuwa ni Zaidi ya ajira 10,000. Katika ajira hizi 10,000 vijana wanaonekana kupewa nafasi kubwa Zaidi katika kunufaika na nafasi hizi za ajira 10,000. Ajira hizi zitapatikana katika usafirishwaji wa mabomba billion 6.5.
Unafuu wa gharama za mafuta : kupitia mradi huu utasaidia katika kupata mafuta kwa bei nafuu hasa mkizingatia hivi sasa gharama za mafuta zimeendelea kupea juu. Hivyo mradi huu utapunguza sana gharama za mafuta siyo tu kwa Tanzania na Uganda bali hata kwa nchi nyingine za Africa Mashariki.
Uwekezaji: Gharama za mafuta zinapokuwa za bei nafuu basi ni rahisi sana kuvutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza katika nchi hizi kwa nafuu ya mafuta itapelekea unafuu katika sekta nyingine hasa usafirishaji, Mradi huu ni kivutio kikubwa cha uwekezaji kwa nchi hizi mbili za Afrika mashariki.
Mahusiano mazuri kibiashara; Mradi utaendelea kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya Uganda na Tanzania, japo kumekuwa na mahusiano mazuri kwa muda mrefu lakini bomba hili litaendelea kuimarisha mahusiano mazuri ya kiuchumi kati ya nchi hizi mbili hususani kibiashara zaidi.
Mapato: Tunaambiwa katika mradi huu Tanzania itakuwa kipokea takribani dola milioni 2.6 kwa miaka 25 kwa hivyo kama pesa hizi zitakukwa zikiingia nchini basi zitakuwa na mchango mkubwa sana kwa nchi kimapato hasahasa katika ukuaji wa kiuchumi.
Ikumbukwe kiasi hiki cha dola milioni 2.6 za kimarekani zitakuwa zikilipwa kwa kila siku kwa miaka 25. Hivyo zitasaidia sana katika kupata fedha za kigeni, kuchangamsha uchumi wa nchi na vilevile zitapelekea kuongezeka kwa mzunguko wa fedha katika nchi ya Tanzania na Uganda vilevile.
Umahiri wa Tanzania katika miradi ya aina hii
Tanzania inauzoefu mkubwa sana katika shughuli za aina hii. Kumbuka Tanzania wana mabomba haya ya mali ghafi kama lile la Zambia la mwaka 1986 ambalo linasafirisha mafuta kutoka Bandari ya Dar Es Salaam mpaka mji wa Ndola ambapo mafuta hayo husafishiwa na bomba hili ni maarufu kama "TAZAMA"
Tanzania wana uzoefu wa mabomba ya gesi kama lile la Songosongo hadi Dar es Salaam na lile la Mnazi Bay hadi Dar Es Saalam.
Kwa uzoefu huu Tanzania tunaamini watasimamia na kuishauri vyema Uganda katika utekelezaji wa mradi huu.
Madhara yanayotathminiwa yanaonekana wakati wa utekelezaji wa mradi
Mazingira: Wataalam wa masuala ya mazingira wamekuwa wakionyesha kuwa wakati wa utekelezwaji wa mradi huu mazingira kwa kiasi kikubwa yatapata kuathirika kwa ukubwa sana ikiwa ni pamoja ukataji mkubwa wa miti wakati wa uandaaji wa njia za upitaji wa bomba hili.
Shughuli za kiuchumi: katika utekelezwaji wa mradi huu inaonekana kwamba shughuli za kiuchumi kama kilimo zitapata kuathiriwa sana hasa kwa yale maeneo ambayo bomba hili litapita.
Pamoja na kuwa Tanzania ina uzoefu wa mabomba hayo lakini ni vyema kuangalia namna ambayo mradi huu utaweza kusaidia nchi zote za Afrika ya Mashariki ikiwa ni pamoja na Kenya, Burundi, Rwanda na nyinginezo, kwani kwa mradi huu kunufaisha nchi zote za Afrika Mashariki kutasaidia sana kuimarisha umoja wetu kama nchi majirani hususani kiuchumi.
Kwa ulazima ni vyema sasa kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuona ni kwa namna gani wanaweza kuja na sera ya kipekee inayohusu rasilimali hii adimu dunia ya mafuta ikizingatiwa kuna maeneo mengine yanaonekana kuwa na mafuta haya kama Congo tena eneo ambalo si mbali na mafuta ya Uganda yanakopatikana na Zanzibar.
Inasemekana kuwepo na mafuta haya sasa ikiwezekana waangalie ni kwa jinsi gani wanaweza kutumia bomba moja la mafuta kusafirishia kuliko kururuhusu kuwepo kwa mabomba mengi.
Na hili litasaidia kuokoa fedha nyingi, kutengeneza faida kubwa kwa haraka na kuokoa uharibifu wa mazingira.
Mradi huu ni muhimu sana kiuchumi hasa kwa Tanzania na Uganda pamoja na Afrika Mashariki kwa ujumla hivyo ili kuweza kuutekeleza vizuri ni vyema kujifunza kwa nchi zenye uzoefu mkubwa katika shughuli hizi hasa Marekani ambao mpaka 2020 wanajumla ya mabomba ya mafuta 111 na miradi mingine 25 ikiwa kwenye utekelezwaji.
Hii itatupunguzia kuingia hasara kama tulizoingia kwenye miradi mingine.
Suala la fidia kwa watu watakaopata kuathiriwa na mradi huu unapaswa kupewa kipaombele kikubwa sana kwani kumekuwa na tabia ya kutokuwapatia watu haki zao wanazo stahili pale wanapoathiriwa na miradi mikubwa kama hii.
Wakati Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza alisema kuna mambo hayajamaliziwa kuzungumzwa na hivyo akahamasisha kuwa mazungumzo hayo yakamilishwe.
Ni rai yangu kuwa ni vyema kufanya hivyo mapema kama kuna mambo bado hayajakamilika ili ipate kujulikana ni kwa namna gani mradi huu unafaida kwa nchi hizi mbili ikiwa na maana ya Tanzania na Uganda.