China yaanza kuwafundisha vijana ukakamavu

Soldiers in China's army

Chanzo cha picha, Barcroft Media/Getty Images

Maelezo ya picha, Wakati China inataka vijana kuwa wanajeshi, sio wengi wenye ndoto hiyo

Tangazo kutoka wizara ya elimu nchini China limesababisha gumzo baada ya kusema kuwa vijana wadogo nchini China wameanza kuwa na tabia za "kike".

Taarifa hiyo imekosolewa kama yenye ubaguzi wa kijinsia na watumiaji wa mitandao - lakini baadhi wanasema kuwa kwa kiasi fulani wasanii wa kiume wanastahili kulaumiwa.

Kwa kipindi fulani, serikali ya China imeonesha wasiwasi wake kwamba wanaume maarufu kama vile wanariadha, wanajeshi mashujaa na wengine ambao wangekuwa mfano mwema wa kuigwa hawapo tena.

Hata Rais Xi Jinping ambaye anafahamika kama shabiki wa mpira, kwa kipindi kirefu amekuwa akitoa wito wa kukuza vipaji watakao kuwa mfano wa kuigwa katika michezo.

Wiki iliyopita, wizara ya elimu ilitoa tangazo lililokuwa na kichwa chenye kuelezea kinaga ubaga lengo lake.

Pendekezo la kuzuia vijana waliobalehe kuwa na tabia za kike lilitoa wito kwa shule kubadilisha kabisa wanachofunza katika masomo yao na kuimarisha usajili wa walimu.

Ujumbe huo ulishauri usajili wa wanamichezo waliostaafu na watu wenye historia ya michezo - na kuendeleza michezo mingine kama vile kandanda kwa lengo la "kukuza sifa za kiume".

Ni hatua iliyoazimiwa katika nchi ambayo vyombo vya habari haviruhusu kingine chochote zaidi ya kile ambacho ni kisafi kabisa, "nyota" wanaowajibka katika jamii.

Lakini kulikuwa na dalili za awali zilizoashiria kuwa hatua hiyo inakaribia. Mwezi Mei mwaka jana, mjumbe kutoka bodi ya juu ya ushauri, Si Zefu, ilisema kuwa vijana wengi wa China wamekuwa, "dhaifu, wenye uoga na kujidhalilisha".

Kulikuwa na mtindo miongoni mwa vijana wa China wa kuwa na tabia za "kike", Si Zefu alidai, ambako bila shaka "kutahatarisha uwepo na maendeleo ya taifa la China" tatizo hilo "lisipodhibitiwa kikamilifu", aliongeza.

Si Zefu alisema kuwa mazingira ya nyumbani kwa kiasi fulani yanastahili kulaumiwa kwa hilo, huku wavulana wengi wa kiume wakilelewa na mama zao au bibi zao.

Pia alisema kuwa ushawishi wa baadhi ya wasanii wa kiume uneondelea kuongezeka, kumefanya watoto wengi kutotaka tena kuwa mashujaa katika jeshi tena.

Kwahiyo, akapendekeza kwamba shule zinastahili kuchukua jukumu kubwa kuhakikisha vijana wa China wanapata elimu yenye uwiano.

'Wanaume wanaogopa nini?'

Idadi kubwa ya raia wa China walikasirishwa na tangazo hilo.

Mamia ya maelfu ya raia wa China wameenda kwenye mitandao ya kijamii kuonyesha hasira zao huku idadi kubwa ikisema ujumbe uliotolewa na serikali ni ubaguzi wa kijinsia.

"Kwani sifa za kike sasa zimekuwa jambo la kudhalilisha?

Mmoja ameuliza, na ujumbe wake ukapendwa na watu 200,000.

Mwingine akauliza: "Wavulana pia ni binadamu… kuwa na hisia, uoga au kuwa wapole kitabia hizi ni sifa za kibinadamu."

"Waume wanaogopa nini? Kuwa sawa na mwanamke?" mmoja ameuliza.

TF Boys are known as some of China's 'little fresh meats'

Chanzo cha picha, VCG/Getty Images

Maelezo ya picha, Makundi ya vijana kama TF Boys ni maarufu sana nchini humo lakini vyombo vya habari huuliza ikiwa wanastahili kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana

"Kuna wanaume zaidi ya milioni 70 kuliko wanawake katika nchi hii," mwingine akadai. "Hakuna nchi katika dunia hii yenye uwiano wa kijinsia mbaya namna hii. Hizo sifa za kiume hazitoshi?"

Mwingine akasema: "hakuna katika mapendekezo haya ambalo limetoka kwa mwanamke."

Huenda wako hapa - awali, mengi yameandikwa kuhusu uongozi wa China vile ulivyotawaliwa na wanaume.

Xi Jinping visited the Manchester City Football Club in 2015

Chanzo cha picha, WPA Pool/Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Xi, shabiki wa soka alitembelea uga wa Manchester City katika ziara yake Uingereza mwaka 2015

Wakati watu mashuhuri kama mchezaji wa mpira wa kikapu Yao Ming amekuwa maarufu sana nje ya nchi, kandanda ndio iliyopendekezwa.

Lakini hilo sio ajabu kwsababu kuna wakati Rais Xi aliwahi kusema ana matumaini iko siku nchi hiyo itakuwa na "nguvu zaidi duniani katika soka" kufikia mwaka 2050.

Lakini akarejelea kuwa jitihada za kuimarisha mchezo wa mpira wa miguu nchini China zimefeli na pia zimekejeliwa kama jukumu ambalo ni vigumu kutekeleza.

Hilo ndio lilikuwa jibu miaka miwili iliyopita pale Marcello Lippi, aliyeongoza Italia kushinda kombe la dunia FIFA mwaka 2006, alipojiuzlu kama kocha wa timu ya taifa ya mpira wa miguu.

Wakati huo huo, miaka ya hivi karibuni serikali imekuwa kichocheo kuwatambua na kukuza vijana wapya wadogo watakaokuwa mfano mwema kwa nchi hiyo hiyo.

Janga la virusi vya corona limekuwa fursa nzuri ya kuonesha jukumu la mwanamke kama waliomstari wa mbele katika afya.

Lakini Si Zefu, alidokeza mwaka jana kwamba wito umepungua wa kutaka vijana wa kiume nchini China ama kuwa wanajeshi, maafisa wa polisi au zima moto wenye ujasiri.

Miaka ya hivi karibuni, vyombo vya habari vimekuwa na wakati mgumu kuruhusu nyota vijana wa kiume kujitokeza katika runinga za China wakiwa na michoro ya chale yaani tattoos au kama wamevaa vipuli.

Na mmoja wa nyota nchini humo, alikosolewa vikali mwaka 2019 alipopigwa picha kama anavuta sigara.