Amazon vs Reliance: Kwa nini kampuni hizi tajiri zaidi duniani zinakabiliana mahakamani?

Jeff Bezos speaking

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wachambuzi wanasema Amazon haijawahi kukabiliwa na ushindani mkali kama ule inayoshuhudia kutoka kwa Reliance

Mzozo juu ya kampuni ya mboga ya India umeikutanisha mahakamani kampuni kubwa ya biashara mtandaoni Amazon na kampuni kubwa zaidi ya biashara ya aina hiyo nchini India -Reliance.

Kampani hizo mbili zimejipata katika mzozo huo kwasababu zilikuwa zimefikia mkataba na kampuni ya mauzo ya reja reja ya India - Future Group.

Wachambuzi wanasema mzozo wa kisheria, unaohusisha kampuni ya Marekani na kampuni hiyo kubwa ya India nyumbani, huenda ukachangia ukuaji wa biashara ya mtandaoni nchini India katika miaka ijayo.

“Nadhani hii ni kali. Amazon haijawahi kupata upinzani kama huu katika soko lao lolote,” Satish Meena, mchambuzi wa ngazi ya juu wa masuala ya masoko kutoka kampuni ya Forrester, aliambia BBC.

Amazon ilimfanya muanzilishi wake Jeff Bezos kuwa mtu tajiri zaidi duniani (japo sasa hashikilii nafasi hiyo) na kampuni hiyo kubadili biashara ya mtandaoni kote duniani. Lakini Afisa mkuu mtendaji wa Reliance Mukesh Ambani - ambaye ndiye mtu tajiri zaidi India - pia ana historia ya kuvuruga hali hiyo.

Wachambuzi wa sekta hiyo wanafikiri mpango wa biashara yake itaipatia Amazon changamoto, ikiwa ni pamoja na Flipkart inayomilikiwa na Walmart.

Amazon imekuwa imekuwa ikipanua kwa kasi biashara yake nchini India, ambako inatarajia kuongeza kipato kupita ukuaji wa soko la mtandaoni. Reliance pia ina mpango wa kuimarisha biashara yake mtandaoni na hali kadhalika biashara ya mboga.

Mukesh Ambani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mukesh Ambani has a home advantage against Amazon

Mzozo dhidi ya Future Group unahusu nini?

Kampuni ya Future Group hivi karibuni iliwasilisha mpango wa kuuza mali ya rejareja yenye thamani ya $ 3.4bn kwa Viwanda vya Reliance mapema mwaka huu.

Tangu mwaka 2019, Amazon imekuwa inashikilia 49% ya hisa za kampuni ya Future ambazo ziliipatia umiliki usiokuwa wa moja kwa moja wa ununuzi wa rejareja wa Future. Amazon inasema kuwa kama sehemu ya ununuzi huo, Future Group ilizuiwa kuuzia bidhaa zake makampuni ya India, ikiwemo Reliance.

Future Retail, ambayo zaidi inajihusisha na biashara ya matofali na mortar iliathiriwa vibaya na na janga la corona inasema nia yake ya kushirikiana na Reliance ilikuwa ni kuilinda kampuni isiporomoke.

Duru ya hivi karibuni kortini ilikwenda kwa Kundi la Baadaye. Jumatatu iliyopita, korti kuu ya Delhi ilibadilisha uamuzi kutoka wiki moja mapema ambayo ilisitisha uuzaji huo

Zama ya hivi karibuni mahakamani ilikuwa ya kampuni ya Future Group. Jumatatu iliyopit, mahakama kuu mjini Delhi ilibatilisha uamuzi wa kusitisha mauzo.

Amazon imekata rufaa.

Ni nini kilicho hatarini?

Ikiwa Reliance itaruhusiwa kendelea mbele na shughuli za ununuzi, huenda kitengo chake cha uzaji wa rejareja ukafikia zaidi ya maduka 1,800 katika zaidi ya miji 420 nchini India, pamoja na kitengo cha biashara ya jumla ya kampuni Future Group.

“Reliance ina uwezo wa kifedha, ambao unahitajikakatika ushawishi wa soko hili japo hawana utaalamu wa biashara ya mtandaoni lakini ,” alisema Bw. Meena.

Ikiwa Amazon itafanikiwa, huenda ikapata nguvu ya kuwadhibiti washindani wao wakuu kuendelea mbele na mpango wa kujiimarisha katika biashara ya mtandaoni.