Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Paul Rusesabagina: Rwanda yakiri kuwa 'iliilipa ' ndege iliyomtoa Dubai na kumpeleka Kigali, bila kujua
Rwanda imekubali kuwa ndiyo iliyolipa ndege iliyokuwa imembeba Paul Rusesabagina, mpinzani wa utawala wa Kigali ambayo ilimtoa Dubai na kumpeleka mjini Kigali Rwanda mwishoni mwa mwezi Agosti 2020.
Kulingana na televishini ya Al Jazeera, Waziri wa sheria wa Rwanda Johnston Busingye yalikubali kuwa Rwanda iliilipa ndege hiyo, baada ya kuonyeshwa video ambapo yeye na washauri wake wa masuala ya mahusiano ya umma ambayo aliitumia televisheni ya Al Jazeera kimakosa.
"Serikali ililipa ," Busingye alimuambia mtangazaji wa kipindi cha UpFront Marc Lamont Hill.
"Kulikuwa na mtu aliyekuwa anafanya kazi na Rusesabagina kwa muda mrefu, ambaye alikuwa akifanya kazi na idara yetu ya upelelezi wa makosa ya uhalifu, ambaye alikubali kumlaghai na malipo yalitumiwa kusaidia kufanikisha kumleta Rusesabagina hadi Rwanda," aliongeza. "Serikali haikuhusika kumsafirisha. Ilimlipa huyu mwanaume aliyetaka kumleta nchini Rwanda ."
Busingye alisema kuwa serikali ya Rwanda ilitekeleza sheria wakati ilipomlaghai Rusesabagina, mwenye uraia wa Ubelgiji na Marekani, kupanda ndege iliyompeleka hadi Kigali.
Ni kwa jinsi gani mwanasiasa huyo wa upinzani alifika Rwanda bila utashi wake, ni mojawapo ya mambo yanayojadiliwa katika kesi inayomkabili, kwani yeye anadai alitekwa nyara na kufikishwa Rwanda.
Katika mazungumzo na waandishi wa habari mwezi Septemba, Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema kuwa Bw Rusesabagina ''alijileta mwenyewe''.
Taarifa ya Wizara ya afya ya sheria ya Rwanda yenye kichwa cha habari kinachosema "ufafanuzi kuhusu mahojiano na Al Jazeera", imesema kuwa baadhi ya yaliyozungumziwa katika mazungumzo hayo ya tarehe 26 mwezi wa pili "kwa upande mmoja yanatokana na sauti ya siri iliyorekodiwa ambayo haielezei sera ya serikali ".
Taarifa hiyo inasema kuwa "msimamo wa serikali ...ni kwamba kukamatwa kwa Rusesabagina kulifuata sheria ... na kwamba hakuna haijakiuka popote haki ya Rusesabagina ".
Taarifa hiyo pia inasema kuwa sheria ya Rwanda inalinda kutoingiliwa kwa mawasiliano kati ya mawakili na wateja wao, ikiwa ni pamoja na ifungo cha awali cha mahabusu, lakini vitu vyote vinavyoingia gerezani sharti vifanyiwe msako na idara ya magereza, kulingana na sheria.
Nini kilichozungumziwa katika mazungumzo na Al Jazeera?
Katika mazungumzo na mwandishi wa habari wa Aljazeera Marc Lamont Hill, Bwana Busingye alisema:
"Kulikuwa na mtu ambaye kwa muda mrefu alikuwa akifanya kazi na Rusesabagina, ambaye alikuwa anasakwa idara ya uendeshaji mashitaka nchini Rwanda, ambaye alikubali kumleta Rwanda, malipo yalikuwa ni ya kusaidia mpango wa mwanaume huyo kumchukua Rusesabagina na kumleta Rwanda.
"Serikali haikuhusika katika kummleta. Ilikuwa ni kumsaidia mwanaume huyo aliyetaka kumleta Rwanda".
Alisema : "Katika sheria za kimataifa za uhalifu, kuwalaghai watu wafike mahali ambako wanaweza kufikishwa mbele ya sheria ni jambo ambalo limewahi kufanyika katika sheria za nchi nyingi ".
