Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Facebook na Google Australia unahusu nini?
Mzozo kuhusu sheria itakayozilazimu kampuni kubwa za teknolojia, Facebook na Google kulipia maudhui ya habari nchini Australia inafuatiliwa kwa karibu kote duniani.
Sheria hiyo ambayo itakuwa ya kwanza duniani inalenga kutatua suala la makampuni ya teknolojia ya Marekani kukosesha vyombo vya habari mapato yanayotokana na matangazo ya biashara.
Ikiidhinishwa, sheria hiyo itaathiri pakubwa makampuni ya teknolojia duniani na jinsi ya kupata habari mtandaoni.
Lakini makampuni ya teknolojia yameonekana kusalimu amri, baada ya Facebook kudhibiti maudhui ya habari nchini Australia.
Lakini mzozo huo unahusu nini?
Huenda unajiuliza mzozo huu ulifikaje hapa, lakini kwa muda mrefu kumekuwa wasiwasi kuhusu jinsi kampuni za teknolojia zinavyotawala soko la biashara dhidi ya mashirika ya habari.
Google ni maarufu sana nchini Australia na imetajwa na serikali kuwa bidhaa muhimu, ikizingatiwa jinsi inavyokabiliwa na ushindani mdogo.
Na mitandao ya kijamii ikiwa cha kikuu cha habari .
Kwa mujibu wa Ripoti ya Taasisi ya Reuters ya Habari za Dijitali 2020, asilimia 52 ya Waaustralia wanatumia mitandao ya kijamii kama chanzo cha habari. Facebook iliorodheshwa ya kwanza kama chanzo cha habari katika mitandao ya kijamii ikifuatiwa na YouTube na Facebook Messenger.
Mwaka 2018, Serikali ya Australia kupitia asasi inayodhibiti masuala ya mawasiliano ilizindua uchunguzi juu ya athari za ushindani wa Google na Facebook dhidi ya mashirika ya habari na biashara.
Uchunguzi huo uliofanywa na Tume ya kudhibiti ushindani wa kibiashara nchini Australia ulibaini ukosefu wa usawa wa uwezo kati ya mashirika ya ya kiteknolojia na mashirika ya habari.
Kutokana na hilo, Tume hiyo ilipendekeza kubuniwa kwa kanuni za maadili ambayo ilisema itasaidia kuleta usawa.
Mwezi Julai mwaka uliyopita, serikali ya Australia ilizindua rasimu ya sheria ya habari itakayowezesha kubuniwa kwa kanuni hizo, na kuzuo hofu huenda Facebook na Google zikaondoa huduma zao nchini humo.
Rasimu ya sheria ya habari inasema nini?
Rasimu hiyo inazitaka makampuni ya teknolojia kulipia maudhui, ingawa haielezi ni nini inafaa kulipiwa.
Sheria hiyo huenda ikaziwezesha mashirika ya habari kwa pamoja kushauriana na mashirika ya teknolojia ni maudhui ya aina gani itakayotumiwa na mashirika hayo hata watumiaji wakitafuta.
Wasipokubaliana, suala hilo litaamuliwa na mamlaka ya mawasiliano ya Australia na ile ya vyombo vya habari.
Watakaokiuka sheria hiyo huenda wakatozwa faini ya hadi dola milioni saba kwa kila kosa au asilimia 10 ya mapato kampuni hiyo nchini humo.
Serikali inasema kanuni hiyo ya maadili kwanza itazilenga Google na Facebook, lakini itapanuliwa ili kutajumuisha kampuni nyingine za teknolojia.
Kwa nini Australia inataka sheria hii?
Serikali inahoji kuwa kampuni kubwa za teknolojia zinastahili kulipa vyombo vya habari "haki" yao kutokana juhudi zao.
Pia imeongezea kusema msaada wa kifedha unahitajika kutolewa kwa mashirika ya habari ya Australia kwasababu vyombo imara vya habari ni muhimu kwa demokrasia.