Uchumi wa China 'kuupiku ule wa Marekani kufikia 2028' kutokana na janga la corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Uchumi wa China utaupiku ule wa Marekani kufikia 2028 , miaka mitano mapema ya ilivyokadiriwa ripoti imesema.
Kituo cha kutafiti uchumi na biashara kilicho na makao yake huko Uingereza CEBR kilisema kuwa uwezo wa China kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona utaimarisha ukuaji wake ikilinganishwa na Marekani na Ulaya katika kipindi cha miaka ijayo.
Wakati huohuo India inatarajiwa kuwa taifa la tatu lenye uchumi mkubwa duniani kufikia 2030.
Kituo hicho cha CBR hutoa matokeo ya utafiti wake kila mwaka tarehe 26 mwezi Disemba.
Ijapokuwa China ilikuwa nchi ya kwanza kuathiriwa na mlipuko wa virusi vya corona , ilifanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo kupitia vitendo vyenye masharti makali ikimaanisha kwamba haikulazimika kusitisha kufunga baadhi ya maeneo na kufungua kama inavyofanyika barani Ulaya.
Kutokana na hilo ikilinganishwa na mataifa mengine yenye uchumi mkubwa , imefanikiwa kuzuia mfumuko wa kiuchumi mwaka 2020 na badala yake taifa hilo linatarajiwa kukua kwa asilimia 2 mwaka huu.
Uchumi wa Marekani umeathiriwa vibaya na virusi vya corona kulingana na takwimu. Zaidi ya watu 300,000 wamefariki nchini humo huku takriban watu milioni 18.5 wakiambukizwa .
Uharibifu wa kiuchumi umezuiwa na sera za kifedha pamoja na vichocheo vya kiuchumi , lakini tofauti za kisiasa kuhusu kiwango cha kifedha cha kuchochea uchumi huo huenda zikawawacha takriban Wamarekani milioni 14 bila ajira na marupurupu mwaka mpya.

" Kwa muda, mada kuu ya uchumi wa ulimwengu imekuwa mapambano ya kiuchumi kati ya Marekani na China, "inasema ripoti ya CEBR.
Janga la Covid-19 na uchumi unaolingana kwa kweli umesababisha China kufaidika zaidi na uhasama huo.
Ripoti hiyo inasema kwamba baada ya kuimarika kufuatia kuisha kwa virusi vya Covid 19 , uchumi wa Marekani utakuwa kwa asilimia 1.9 kila mwaka kutoka 2022-24 na baadaye kupunguza kasi kwa asilimia 1.6% katika miaka itakayofuata.
Kwa upande mwingine uchumi wa Wachina umedhamiriwa kukua kwa 5.7% kila mwaka hadi 2025, na 4.5% kila mwaka kutoka 2026-2030.
Sehemu ya China ya uchumi wa dunia imepanda kutoka 3.6% mwaka 2000 hadi 17.8% sasa na nchi hiyo itakuwa na "uchumi wa kipato cha juu" ifikapo 2023, ripoti inasema.

Uchumi wa China haunufaiki tu kwa kuwa na Covid-19 iliyodhibitiwa mapema, lakini pia kutengeneza sera mahsusi kulenga viwanda kama utengenezaji wa bidhaa za hali ya juu, alisema naibu mwenyekiti wa CEBR Douglas McWilliams
"Wanaonekana wanajaribu kuwa na udhibiti wa kati katika ngazi moja, lakini uchumi wa soko huria katika maeneo mengine," aliiambia BBC
"Na ni soko huria ambalo linawasaidia kusonga mbele haswa katika maeneo kama teknolojia."
Lakini wastani wa Wachina utasalia kuwa na watu masikini zaidi katika suala la kifedha kuliko Mmarekani wa kawaida hata baada ya China kuwa na uchumi mkubwa zaidi ulimwenguni, ikizingatiwa kuwa idadi ya Wachina ni kubwa mara nne.












