Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni kwanini ndugu wa karibu wanapooana ni hatari?
Kuoana kati ya watu wenye uhusiano wa karibu wa damu ni jambo la kawaida miongoni mwa makabila mbalimbali, huku baadhi yao wakifanya hivyo ili kuimarisha uhusiano ndani ya familia na wengine wakifanya hivyo ili mali ya familia ibaki ndani ya familia au ukoo.
Lakini licha ya ukweli kwamba ndoa za watu wa ukoo na familia moja, zina faida za kijamii na kuongeza uwezekano mkubwa wa wanandoa kupendana zaidi na kuheshimiana, madaktari wanaonya kuwa ndoa hizi ni hatari.
Dkt Ibrahim Musa, ambaye ni mtaalamu wa sayansi ya damu, damu inayotengeneza viungo vya ndani ya mwili na magonjwa ya damu katika hospitali ya Malam Aminu Kano kaskazini mwa Nigeria , anasema ndao ya watu wenye uhusiano wa damu inauwezekano mkubwa wa kusababisha hatari ya magonjwa ya urithi kutoka kwa wazazi.
Kwa mfano, ugonjwawa seli mundo( sickle celll) ambao mara nyingi mtu huurithi kutoka kwa wazazi, inapotokea kwamba mtu wa familia anaolewa na mtu kutoka familia yenye ugonjwa huo, inakuwa ni rahisi sana kuendlea kuusambaza hata kwa vizazi vyao.
Mtaalamu huyo pia anasema kwamba kuna magonjwa ya urithi ambayo husababishwa na kuoana kwa watu wa familia moja bila wao kufahamu.
Jeni za ndugu
Jarida la masuala ya afya la Lancet mwaka 2013, linasema kuwa jeni za wanandoa zinaweza kumuathiri mmoja wao, bila kujali kabila au jamii atokayo.
Kwa mfano mwanamke ambaye ameolewa na kaka yake au mwanaume kutoka familia sawa na yake ana uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya kiafya ya watoto wake.
Licha ya kwamba ripoti ya kina ya huduma za afya za Uingereza (HHS) kuhusiana na suala hilo inasema kuwa ni mara chache kwa watoto waliozaliwa katika familia za wazazi wenye undugu , na kwamba wengi wao huzaliwa wakiwa na afya ya kawaida.
Lakini inasema hata hivyo kwamba , ndoa kama vile za wapwa na wapwa au mabinamu na mabinamu zinauwezekano mkubwa wa kusababisha matatizo ya kiafya kwa watoto wanaowazaa kwa asilimia tatu hadi sita , lakini matatizo haya hayatokei mara kwa mara.
Matatizo hujitokeza pale kila mmoja wa wanandoa anaporithi magonjwa ya urithi kutoka kwa wazazi wapo.
Ni kwanini maumbile ni muhimu sana kwa ndugu
Ndugu kutoka katika familia moja wanakiwango cha juu cha jeni zinzazofanana . Molekuli pia ni mhumili unaodhibiti mwili.
Jeni hutengeneza na kudhibiti rangi ya macho na ukubwa pamoja na ukubwa wake pamoja na ukubwa wa miguu , mikono yetu na sehemu nyinginezo za mwili.
Mambo mengi huwa tunayarithi kutoka kwa wazazi wetu , sawa na tunavyorithi magonjwa kutoka kwao, kupitia jeni zao.
Hii inaweza kuathiri jamii nyingi, lakini athari hizi huzipata familia zenye ndoa kati ya ndugu wa damu au ukoo mmoja.
Kuzaliwa kwa mtoto mwenye ulemavu
NHS inasema kuwa kuna matatizo ya urithi ya kiafya katika jamii nyingi. Na katika jamii zinazooa wake wengi wana uwezekano mkubwa wa watoto wao kurithi matatizo hayo.
Kwa mujibu wa NHS jamii ya wazawa wa Pakistani nchini Uingereza wana uwezekano mkubwa wa kuoana miongoni mwa Umwao wana uwezekano wa kupata watoto wenye kasoro za kimaumbile.
Matatizo ya hutokea kunapokuwa na utofauti wa jeni katika familia na wazazi wote wawili wana jeni sawa. Kama katika familia wengine wanaoana kuna uwezekano wa watoto wao kurithi jeni hii kutoka kwa wazazi wote wawili.
Dkt Ibrahim amesema kwasababu tayari wazazi walikuwa katika familia na kuendelea kuoana, ugonjwa utaendelea kusambaa kupitia kizazi.
Magonjwa mengine ya urithi yaliyoelezewa na mtaalamu huyo kama matokeo ya ndoa ya watu wa familia moja ni pamoja na : magonjwa ya akili na ulemavu wa maumbile.
Kwamujibu wa daktari , utafiti umeonesha kuwa ndoa za watu wenye uhusiano wa damu yanaweza kuongeza magonjwa ya urithi kama vile shinikizo la damu.
Saratani ya macho
Ndoa za watu wenye uhusiano wa damu wanaweza kusababisha saratani mbali mbali za macho kwa vizazi vyao , kwa mujibu wa afisa wa udhibiti wa saratani nchini Nigeria, Dkt. Ramatu Hassan katika mahojiano na BBC.
Ugonjwa huo hujitokeza katika eneo la jicho inayomsaidia mtu kuona, halafu mtoto huurithi na inaendelea kukua, wakati mtoto anapoanza kutembea.
Kwa mujibu wa daktari , ndoa za watu wenye undugu wa damu huwasababishia watoto matatizo kama hayo.
Unaweza pia kusoma:
Maeneo yenye ndoa nyingi za ndugu wa damu kama vile kaskazini mwa Nigeria yana idadi kubwa ya magonjwa ya urithi , anasema daktari.
"Aina hii ya saratani ya macho ni jambo la kawaida kwa watoto wachanga , na hutokea mara nyingi miongoni mwa watoto wanaozaliwa kwa wazazi wenye undungu na hivyo kuendelea katika vizazi hadi vizazi, '' anasema.
Wataalamu wa afya wanasema ni muhimu watu wapate taarifa kuhusu magonjwa ya urithi yanayowapata ndugu wenye uhusiano wa damu wanapooana na umuhimu wa jeni kati ya ndugu.