Virusi vya corona: Marekani yaidhinisha Moderna kuwa chanjo ya pili

Chanzo cha picha, Moderna
Moderna imeidhinishwa na serikali ya Marekani kama chanjo ya pili ya corona nchini humo, baada idhini ya kusambazwa kwa dozi za chanjo hiyo kutolewa.
Mamlaka ya kusimamia usalama wa chakula na dawa (FDA) iliidhinisha chanjo hiyo iliyongenezwa Marekani karibu wiki moja iliyopita baada ya kuidhinisha chanjo ya Pfizer/BioNTech ambayo kwasasa inatolewa.
Marekani ilikubali kununua dozi milioni 200 ya Moderna, na milioni sita kati ya hizo huenda ziko tayari kusafirishwa.
Nchi hiyo ina idadi ya juu zaidi ya vifo vilivyotokana na ugonjwa wa corona na hali kadhalika viwango vya juu vya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.
Imerkodi zaidi ya vifo 313 na karibu maambukizi milioni 17.5, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Kamishena wa FDA Stephen Hahn amesema kuidhinishwa kwa dharura kwa chanjo hiyo siku ya Ijumaa kunaashiria ''hatua nyingine muhimu katika juhudi za kukabiliana na janga la kimataifa ".
Hatua ya kuidhinishwa kwa chanjo hiyo ilifikiwa baada ya jopo la wataalamu kupiga kura siku ya Alhamisi 20-0 huku wito ukitolewa kwamba ubora wa chanjo ya Moderna unazidi madhara yake kwa watu waliyo na umri 18 na zaidi.
Wadhibiti waliripoti mapema wiki hii kwamba chanjo ya Moderna ilikuwa salama na inafanya kazi kwa asilimia 94.
Rais wa Marekani Donald Trump,aliandika katika mtandao wake wa Twitter saa kadhaa kabla ya tangazo rasmi kutolewa alisema chanjo hiyo "imeidhinishwa kwa kishindo" na itaanza kusambazwa "mara moja ", aliandika kwenye Twitter: "Pongezai chanjo ya Moderna vaccine sasa inapatikana!"
Rais -mteule Joe Biden, ambaye anajiandaa kupewa chanjo siku ya Jumatatu, amesema kuidhinishwa kwa chanjo za sindano za Pfizer na Moderna "kunatuhakikishia siku njema huko mbele". lakini akaongeza kuwa, "vita dhidi ya Covid-19 havijaisha."

Chanzo cha picha, Moderna
Itapatikana lini?
Kampuni ya Moderna inatarajia kuwa na hadi dozi bilioni moja kiasi kinachoweza kutumiwa ulimwenguni kote mwakani na imepanga kutafuta idhini katika nchi nyingine pia.
Serikali ya Uingereza bado inajadiliana na Moderna kwani chanjo hiyo si miongoni mwa aina sita za chanjo zilizoagizwa tayari.
Uingereza imeelezea mipango ambayo inatoa kipaumbele kwa watu wakongwe zaidi kupata chanjo.
Ina athari yoyote?
Hakuna wasiwasi mkubwa wa usalama wa chanjo hiyo ulioripotiwa, , pamoja na paracetamol, iko salama kwa 100%.
Uchovu wa muda mfupi, maumivu ya kichwa na maumivu yaliripotiwa baada ya sindano kwa wagonjwa wengine.
"Athari hizi ndio tungetarajia kwa chanjo ambayo inafanya kazi na kushawishi mwitikio mzuri wa kinga," alisema Prof Peter Openshaw, kutoka Chuo cha Imperial London.
Covid-19 itakwisha lini?
Katika kipindi cha wiki moja, matokeo mazuri kutoka kwa Pfizer, Moderna na Urusi yamebadili uwezekano wa kumaliza ugonjwa huo.
Kabla ya matokeo ya kwanza, mazungumzo yalikuwa ya chanjo ambayo ilitoa ulinzi wa 50%. Matarajio hayo ni kuwa sio tu chanjo zinawezekana, lakini pia zinaonekana kuwa na nguvu.
Takwimu hadi sasa pia zinaongeza matumaini kwamba chanjo nyingine zilizo katika kutengenezwa zitafanikiwa pia, lakini sasa changamoto moja inapomalizika, nyingine huanza.