Alipoulizwa iapo ni sahihi kisheria kwa Bw Rusesabagina kupelekwa Rwanda bila utashi wake , Bwana Busingye alisema : "Ndio ni sahihi".
Kabla ya mazungumzo na Al Jazeera, video hiyo inamuonyesha Waziri wa sheria wa Rwanda akishauriwa na wataalamu wawili wa taasisi ya Chelgate ya Bwongereza alipokuwa akijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari na video hiyo ilitumwa kimakosa kwa waandaaji wa kipindi cha UpFront cha Al Jazeera, kulingana na televishei hiyo.
'Mazungumzo yaliyonaswa kwenye video'
Katika video iliyotumwa kwa Aljazeera kimakosa, Bwana Busingye alikubali kuwa wakuu wa gereza walinasa mazungumzo baina ya Rusesabagina na mawakaili wake.
Akizungumza na washauri wake Bw Busingye alisema : "Kuna waraka mmoja ambao ulikuwa unaashiria kuwa alikuwa nataka kutoroka- barua hiyo ilikamatwa na wakuu wa gereza, lakini Rusesabagina alirudishiwa barua hiyo".
Al Jazeera inasema kuwa katika mazungumzo ya awali iliyofanya na Bw Busingye, alikuwa amekana kuwa wakuu wa gereza hawahusiki na mazungumzo baina ya Rusesabagina na mawakili wake. "Huongea nao kwa siri", alisema.
Baada ya kutathmini video hiyo iliyoifikia Al Jazeera kimakosa, televisheni hiyo ilisema kuwa iliomba kufanya mahojiano ya pili na na Bw Busingyeili atoe mwangaza kuhusiana na kauli zake mbili tofauti zinazokinzana.
Katika mahojiano ya pili, Waziri usingye aliunga mkono haki ya wakuu wa magereza ya kuchunguza taarifa baina ya Rusesabagina na mawakili wake, kwa misingi ya kiusalama.
"Idara ya magereza iko huru. Hufanya kazi yake kwa amani. Haya yakisha fanyika, hawana uwezo wa kutoboa siri ya yale waliyoyashuhudia ".
Alipoulizwa iwapo aliweza kupata ujumbe wa siri baina ya Bwana Rusesabagina na mawakili, alisema kuwa: "ndio, bila shaka ".
Aliongeza kuwa: "Nimesema taarifa za kisheria, lakini ujumbe kati ya mawakili na mteja wao unalindwa. Hilo nilikueleza awali ".
Unaweza pia kusoma:
Kesi ya Rusesabagina imefikia wapi?
Ijumaa Mahakama kuu ya Rwanda ilitangaza kuwa hoja zilizotolewa na Paul Rusesabagina za kupinga kuendeshwa kwa kesi yake nchini Rwanda hazina msingi.
Bw Rusesabagina na washitakiwa wenza 20 katika kesi yake wanashutumiwa kufanya vitendo vya vilivyotekelezwa na kundi la FLN vilivyosababisha vifo vya watu nchini Rwanda katika miaka ya 2018 na 2019.
Alikuwa amedai kuwa yeye sio raia wa Rwanda, na kwamba alikamatwa akafikishwa nchini Rwanda kwa njia isiyo ya kawaida na iliyo kinyume cha sheria.
Serikali ya Marekani ilitangaza kuwa imezungumza na serikali ya Rwanda kuhusu kesi hiyo.
Rusesabagina alikuwa ameomba kesi yake kama raia wa Ubelgiji, iendeshwe na mahakama ya Ubelgiji.
Hatahivyo waendesha mashitaka katika kesi yake walisema kuwa hakuna ushahidi ambao Bw Rusesabagina aliuonesha kwamba alijivua uraia wa Rwanda kwa njia inayokubalika kisheria.
Walisema kuwa kuwa na uraia wa Ubelgiji hakuna sheria inayozuia mahakama za Rwanda kuendesha kesi dhidi yake.