Kuapishwa kwa Joe Biden: Rais mpya wa Marekani anakabiliwa na mitihani gani katika Mashariki ya Kati ?

Supporters of Yemen's rebel Houthi movement protest in Sanaa against a decision by the Trump administration to declare it a foreign terrorist organisation (18 January 2021)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kundi la harakati za Houthi nchini Yemen lilipinga uamuzi wa utawala wa ' Trump

"Wenzangu ni kipindi cha majaribu ." Alisema hivyo rais mpya wa Marekani Jumatano wakati alipokuwa akitoa hotuba ya kuapishwa kwake kabla ya kuorodhesha changamoto zinazoikabili nchi na kuikamilisha kwa "Nafasi ya Marekani kwa dunia ".

Baadhi ya maswali magumu katika mtihani huo ni uhusiano na mataifa ya Mashariki ya kati.

Kikosi cha Joe Biden kina watu wengi ambao walikuwa katika utawala wa Obama hivyo wakirudi katika ukanda huo inabidi waangalie masuala waliyoacha zamani na utaratibu ambao upo sasa.

Changamoto zao kubwa zinajumuishwa na sera ambazo wao walishiriki kuziweka - katika maeneo mbalimbali ambayo yapo kwenye hali mbaya sasa. Lakini baadhi wanaona mwanya na fursa katika hilo.

File photo showing Antony Blinken speaking next to Joe Biden (24 November 2020)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Antony Blinken amehaidi kushauriana na washirika wa Marekani kabla hawajaingia tena katika makubaliano ya nyuklia

"Wamejifunza kutokana na kile kilichokuwa makosa katika namna utawala wa Obama ulivyoshugulikia masuala ya Mashariki ya Kati ," anasema Kim Ghattas, mwandishi wa kitabu cha Black Wave, kuhusu uhasama baina ya Saudia na Iran katika kanda hiyo. "Huenda wakachukulia mambo katika mtazamo tofauti kwasababu wamejifunza kutokana na makosa, na kwasababu kanda ya Mashariki ya kati ni eneo tofauti sana leo ."

Muhula wa Rais Trump ulioanza kwa chaguo ambalo wengi hawakulitarajia kwa kuichagua Riyath kama kituo cha kwanza cha sera yake ya kigeni mwezi Mei 2017, ambako alisaini mkataba wa silaha wa dola bilioni 110 za kimarekani-ambao ulikuwa ni mkubwa wa aina yake kuwahi kusainiwa na Marekani katika historia yake.

US President Donald Trump speaks with Saudi Arabia's Crown Prince Mohammed bin Salman during a photo session at the G20 summit in Osaka, Japan (28 June 2019)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Donald alitetea vitendo vya Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman

Ilitoa mwangaza kuhusu sera ya taifa hilo katika Mashariki ya Kati na ukawa mwanzo wa utiifu kwa ufalme huo na "shinikizo la hali ya juu zaidi " dhidi ya Iran.

"Diplomasia itakayofanywa na wanadiplomasia wa zamani waliohudumu chini ya utawala wa Obama huenda ikawa tu ndio kile kinachohitajiwa katika kanda hiyo ," anasema Hassan Hassan, mhariri wa jarida la Newlines , chapisho jipya linaloangazia masuala ya Mashariki ya Kati.

"Mataifa ya kiarabu yanaamini yanaweza kuchora upya ramani ya siasa ya kanda yao bila ya kuwepo uongozi wa Marekani . Lakini baada ya kujaribu kwa nusu muongo , hivi karibuni walitambua kuwa hawana uwezo wa kufanya hilo hasa katika maeneo kama Libya, Yemen, Iran, n ahata dhidi ya jirani mdogo kama Qatar."

Iranian President Hassan Rouhani speaks at a cabinet meeting in Tehran, Iran (6 January 2021)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Rais wa Iran Hassan Rouhani alisema kuwa sera ya Trump ya kuweka "shinikizo la hali ya juu " dhidi ya Iran ilishindwa

Utawala mpya wa Marekani pia utakabiliana na mahesabu nyumbani pia.

