Virusi vya corona: Chanjo ya Moderna inazuia Covid-19 kwa 95%

Chanzo cha picha, Getty Images
Chanjo mpya inayozuia ugonjwa wa Covid-19 ina karibu 95% ya ufanisi , data kutoka Kampuni ya Marekani Moderna inaonesha,
Matokeo haya yamekuja sawa na yale ya chanjo ya Pfizer, na kuongeza imani kuwa chanjo zinaweza kusaidia kumaliza janga hili.
Kampuni zote mbili zilitumia mbinu na majaribio ya chanjo zao.
Moderna inasema hiyo ni "siku muhimu" na wanapanga kuomba idhini ya kutumia chanjo hiyo katika wiki chache zijazo.
Hatahivyo hizi ni data za awali , na maswali muhimu bado yamebaki yakiwa hayajajibiwa
Ni nzuri kiasi gani?
Jaribio hilo lilihusisha watu 30,000 huko Marekani na nusu wakipewa dozi mbili za chanjo, wiki nne tofauti. Wengine walikuwa na sindano .
Uchambuzi huo ulitokana na 95 wa kwanza waliokuwa na dalili za Covid-19.
Takwimu hizo pia zinaonesha kulikuwa na wagonjwa 11 wa Covid lakini hakuna hata mmoja aliyetokea kwa watu ambao walikuwa wamepewa chanjo.
"Ufanisi wa jumla umekuwa wa kushangaza ... ni siku nzuri," Tal Zaks, afisa mkuu wa tiba huko Moderna, aliambia BBC News.
Rais wa Kampuni hiyo Dkt Stephen Hoge aliiambia BBC News: "Sidhani kama yeyote kati yetu alitumai kweli kwamba chanjo hiyo itakuwa na ufanisi wa 94% katika kuzuia ugonjwa wa Covid-19, huo ulikuwa utambuzi mzuri sana."
Itapatikana lini?
Hiyo inategemea mahali ulipo ulimwenguni na una umri gani.
Moderna inasema itapelekwa kwa mammlaka ya dawa katika wiki zijazo. Inatarajia kuwa na dozi milioni 20 zinazopatikana nchini.
Kampuni hiyo inatarajia kuwa na hadi dozi bilioni moja kiasi kinachoweza kutumiwa ulimwenguni kote mwakani na imepanga kutafuta idhini katika nchi nyingine pia.
Serikali ya Uingereza bado inajadiliana na Moderna kwani chanjo hiyo si miongoni mwa aina sita za chanjo zilizoagizwa tayari.
Uingereza imeelezea mipango ambayo inatoa kipaumbele kwa watu wakongwe zaidi kupata chanjo.

Chanzo cha picha, Moderna
Tusichokijua
Bado hatujui kinga itachukua muda gani kwani waliojitolea watalazimika kufuatwa kwa muda mrefu kabla ya swali hilo kujibiwa.
Kuna vidokezo ambavyo hutoa ulinzi katika makundi ya wazee, ambao wako katika hatari ya kufa kutokana na Covid, lakini hakuna data kamili.
Bwana Zaks aliambia BBC data zao hadi sasa zinaonesha chanjo hiyo "haionekani kupoteza nguvu zake" kutokana na umri.
Na haijulikani kama chanjo hiyo itawafanya watu wasiwe wagonjwa sana, au ikiwa inawazuia kueneza virusi pia.
Maswali haya yote yatategemea jinsi chanjo ya virusi vya corona inatumiwa.
Ina athari yoyote?
Hakuna wasiwasi mkubwa wa usalama wa chanjo hiyo ulioripotiwa, , pamoja na paracetamol, iko salama kwa 100%.
Uchovu wa muda mfupi, maumivu ya kichwa na maumivu yaliripotiwa baada ya sindano kwa wagonjwa wengine.
"Athari hizi ndio tungetarajia kwa chanjo ambayo inafanya kazi na kushawishi mwitikio mzuri wa kinga," alisema Prof Peter Openshaw, kutoka Chuo cha Imperial London.
Covid-19 itakwisha lini?
Katika kipindi cha wiki moja, matokeo mazuri kutoka kwa Pfizer, Moderna na Urusi yamebadili uwezekano wa kumaliza ugonjwa huo.
Kabla ya matokeo ya kwanza, mazungumzo yalikuwa ya chanjo ambayo ilitoa ulinzi wa 50%. Matarajio hayo ni kuwa sio tu chanjo zinawezekana, lakini pia zinaonekana kuwa na nguvu.
Takwimu hadi sasa pia zinaongeza matumaini kwamba chanjo nyingine zilizo katika kutengenezwa zitafanikiwa pia, lakini sasa changamoto moja inapomalizika, nyingine huanza.












