Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Je kutakuwa na chanjo zaidi ya moja dhidi ya virusi vya corona?
Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kampuni za Pfizer and BioNtech na Moderna zimetangaza ufanisi wa majaribio ya chanjo ya Covid-19.
Kampuni nyingine zinaendelea kutengezwa, wakati majaribio kubwa la tatu - kutoka kampuni ya Ubelgiji, Janssen - likiendelea nchini Uingereza.
Kwa nini tunahitaji chanjo?
Ikiwa unataka maisha yarejee kama ilivyokuwa, basi tunahitaji chanjo.
Hata sasa, watu wengi wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa virusi vya corona. Ni vizuizi tu katika maisha yetu ambavyo vimeepusha watu zaidi kufariki.
Lakini chanjo inaweza kufundisha miili yetu kupigana na maambukizi kwa njia salama. Inaweza kutukinga dhidi ya virusi vya corona au kufanya Covid kutokuwa hatari kwa maisha.
Kuwa na chanjo , pamoja na utaratibu mzuri wa matibabu ndio ''njia'' pekee ya kukabiliana na janga la corona.
Ni chanjo zipi zina uwezo wa kufaulu?
Pfizer/BioNtech ni kampuni ya kwanza ya dawa kutoa maelezo kuhusu awamu ya mwisho ya kufanyia majaribio chanjo yake.
Matokeo yake inaashiria kuwa chanjo hiyo inaweza kumkinga mtu kutokana na Covid- 19 kwanza asilimia 90.
Karibu watu 43,000 wamepewa chanjo hiyo na hakuna visa vya hofu ya usalama wake vilivyoripotiwa.
Moderna ilifanyia majaribio ya chanjo yake kwa watu 30,000 nchini Marekani, ambapo nusu ya watu hao walidungwa sindano ya majaribio.
Inasema chanjo yake inatoa kinga ya asilimia 94.5 baada ya kutumiwa na watu watano wa kwanza kati 95 waliokua wameonesha dalili ya maambukizi ya Covid kupokea chanjo hiyo.
Matokeo ya majaribio ya chanjo inayotengenezwa na kampuni ya dawa ya Uingereza AstraZeneca na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Oxford, yanatarajiwa kutolewa katika kipindi cha wiki chache zijazo.
Wakati huo huo data ya kutia moyo kuhusu chanjo ya Urusi inayofahamika kama Sputnik V Pia imetolewa.
Kulingana na matokeo ya awali ya awake ya tatu ya majaribio, sawa na away iliyofikiwa na chanjo ya Pfizer, watafiti wa Urusi wanaripoti kuwa chanjo ubora wa chanjo yao kufikia asilimia 92.
Ni chanjo zipi nyingine zinazotengenezwa?
Matokeo kutoka kwa wataalamu wengine wanaoendelea na majaribio ya chanjo pia yanatarajiwa katika muda wa wiki kasha au mizen michache ijayo.
Majaribio ya Janssen imeanza kuwaandikisha watu 6,000 note nchini Uingereza. Chi zingine zitajiunga na mango huo na kufikisha hadi watu 30,000 watakaofanyiwa majaribio ya chanjo.
Kampuni hilo tayari inaandaa kufanya majaribio ya chanjo yake dhidi ya watu wengi, ambapo watu awatakaojitolea kushiriki watapokea dozi moja. Mpango huo ni wa kutathmini ikiwa dozi mbili zitasidia kuimarisha kinga ya mwili.
Chanjo zingine kadhaa ziko katika awamu ya mwisho ya majaribio, ikiwa ni pamoja na ili iliyotengenezwa na Taasisi ya bidhaa za biolojia ya Wuhan na Sinopharm nchini China, na ya Taasisi ya Utafiti Gamaleya nchini Urusi.
Hata hivyo, majaribio yaliyofanywa nchini Brazil dhidi ya dawa iliyotengenezwa kampuni ya China ya Sinovac imesitishwa baada ya kuripoti ''athari mbaya'' inayoaminiwa kusababisha kifo cha mtu aliyejitolea kushiriki mpango wa majaribio.
Chanjo itapatikana lini?
Pfizer inaamini ina uwezo wa kusambaza dozi milioni 50 ya chanjo note duniani kufikia mwisho wa mwaka huu, na karibu dozi bilioni 1.3 billion kufikia mwisho wa mwaka 2021.
Uingereza inatarajiwa kupata dozi milioni 10 kufikia mwisho wa mwaka 2020, huku nyingine milioni 30 zaidi zikiwa tayari zimeagizwa.
Astra Zeneca/Oxford imekubali kusambaza dozi milioni 100 ya chanjo yake nchini Uingereza pekee na zingine bilioni mbili duniani endapo zitathibitishwa kupata ufanisi.
Waziri wa Afya Matt Hancock amesema Uingereza imefikia ''mkataba wa awali" wa kununua dozi milioni tano ya chanjo ya Moderna, ambayo itatolewa hivi karibuni.
Chanjo zinazotengenezwa zina tofauti gani?
Lengo la chanjo ni kugundua uvamizi wa vurusi mapema na kwa njia salama kupitia mfumo wa kinga, ambao unatambua mvamizi na kujua jinsi ya kupigana nae.
Kuna njia nyingi ya kufanya hivyo.
Pfizer/BioNtech (na Moderna) wametengeneza chanjo inayofahamika kama RNA. inatumia mfumo wa majaribio, ambao unahusisha kudunga sehemu maumbile ya kirusi katika mwili wa mwanadamu, ili kupatia mafunzo mfumo wa kinga ya mwili.
Chanjo ya Janssen kwa upande mwingine inatumia virusi vya mafua ambavyo vimefanyiwa mabadiliko ili kuzifanya kuwa salama na ambavyo vinafanana na virusi vya corona katika kiwango cha kwanza. His inasaidia mfumo wa kinga kuigundua na kukabiliana nayo
Chanjo ya Oxford na Urusi pia zinatumia virusi vilivyoambukizwa nyani, na kuguza muundo wake ili ifananne na virusi vya corona kujaribu kupata matokeo .
Miili kati ya chanjo kuu zilizotengenezwa China zinatumia virusi halisi lakini zikiwa katika hali ambayo imedhibitiwa ili kuzuia maambukizi.
Kuelewa ni njia gani inayoleta matokeo bora itakuwa muhimu. Majaribio ya chanjo ambayo watu huambukizwa virusi makusudi, inaweza kusaidia kujibu maswali haya.
Ni nini bado kinastahili kufanywa?
•Majaribio lazima yaonesha kuwa chanjo ni salama
•Majaribio ya kimatibabu lazima yaoneshe kuwa chanjo inaweza kuwakinga watu na magonjwa au angalau kupunguza idadi ya wanaofariki.
•Uwezo wa kutengeza chanjo unastahili kuwa juu kwasababu ikipata ufanisi kampuni zitahitajika kutengeza mabilioni ya chanjo husika
•Mamlaka za udhibiti wa dawa zinatakiwa kuidhinisha chango kabla ianze kupeanwa
•Inadhaniwa kuwa kati ya 60-70% ya idcdi ya watu duniani lazima wapate kinga ya kuzuia kuenea kwa virusi.