Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ushahidi unaoonesha jinsi jeshi la Ethiopia lilivyofanya mauaji Tigray
Uchunguzi uliofanywa na BBC Africa Eye umebaini ushahidi wa mauaji yaliyotokea kaskazini mwa Ethiopia yaliyofanywa na wanajeshi wa Ethiopia.
Ushahidi huo pia unaonesha eneo ambalo watu wapatao 15 waliuawa.
Mapema mwezi Machi, picha tano za video zilikuwa zinaangaliwa katika mitandao ya kijamii zikionesha silaha, wanaume wenye silaha wakiongoza kundi la watu wasio na silaha pembeni ya mwamba, wakiwapiga risasi baadhi yao na kutupa maiti pembezoni mwa miamba.
Shirika la utangazaji la BBC limethibitisha kuwa mauaji yalitokea karibu na mji wa Mahbere Dego kaskazini mwa Ethiopia katika ukanda wa Tigray, ambako jeshi la Ethiopia lilikuwa linapambana na wapiganaji wa Tigray wa chama cha Tigray People's Liberation Front (TPFL).
Mapigano yalianza mwezi Novemba mwaka jana wakati serikali ilipotangaza kuanzisha mapambano ya kijeshi dhidi ya TPLF, ambapo Waziri mkuu Abiy Ahmed aliwashutumu kwa kuvamia ngome ya jeshi.
Chama cha TPLF kinapinga jitihada za bwana Abiy kuongeza nguvu katika serikali shirikisho na alisema kuongeza wigo wa upinzani.
Mgogoro huo umesababisha zaidi ya watu milioni mbili kuhama makazi yao na kusababisha zaidi ya watu milioni nne kuhitaji msaada, kwa mujibu wa utawala wa mpito wa Tigray.
Picha za eneo husika
Kikosi cha uchunguzi cha BBC Africa Eye, wamefanya kazi kwa pamoja na wachambuzi kutoka na chombo cha habari cha Bellingcat na Newsy, na kuonesha jinsi mauaji yalivyotokea.
Watu wa kwanza walioweka picha za video hizo katika mitandao ya kijamii walidai kuwa walipiga picha wakiwa karibu na mji wa Mahbere Dego.
Africa Eye imeelezea eneo na vitu vilivyoonekana katika video hizo, ikiwemo barabara ya vumbi, muonekano wa eneo hilo ambao una na miamba na tabia za watu waliokuwa katika tukio hilo tofauti na picha ya satelaiti ambayo inaonesha eneo la mjini.
Muonekano wa eneo ulitumika kulinganisha na picha zilizopigwa kwa satelaiti.
Maelekezo na vivuli vya wahusika waliokuwa wamebeba silaha imeweza kusaidia kuainisha muda, mazingira yaliyopo kuwa ni Kaskazini-kusini, hivyo imewasaidia Africa Eye kubaini eneo husika.
Mstari wa juu wa picha za video ulikuwa unazuia kuonesha kwenye ramani kuwa eneo husika.
Mto ambao ulikuwa mkavu, muonekano wa majani na miti ulithibitisha kabisa kuwa eneo hilo ndio eneo husika.
BBC iliongea na mkazi wa Mahbere Dego, ambaye alisema jeshi la Ethiopia lilichukua wanaume 73 kutoka mjini na maeneo yanayowazunguka mwezi Januari mwaka huu, wakiwemo ndugu zake watatu.
Alisema hajasikia chochote kuhusu ndugu zake tangu walipochukuliwa.
BBC iliongea pia na mkazi wa kijiji cha jirani ambaye alisema kaka yake ni miongoni mwa watu waliouawa katika mauaji hayo ya kikatili.
Alisema mauaji yalifanyika katika eneo la Mahbere Dego, na alieleza mwezi huohuo wa Januari 2021.
"Waliwauawa katika miamba," alisema.
Kuwatambua wanaume wenye silaha na wahanga
Africa Eye haikuweza kuthibitisha au kutoa utambulisho wa wanaume waliokuwa wamebeba silaha walioonekana katika video hiyo, lakini sare zao zilionekana vizuri na hata beji yenye rangi ya bendera ya Ethiopia - zilionekana kufanana na hizo ambazo zinavaliwa na jeshi la ulinzi la taifa la nchi hiyo- Ethiopian National Defence Force (ENDF).
Vilevile sare zao zilifanana na sare za ENDF, muonekano wote wa vazi hilo unafanana sana, ikiwemo mitindo ya mifuko.
Wanaume wenye silaha walikuwa wanaongea lugha ya Amharic, ambayo ndio lugha rasmi nchini Ethiopia.
Katika video zote tano unaweza kuwasikia wakiongea wenyewe wakiwa wamesimama karibu na kundi la wanaume wasiokuwa na sare waliokuwa wamekaa chini.
"Tusiwaache huru hawa watu. Yani hata mmoja asibaki," ilisikika hivyo kwenye sauti ya camera.
"Lazima tupate hii video ya namna watu hawa walivyokufa," sauti nyingine ilisikika.
Taarifa nyinginr kuhusu mzozo wa Tigray:
Video nyingine nne zilionesha wanaume wasiokuwa na silaha wakinyooshewa silaha katika eneo la ukingo wa muamba, na kuonesha wanaume wenye silaha wakiwaua wanaume waliofungwa na kusukuma maiti kwa kuiangusha chini ya miamba.
Katika picha hizo za video zinaonesha wanaume hao wenye silaha wakipiga risasi maiti na walisikika wakitoa maneno ya kejeli na matusi kwa maiti.
"Natamani ningewamwagia gesi na kuwaunguza," sauti ilisikika katika moja ya video.
"Ingekuwa vyema kama kungekuwa na gesi ya kuwaunguza watu hawa," sauti nyingine ilisikia ikijibu.
"Tuwachoma kama vile Wahindi wanavyochoma maiti."
Wahanga wa mauji hayo pia hawakuweza .Walisikika wakiongea lugha ya Tigrinya, lugha ya ukanda wa Tigray.Katika video hiyo, wauaji alidhani kuwa wahanga ni wafuasi wa TPLF.
"Huu ndio mwisho wa woyane," ilisikika sauti ya mwanaume mmoja mwenye silaha akitumia kauli inayotumiwa na TPLF.
"Hatuna huruma sisi."
Laetitia Bader, Mkurugenzi wa shirika la Human Rights Watch nchini humo, aliiambia BBC kuwa kuna watu walishuhudia ukatili na unyanyasaji wa watu katika miezi ya hivi karibuni, lakini video hizi zinatushtua kuonesha wazi nini kinatok
"Tunachoona kwa wanaume hawa wasio na silaha ni kuwa wameuawa. " Hili ni tukio linalohitaji uchunguzi zaidi kwasababu kile tunachoona katika video hizi inaweza kuwa ni uhalifu wa kivita.
BBC imejumuisha ushahidi ambao iliupata kutoka serikali ya Ethiopia, ambapo taarifa inasema "Video na madai ya mtandaoni hayawezi kuchukuliwa kama ushahidi ", na kuongeza kuwa Tigray iko huru kufanya uchunguzi.