Iran yaapa kulipiza kisasi dhidi ya 'shambulio la Israeli' kwenye kituo chake cha nyuklia cha Natanz

Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema nchi "yake italipiza kisasi" kwa shambulio la kimtandao katika kinu chake cha kufulia nyuklia, shambulio ambalo wanaishutumu Israeri kuwa ndiyo iliyohusika.

Maafisa wa Iran wanasema mtambo huo ulihujumiwa jana Jumapili katika "shambulio la kigaidi", japo awali walipoti kukatika kwa umeme tu.

Shambulio hilo limetokea siku moja tu baada ya nyenzo mpya ya cha urutubishaji wa madini ya urani kuzinduliwa.

Israeli haijasema lolote juu ya tuhuma hizo, lakini vyombo vya habari vya nchini humo na Marekani vinaripoti kutoka kwenye vyanzo vya kijasusi kuwa shambulio hilo limetekelezwa na Idara ya Usalama wa Taifa ya Israeli, Mossad.

Vyombo hivyo vinadai kuwa athari za shambulio hilo ni kubwa zaidi ya Irani inavyoeleza. Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa kuwa itaichukua Iran mpaka miezi tisa ili kurejea kurutubisha madini ya urani kwenye kinu hicho.

Japo Israeli ipo kimya, katika siku za hivi karibuni imekuwa ikichukua tahadhari za mara kwa mara kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Tukio la hivi karibuni linakuja huku juhudi za kidiplomasia za kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 - uliotelekezwa na Marekani chini ya utawala wa Trump katika mwaka 2018 - zikiwa zimefufuliwa.

Jumamosi, rais wa Iran Hassan Rouhani alizindua matumizi ya vifaa vya kutengeneza nyuklia katika eneo la Natanz katika sherehe ambazo zilitangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa.

Vifaa hivyo vinavyofahamika kama Centrifuges vilihitajika kuzalisha urani, ambayo inaweza kutumika kutengeneza mafuta ya vilipuzi pamoja na silaha za nyuklia.

Uzinduzi wa vijfaa hivyo pia ulionesha uvunjaji mwingine wa nchi hiyo wa mkataba iliousaini wa mwaka 2015, ambao unairuhusu Iran kuzalisha na kutunza kiwango kidogo cha uruniam iliyorutubishwa kwa ajili ya kutengeneza mafuta kwa ajili nishati ya viwanda vya kibiashara pekee.

Iran imesemanini?

"They have publicly said that they will not allow this. But we will take our revenge from the Zionists."

"Mazayuni wanataka kulipiza kisasi kutokana na namna ambavyo tumepiga hatua katika kuondolewa vikwazo," Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amenukuliwa na vyombo vya habari vya serikali akisema.

"Wamesema wazi kabisa kuwa hawataruhusu sisi kuendelea na mpango huu wa nyuklia. Lakini nasi tutalipiza kisasi chetu kwa Mazayuni."

Jana Jumapili, msemaji wa Shirika la Udhibiti wa Nishati ya Atomiki nchini Iran (AEOI), Behrouz Kamalvandi, alisema "tukio" lilitokea asubuhi likihusisha mtandao wa nishati wa kituo hicho.

Bw Kamalvandi hakutoa maelezo zaidi lakini aliliambia shirika la habari la Iran -Fars kwamba "hapakuwa na majeruhi wala uvujaji ".

Baadae taarifa ya televisheni ya taifa iliyotolewa na mkuu wa AEOI Ali Akbar Salehi, elezea tukio hilo kama "hujuma" na "ugaidi wa nyuklia''.

"Ikilaani hatua hatua mbaya ya shambulio hilo , Jamuhuri ya kiislamu ya Iran ilisisitiza juu ya haja ya jamii ya kimtaifa Shirika la kimataifa la udhibiti wa nguvu za Atomiki [IAEA] kushugulikia ugaidi huu wa kinyuklia ," alinukuliwa akisema.

"Iran ina haki ya kuchukua hatua dhidi ya wahusika," aliongeza.

IAEA ilisema kuwa inatambua kuhusu taarifa za tukio lakini haikutoa kauli.

