Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ngozi Okonjo-Iweala: Mkuu mpya wa WTO atangaza mikakati yake
Mkuu mpya wa Shirikal la biashara duniani(WTO)ameiambia BBC kuwa chanjo lazima isaidie kutatua janga
Ngozi Okonjo-Iweala amesema "dhana ambapo mataifa tajiri yanawachanja watu wao na nchi masikini zinapaswa kusubiri " lazima iepukwe.
Katika wiki za hivi karibuni, nchi kadhaa zimejaribu kuzuia usafirishaji wa chanjo nje ya mipaka yake.
Lakini Dkt Okonjo-Iweala amesema kulindana kutazuia dunia kupona.
"Asili ya janga na kubadilika kwa maumbile yanayosababisa aina tofauti za virusi kunafanya kwamba hakuna nchi inayoweza kujihisi iko salama hadi pale kila nchi itakapochukua tahadhari kuwachanja watu wake," alisema.
Mkuu wa chanjo
Hadi mwishoni mwa mwaka jana Dkt Okonjo-Iweala alikuwa mwenyekiti wa muungano wa dunia wa chanjo- , GAVI, ambao ulilenga kuongeza upatikanaji wa chanjo kote duniani na sasa anasema kuwa WHO ina kazi muhimu ya kufanya katika eneo hili.
Kuna mjadala unaoendelea kuhusu kulegea kwa sheria za WTO kuhusu akili miliki ili watengenezaji zaidi wa dawa waweze kutengeneza chanjo zaidi. Dkt Okonjo-Iweala anakiri hilo lakini anasema "baadhi ya nchi zinazoendelea zinaomba haki ya kisheria, nchi zinazoendelea zinahisi kuwa hii inaweza kuingilia katika akili miliki ".
Lakini alizungumzia kuhusu "njia ya tatu , ambayo tunaweza kupatia kibali ya utengenezaji kwa nchi ili uwe na bidhaa unayotaka ya kutosha huku ukiendela kuhakikisha kuwa akili miliki inatunzwa ".
Hii tayari inafanyika kwa chanjo ya Oxford-Astra Zeneca, ambayo imepewa kibali cha kwa taasisi ya -Serum Institute of India.
Huku janga likiwa ni changamoto ya dharura inayomkabili kiongozi mpya WTO, sio changamoto pekee.
Shirika hilo linapambana kuhakikisha linaonekana kuwa la umuhimu kwa mataifa mengi ambayo yanadhani lipepitwa na wakati na yanayoamini kuwa shirika hilo limezorota katika kuleta mabadiliko katika uchumi wa dunia.
Baada ya kuzorota kwa mchakato wa kumchagua kiongoni wake kutokana na ukosefu wa uungaji mkono kutoka kwa utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, Dkt Okonjo-Iweala anatambua ushindi wake una maana gani.
"Najivunia kuwa mwanamke wa kwanza na Mwafrika wa kwanza ," alisema.
Mwanamageuzi
Hatahivyo, yuko makini kufanya kazi kama mwana mageuzi , hadhi ambayo aliitamani alipokuwa naibu Mkuu wa Benki ya Dunia na kama Waziri wa fedha wa Nigeria, ambako alifanikiwa kuliwezesha taifa lake kupunguzi wa mzigo wa madeni ya kimataifa.
Alisema kuwa : " Kuna suala la wanacha kupoteza imani na kazi kubwa inahitajika kufanywa kuziwezesha sheria za WTO kuwiana na hali halisikatika karne ya 21 ."
Kama changamoto cha virusi vya corona zitaweza kushughulikiwa, hizo "hatua ndogo, mafanikio madogo madogo ya mapema yanaweza kusaidia kubuni imani na kukuruhusukufanya mageuzi makubwa", alisema.
Miongoni mwa changamoto hizo ni mkataba mgumu kuhusu ruzuku za uvuvi.
"Kutoka pale, tunaweza kuendelea kugeuza mzozo wa mfumo wa makazi, uliopo sasa, lakini ambao unaohitajika, kwasababu hilo ndio eneo pekee duniani ambako wanachama wafanyabiashara wanaweza kuleta mizozo ya kibiashara
Ilivunjwa na kura yaveto ya Trump alipopiga kura hiyo juu ya uteuzi wa majaji wapya wa shirika hilo wenye jukumu la kutatua mizozo hiyo.
"Kuanzia hapo, tunaweza kuendelea kurekebisha sheria katika maeneo kama uchumi wa kidigitali na biashara za kimtandao ," alisema, na kuongeza kuwa pia alitaka kubadili jinsi wanawake wanavyohudumiwa na WTO na jinsi mabadiliko ya hali ya hewa yanavyofikiriwa. ."
Vita vya biashara kati ya Marekani na China
Vita vya biashara kati ya marekani na Uchina ni eneo ambalo WTO limehangaika kupata mafanikio katika upatikanaji wa suluhu, kutokana na ukosefu wa mbinu za utekelezaji. Na hilo ni licha ya uamuzi wa mwaka jana kwama ushuru wa marekani "haukuaendana "na sheria za kimataifa za biashara.
Dkt Okonjo-Iweala amesema: "Tunaweza kuwa wenye usaidizi sana kwa Marekani na China kwa pamoja kuwasaidia kuwaleta pamoja kutatua matatizo ."
Sababu moja inayoifanya WTO kuhangaika kupata mafaniki katika maeno mengi ni kwasababu ya kusisitiza kwamba maamuzi yafanyike kwa maafikiano ya wanachama wote 164.