Bunge la la Congress lililochaguliwa lina wabunge , wenye uzoefu wa sera za kigeni kwa muda mrefu [pia wameonesha ishara kuwa wanataka kuwa na usemi katika mashariki ya kati hii ikimaanisha kuanzia kila kitu kuanzia mikataba yote na Iran, na mwisho wa usaidizi wa kijeshi wa Marekani utakaowezesha vita vya Saudia ; utafutaji wa amani baina ya Waisraeli na Waarabu ; hadi hofu juu ya sera ya haki za binadamu ya Saudi Arabia, ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa wapiganaji na mauji ya mwandhishi wa habari Jamal Khashoggi.

Handout photo shows Iranian Islamic Revolution Guard Corps (IRGC) chief Hossein Salami (R) watching missiles launch during an exercise in Iran (15 January 2021)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Marekani na washirika wake wanataka kukabiliana na mpango wa makombora ya masafa marefu ya Iran

Mkurugenzi wa ujasusi wa taifa wa Biden , Avril Haines, aliulizwa katika kikao cha kumthibitisha iwapo angeweza kumaliza "ukiukaji wa sheria " wa utawala wa Trump na kulipatia bunge la congress taarifa za siri kuhusina na mauaji ya Khashoggi yaliyofanywa na maafisa wa Saudi katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Instanbul Oktoba 2018.

Alijibu : "Ndio, seneta, kabisa .Tutafuata sheria."

Friends of Jamal Khashoggi hold posters bearing his picture as they attend an event marking the second anniversary of his killing in Istanbul (2 October 2020)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Saudi Arabia alipinga madai kuwa Mwanamfalme wake aliamrisha mauaji ya Jamal Khashoggi

Taarifa za vyombo vya habari, kwa kuzingatia vyanzo vya kijasusi, vimesema kuwa CIA iligundua "kwa kiwango cha hali ya juu " kwamba Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman lazima ndiye aliyeamuru mauaji ya yake . Alikana mara kwa mara hilo.

"Wamarekani watatakiwa kumpatia fursa ya kujieleza, kwasababu hakuna ushahidi," anasisitiza Ali Shihabi, mwandishi wa vitabu wa Saudi Arabia na mchambuzi. "

Iwe CIA au wizara ya mambo ya nje , au hata Pentagon , ukweli ni uelewa wa kimsingi kwamba Saudi Arabia ni muhimu kabisa kwao iwapo wanataka kufanya chochote katika kanda hiyo ya mashariki ya kati ."

Israel's Prime Minister Benjamin Netanyahu, US President Donald Trump, Bahrain's Foreign Minister Abdullatif Al Zayani and United Arab Emirates Foreign Minister Abdullah bin Zayed wave from the White House balcony after a signing ceremony for the Abraham Accords (15 September 2020)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Trump alifikia mkataba wa Abraham baina ya Israel na mataifa kadhaa ya kiarabu

Kuna maslahi mengi yanayozihusisha pande mbili, ikiwa ni pamoja na kumalizika kwa janga la vita nchini Yemen . Lakini sawa na matatizo mengine ya mashariki ya kati , hakuna chaguo rahisi.

"Sio rahisi kama kusitisha usaidizi wa kijeshi kwa Saudi Arabia," anaonya Peter Salisbury, mchambuzi wa ngazi ya juu wa masuala ya Yemen kutoka shirika International Crisis Group. " Kama Marekani inataka amani itatakiwa kushiriki kikamilifu kidiplomasia ."

Diplomasia itakuwa na mabadiliko ya ajabu, hususan kwa utawala ambao tayari umeweka haki za binadamu katika ajenda zake. Hilo litamaanisha mazungumzo magumu kila mahali kuanzia Riyadh hadi Tehran , Cairo na kwingineko . Wengi watatazama kwa shauku -kuona iwapo mazungumzo yatatekelezwa kwa vitendo.