Mgogoro wa nyuklia Iran: Iran kurutubisha madini yake ya uranium kwa asilimia 20, UN yasema

Chanzo cha picha, EPA
Iran inapanga kuanza tena kurutubisha madini yake ya uranium yaani urani kwa asilimia 20, hayo ni kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya atomiki (IAEA), hatua ambayo hadi kufikia sasa itakuwa ni ukiukaji mkubwa wa makubaliano ya kimataifa ya nyuklia.
Hiyo inamaanisha kwamba Iran itakuwa na mapungufu ya asilimia 90 ya kiwango kinachohitajika kutengeneza bomu la nyuklia.
Lakini kulingana na makubaliano ya mwaka 2015, Iran ilihitajika kuimarisha madini yake ya uraniaum kwa kiwango cha chini ya asilimia 4.
Iran ilianza kukiuka makubaliano hayo baada ya rais Trump kuindoa Marekani kwenye makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa na kuiwekea tena nchi hiyo vikwazo. ambavyo vimeyumba pakubwa uchumi wa nchi hiyo.
Hata hivyo, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ufaranza na Uchina zote zina matumaini kuwa uhusiano wa pande hizo mbili unafursa ya kuimarika tena.
Iran inapanga nini?
Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya atomiki (IAEA), limesema Iran ilikuwa imeifahamisha mpango wake wa kurutubisha madini yake ya urani hadi asilimia 20 katika mtambo wake ambao umejengwa ndani ya mlima.
Lakini shirika hilo limeongeza: "Barua ya Iran ... haikusema shughuli hizo zitataanza lini."
Iran ilikiuka kiwango ambacho kilikuwa kimewekwa kwa uimarishaji wa madini yake cha asilimia 3.67 kulingana na makubaliano ya nyuklia yam waka 2019 lakini Iran iliamua kuendeleza kiwango hicho kwa hadi asilimia 4.5 tangu wakati huo.
Hata hivyo, kuongeza urutubishaji wa madini ya uranium hadi asilimia 20 kumetokana na sheria iliyopitishwa na bunge la Iran mwezi uliopita baada ya kifo cha mwanasayansi mkuu wa masuala ya nyuklia nchini humo, Mohsen Fakhrizadeh.
Mswada huo ulihitaji serikali ya Iran kuanza tena kuimarisha madini yake ya urani hadi asilimia 20 ikiwa vikwazo vya mafuta na fedha dhidi ya nchi hiyo havitalegezwa ndani ya kipindi hca miezi miwili.
Pia bunge lilitaka wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kuzuiwa kutembelea kiwanda chake cha utengeenzaji madini ya urani maeneo ya Natanz na Fordow.
Urutubishaji wa madini uranium ni nini?
Madini ya Uranium yaliorutubishwa hutengenezwa kwa kuweka gesi ya uranium hexafluoride ndani ya mashine ya kuzunguka ijulikanayo kama centrifuges kwa lengo la kutenganisha viini muhimu vya kutengeneza nyuklia vijulikanavyo kama U-235.
Chini ya mkataba huo makubaliano ya nyuklia , Iran inaruhusiwa kutengeneza kiwango kidogo cha madini yaliorutubishwa ya uranium yalio na asilimia kati ya 3- 4 ya U-235, na yanaweza kutumika kutengeneza nishati kwa vinu vya nyuklia.
Viwango vya kutengeneza silaha-ni 90% ya uranium iliyorutubishwa au zaidi.
Makubaliano hayopia yanaizuia Iran kuweka akiba inayozidi 300kg ya madini hayo yaliorutubishwa kwa kiwango kidogo.
Iran imekuwa ikikana inarutubisha madini hayo kwa minajili ya kujenga zana za nyuklia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwanini kuna umuhimu wa kuwa na ukomo wa urutubishaji madini ya uranium?
Waangalizi wanasema kuwa urutubishaji wa madini ya uranium kunaweza kufupisha muda unaohitajika kutengeneza bomu la nyuklia.
Iran inasisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani.
Hata hivyo, mashaka ya kuwa Iran huenda inatengeneza bomu la nyuklia kisiri yalifanya Umoja wa Ulaya, Marekani na Umoja wa Mataifa kuiwekea Iran vikwazo mwaka 2010. .
Makubaliano ya mwaka 2015 yaliyotiwa saini na China, Ufaransa, Ujerumani, Urusi Uingereza na Marekani yalifikiwa ili kusitisha mpango huo kwa mabadilishano ya Iran nayo iondolewe vikwazo.
Matarajio ya kufufuka tena makubaliano hayo yakoje?
Rais Trump alijiondoa kwenye makubaliano hayo mwaka 2018, alipoyaita "muozo na usiokuwa na maana yoyote".
Lakini rais Joe Biden kwa upande wake, amesema kuwa atairejesha Marekani katika makubaliano hayo - yaliyopatanishwa na Rais Barack Obama na pia ataiondolea Iran vikwazo ikiwa itakubali kuanza "kutekeleza makubaliano ya nyuklia kwa ukamilifu".













