John F Kennedy: Wakati rais wa Marekani alipokutana na Mwalimu Nyerere na wapiganiaji uhuru wengine wa Afrika

Katika msururu wa barua za wandishi wa Afrika ,mwandishi wa Sierra Leone-Gambia Ade Daramy amezama na kuibuka na picha za rais wa Marekani John F Kennedy ambaye alikuwa mstari wa mbele kuanzisha uhusiano wa taifa lake na Afrika .

Kabla ya Kennedy kuwa rais mwaka wa 1961 nchi yake haikuwa imechukua hatua ya kuelewa mageuzi makubwa yaliokuwa yakifanyika Afrika

Kufikia wakati alipouawa mwaka wa 1963 tasiwra hiyo ilikuwa imebadilika sana.

Katika muda wake mfupi afisini Kennedy alikuwa amepokea kila kiongozi aliyekuwa akipigania uhuru wan chi yake katika Ikulu ya White House nahata viongozi ambao kwa wakati huo walikuwa wakiongoza nchi zao .

Mwaka mmoja kabla ya kuwa rais mataifa 17 ya Afrika yalikuwa yamepata uhuru na kwa sabau alifahamu mambo yalikuwa yakibadiliska Kennedy alikuwa ameanzisha uhusiano nao na kuanza kuyaunga mkono mataifa ya Afrika .

Sera hiyo ya uhusiano wa kidiplomasia ilidumu kwa muda mrefu isipokuwa wakati wa utawala wa rais Donald Trump ambaye hakuwa na uhusiano wa karibu sana na Afrika na hata lugha yake alipozungumzia nchi za Afrika ilisaliti msimamo wake kuhusu alivyoataka Marekani kuhusiana na nchi za Afrika.

Mtangaluzi wa Dwight D Eisenhower pia hakuwa na sifa nzuri kuhusu uhusiano wake na nchi za Afrika.

Aliamuambia rais wa Togo Sylvanus Olympio, kwamba sababu ya Marekani kuwa na balozi mmoja kuzishughulikia Togo na Cameroun ni kwa sababu hakutaka mabalozi wake 'kuishi katika mahema'

Wakati wa kampeini za uchaguzi wa mwaka wa 1960 Kennedy alikosoa utawala wa Eisenhower kwa kutelekeza maazimio ya watu wa Afrika na kwamba Marekani ilifaa kuwa upande unaopinga ukoloni.

Alipochukua uongozi Kennedy aliwaalika viongozi wa Afrika White House pamoja na Jackie Kennedy, alimsalimia kila mmoja wao akiwemo Emperor wa Ethiopia Haile Selassie na Mfalme Hassan IV wa Morocco - walipowasili nchini humo.

Pia kuwa na gwaride la heshima ,dhifa za chakula na ziara za kwenda kumbi kubwa za tamasha za muziki katika sehemu zenye historia .

Ziara hizo ziliangaziwa katika vyombo vya habari na wananchi walihimizwa kujitokeza na kushangilia.

Kulikuwa na njama ya kisiasa katika yote hayo. Muungano wa Kisovieti pia ulikuwa ukiendeleza juhudi kama hizo katika nchi za Kiafrika kwa kujitenga na Wakoloni wa zamani wa nchini hizo.

Alipoingia madarakani, Kennedy aligundua haraka umuhimu wa kuwa karibu na mataifa yanayoibuka Barani Afrika.

Kennedy hata hivyo alionekana kujitolea kabisa kuiendeleza Afrika na watu wake.

Wakati alipouawa bara la Afrika liliathiriwa sana na mauaji yake na hasa ikizingatiwa kwamba mrithi wake Johnson, hakuwa na msimamo wa kuendeleza uhusiano huo kati ya Marekani na Afrika.

Kuuawa kwa shujaa wa ukombozi wa Congo Patrice Lumumba huku shirika la CIA likishukiwa kuhusika ni kumbusho kwamba vita baridi vya wakati huo vilivyohusisha muungano wa Soviet vilikuwa pia vikiendelezwa barani Afrika.

Miaka 60 baadaye Joe Biden ameanza tena kuchonga upya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Afrika. Kupitia taarifa mapema mwezi huu alisema Marekani iko tayari kuwa 'Mshirika wa Afrika kwa kuisaidia na kunufika kwa pande zote mbili'

Maneno ya Biden yalikariri kujitolea kwa Kennedy kuboresha uhusiano huo - na sasa kinachongojewa ni iwapo vitendo vitaambatana na tamko hilo.

Picha za Robert Knudsen, Cecil Stoughton, Abbie Rowe, Picha za White House, ziliwasilishwa na Maktaba ya Rais John F Kennedy na makavazi ya, Boston