Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Uchina yasema haikuwapima corona wanadiplomasia wa Marekani kwa kipimo cha njia ya haja kubwa
China imekanusha kwamba ililazimisha wanadiplomasia wa Marekani kufanyiwa vipimo vya corona kupitia njia ya haja kubwa
China imekanusha madai kwamba ililazimisha wanadiplomasia wa Marekani kufanyiwa vipimo vya corona kupitia njia ya haja kubwa
IMAGE media claimed that diplomats were made to undergo the tests
China imekanusha madai ya kwamba ililazimisha wanadiplomasia wa Marekani kufanya uchunguzi wa virusi vya corona kupitia njia ya haja kubwa.
Vyombo vya habari vya Marekani vimesema kwamba wanadiplomasia walikuwa wamelalamika baada ya kulazimishwa kupitia mchakato huo.
Baadhi ya miji ya China imeanzisha uchunguzi wa virusi vya corona kwa kupitia njia ya kupitisha haja kubwa huku wataalamu wakidai kwamba kuna madai njia hiyo inaongeza uwezekano wa kubainika kwa maambukizi ya virusi hivyo. Nchi hiyo kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kudhibiti virusi hivyo vya corona.
Unaweza pia kusoma:
Msemaji wa mambo ya nje wa China Zhao Lijian amekanusha madai hayo Alhamisi, na kuelezea vyombo vya habari kwamba "China haijawai kutaka wanadiplomasia wa Marekani waliopo nchini China kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya corona kupitia njia ya kupitisha haja kubwa".
Wiki jana, gazeti la Washington Post liliripoti kwamba baadhi ya wafanyakazi walikuwa wameiambia wizara ya mambo ya nje kwamba wametakiwa kufanya uchunguzi huo.
Uchunguzi wa aina hiyo unajumuisha kuingizwa pamba urefu wa sentimita 3-5 sawa na (inchi 1.2-2.0) katika njia ya kupitisha haja kubwa na kuanza kuizungusha taratibu.
Bado haijafahamika ni wanadiplomasia wangapi wa Marekani huenda wamefanyiwa uchgunguzi wa virusi vya corona kupitia njia hiyo.
"Wizara ya mambo ya nje haikuwahi kukubali uchunguzi wa corona kupitia njia hii na tumeipinga moja kwa moja kupitia ofisi ya Wizara wa mambo ya nje baada ya kubaini kwamba baadhi ya wafanyakazi wamelazimishwa kufanyiwa," Msemaji wa wizara ya mambo ya nje amezungumza na Vice News Jumatano.
Wizara ya mambo ya nje iliongeza kwamba imearifiwa na Beijing kuwa uchunguzi huo ulifanyika kimakosa.
Unaweza pia kutazama:
China ilianzisha uchunguzi wa corona kupitia njia ya haja kubwa mnamo mwezi Januari.
Li Tongzeng, daktari wa magonjwa ya kuambukiza na kupumua nchini China aliviambia vyombo vya habari kuwa uchunguzi kwa njia hiyo unaondoa makosa ya kutobainika kwa aliyepata maambukizi ikilinganishwa na njia ya mdomo na pua.
Ingawa alisisitiza kuwa chanjo hiyo inafanyika kwa makundi fulani kama watu walio karantini.