Waziri wa Malawi aidhinisha Nabii Bushiri na mkewe warudishwe Afrika Kusini

Waziri wa usalama wa ndani ya nchi wa nchini Malawi , Richard Banda, amesaini nyaraka kwa ajili ya mchungaji tajiri na maarufu Shepherd na mke wake, Mary, vimeripoti vyambo vya habari vya Malawi.

Hii inafuatia ombi la mahakama ya nchi jirani ya Afrika Kusini ambako Bushiri na mke wake Mary wanasakwa na mashitaka ya utakasaji wa fedha na ufisadi.

Mahakama ya juu zaidi nchini Malawi iko tayari kuamua kuhusu kukamatwa kwa wawili hao baada ya kuachiliwa huru bila masharti na mahakama ya hakimu mkazi ambayo ilisema kuwa ilichukua uamuzi huo kwasababu hapakuwa na ombi rasmi la kumrejesha lililotolewa na Afrika Kusini.

Mahakama itaamua kuhusu kesi hiyo tarehe 22 Disemba, kwa mujibu wa gazeti la Daily Times newspaper.

Bushiri na mke wake walitoroka kutoka Afrika Kusini mwezi uliopita, baada ya kukaidi sharti la kulipa dhamana ambayo ilikuwa inawazuia kuondoka nchini Afrika Kusini mpaka kesi yao itakapokamilika.

Mchungaji huyo au Pastor Bushiri wakati huo alisema kuwa maisha yake yamo hatarini iwapo hataondoka nchini humo.

Serikali za Malawi na Afrika Kusini zilikuwa zimetoa taarifa kuhusiana na kutoroka kwao baada ya rais wa Malawi Lazarus Chakwera -ambaye alikuwa ziarani nchini Afrika Kusini- kushutumiwa kusaidia kutoroka kwa mchungaji Bushiri.

Kesi inayomkabili Mchungaji Bushiri Afrika Kusini

Bushiri, na mke wake na watu wengine wawili wanakabiliwa na shutuma za kutakatisha fedha na mashitaka mengine 419.

Wapelelezi wa uhalifu wanasema kesi hiyo inahusu ina thamani ya randi ya Afrika kusini milioni 102 ($6.6m).

Alifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Pretoria tarehe 21 Oktoba na kesi yake ilitarajiwa kuanza Mei.

Hatua zilizochukuliwa dhidi ya Bushiri na mke wake

Kasri hiyo ya kifahari iliyopo karibu na mji wa Pretoria ina thamani ya randi milioni 5.5 za Afrika Kusini sawa na dola 350,000 au pauni 260,000, kwa mujibnu wa taarifa.

Jaji aliwaamuru Nabii Bushiri na mke wake kutoa stakabadhi za nyumba wakati mahakama hiyo ilipowapa dhamana kufuatia tuhuma za utakatishaji wa fedha na ufisadi zinazowakabili.

Hatua hiyo ya mahakama ilitokana na kwamba Mchungaji huyo maarufu akikabiliwa na mashitaka 419 na utakatishaji wa fedha nchini Afrika Kusini.

Mamlaka za Botwana zilifunga kanisa lake baada ya madai kuwa alikuwa anawataka watu wampatie pesa bila huduma yoyote, kitu ambacho kilikuwa ni kinyume na sheria za fedha nchini humo.

Nabii Shepherd Bushiri ni nani?

Nabii Mchungaji Shepherd Bushiri ni mzaliwa wa Malawi ambaye huendesha shughuli zake za "unabii" katika makanisa mbalimbali kuanzia Ghana hadi Afrika Kusini.

Anadai kuwa anatibu virusi vya Ukimwi/HIV na kuwafufua watu, kwa mujibu wa magazeti ya Afrika Ksuini ya Mail & Guardian yaliyotolewa 2018.

Bushiri aliwahi kubashiri kuwa Uingereza itagawanyika, "majimbo" na itaingia vitani na kuwa katika "vurugu", jarida la Maravi Post lilisema katika moja ya ripoti zake.

Na katika moja ya video zake alionekana akitembea hewani, video ambayo ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii .

Bushiri alimwambia mwanasiasa wa Zimbabwe Kembo Mohadi kuwa atapata "madaraka " hata kabla ya kutangazwa kuwa makamu wa rais, kulingana taarifa ya New Zimbabwe.

Mchungaji Shepherd Bushiri ni muanzilishi wa kanisa la Afrika Kusini lenye matawi yake katika nchi nyingine.

Wengi husema Mchungaji milionea ndiye kiongozi wa kidini tajiri zaidi barani Afrika.

Mchungaji Bushiri alikulia katika mji wa Mzuzu, uliopo Malawi kabla ya kwenda Pretoria nchini Afrika Kusini.

Taarifa zinasema kuwa alipigwa marufuku kukanyaga katika ardhi ya Botwana kwasababu ya "pesa za miujiza".

Amekuwa maarufu sana kutokana na mikusanyiko mikubwa ya wafuasi wake wanaojaa katika viwanja vikubwa vya michezo.

Lakini watu wanamshutumu kuwa anawatumia vibaya masikini wanaotaka kubadili hali zao za maisha kwa kuwauzia "mafuta ya muujiza" .

Akifahamika kama Major au Nabii Shepherd , Bushiri alizaliwa tarehe 20 Februari, 1983.

Mamlaka za Botwana zilifunga kanisa lake baada ya madai kuwa alikuwa anawataka watu wampatie pesa bila huduma yoyote, kitu ambacho kilikuwa ni kinyume na sheria za fedha nchini humo.