Mwezi Julai mwaka jana, pia hujuma zililaumiwa kwa moto uliowaka kwenye kiwanda cha nyuklia cha Natanz, ambako shughuli za kifaa cha centrifuge kilipigwa zinaendeshwa.

Mzozo wa nyuklia wa Iran: Maelezo ya kimsingi

  • Mataifa yenye nguvu duniani hayaimini Iran: Baadhi ya nchi zinaamini kuwa Iran inataka nyuklia kwasababu inataka kujenga mabomu ya nyuklia - lakini inakanusha haya.
  • kwahiyo mkataba ulifikiwa : Mwak 2015, Iran na nchi nyingine sita zilifikia makubaliano makuu. Iran ilitarajiwa kusitisha baadhi ya kazi zake za nyuklia na kuondolewa kwa adhabu kali, ambazo zinaumiza uchumi wake
  • Tatizo liko wapi sasa ? Iran ilianza tena kazi zake za nyuklia zilizopigwa marufuku baada ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kujiondoa kwenye mkataba na kuiwekea tena vikwazo Iran. Ingawa kiongozi mpya Joe Biden anataka kujiunga tena, pande zote mbili zinasema kila upande lazima apige hatua kwanza

Je Israeli inaweza kuwa imehusika?

Redio ya umma ya Israeli, Kan, ilinukuu vyanzo visivyojulikana vya kiintelijensia vikisema ukosefu wa umeme katika kituo cha nyuklia ulisababishwa na harakati za kimtandao za Israeli.

Gazeti la Haaretz pia lilisema tukio hilo linaweza kuwa linaweza kuchukuliwa kuwa ni shambulio la kimtandao la Israeli.

Ron Ben-Yishai, mchanganuzi wa masuala ya ulinzi katika wavuti wa habari wa Ynet, alisema kwamba huku Iran ikiendelea kujiimarisha kuelekea kuwa na uwezo wa silaha za nyuklia ni jambo la "busara kuchukulia kuwa tatizo ... huenda halikusababishwa na ajali, bali hujuma za kimakusudi zilizolenga kupunguza kasi ya nyuklia kwa mazungumzo na Marekani juu ya kuondoa vikwazo ".

Baadaye Jumapili, waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema "mapambano dhidi ya Iran na watetezi wake na juhudi za Iran za kujihami ni kazi kubwa ".

"Hali ambayo ipo leo sio lazima ndiyo itakayokuwepo kesho," aliongeza, bila kuitaja Iran moja kwa moja.

Mkataba wa nyuklia wa Iran, unaofahamika kama mpango wa kina wa uutekelezaji-Comprehensive Plan of Action (JCPOA), umekuwa taabani tangu Donald Trump alipoiondoa Marekani kwenye mkataba huo.

Chini ya utawala wa Biden juhudi za kidiplomasia zimeongezwa maradufu ili kuufufua.

Lakini Bw Netanyahu ameonya dhidi ya kurejeshwa kwa mkataba huo, na kutangaza wiki iliyopita kwamba hatofungwa na makubaliano mapya na Tehran.

Nini kilichotokea katika mkataba?

Mkataba wa nyuklia unairuhusu Iran kuzalisha na kutunza kiwango kidogo cha madini ya uranium yaliyorutubishwa cha hadi 3.67% pekee. Urani iliyorutubishwa hadi 90% au zaidi inaweza kutumiwa kutengeneza silaha za nyuklia.

Bw Trump alisema mkataba huo ulikuwa na misingi "fikra kuu za kufikirika kwamba utawala wa wauaji unataka mpango wa amani wa nyuklia tu" na akarejesha vikwazo vikali vya kiuchumi katika jaribio la kuilazimisha Iran kufanya mazungumzo ya mkataba mwingine.

Iran, ambayo inasisitiza kuwa haitaki silaha za nyuklia, ilikataa kufanya hivyo na ikalipiza kisasi kwa kukiuka ahadi zake kadhaa muhimu chini ya mkataba huo.

Tangu wakati huo imekuwa ikiharakisha uvunjaji wa mkata huo katika jaribio la kuongeza shinikizo kwa Marekani. Ukiukaji huo ni pamoja na matumizi ya vifaa vya kurutubisha madini ya uranium, ikifuua urtubishaji wa hadi 20%, na kuongea akiba ya nyenzo za nyuklia.