Uchaguzi wa Marekani 2020: Vichwa vitatu vya matokeo ya uchaguzi wa Marekani vinavyotarajiwa

Uchaguzi wa Marekani hatimaye umefika hapa. Ni sawa na hatua ya mwisho katika mashindano ya mbio za Olimpiki ya masafa marefu ambapo wanariadha wanaingia uwanjani kumaliza mita 400 za mwisho. Awamu hiyo ya mashindano ni ngumu sana kwa wanariadha kwasababu wamechoka, wanaumwa na misuli ya mwili lakini wanahitajika kukimbia mbio ili wakamilishe mashindano.

Imekuwa hali ya kushangaza wakati mwingine ya kubabaisha (nani aliyetarajia kutokea kwa janga la corona?) kufanya kampeni ukiwa na hofu nini kitakachofuata baadaye wakati lakini kila kitu kiko wazi kwangu.

Kuna matukio matatu yanayoweza kutokea, nna sia ajabu moja kati ya matukio haya ikawa ukweli kama inavyobashiriwa ( alafu kuna uwezekano wa tukio la nne, lakini nitaangazia hilo baadaye).

Nimeripoti taarifa kadhaa kumhusu rais Trump, ikiwa ni pamoja na wakati alipofutulia mbali ziara ya kitaifa kama hatua ya kulipiza kisasi; baada ya kujilikana alimlipa nyota wa filamu za ngono kabla ya uchaguzi uliyopita; Baada ya kuwa naye Helsinki na kumsikiliza akisema anamuamini Rais wa Urusi Vladimir Putin ambaye alikuwa amesimama kando yake kuliko anavyamini shirika lake la ujasusi; nimeshuhudia akichunguzwa, akikabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye hadi alipondolewa hatiani; nimemuangazia gari lililokuwa limembeba likiendeshwa karibu yangu kwenda hospitali Walter Reed alipokuwa ameambukizwa virusi vya corona; nimeitwa "mrembo mwingine", kwasababu nilisema natoka BBC, Nimegundua kwamba lolote linaweza kutokea, na mara nyingi hutokea.

Wacha tuangazie mazingira matatu yanayoweza kuamua uchaguzi huu.

1. Biden aibuka mshindi

Kwanza kabisa ikiwa matokeo ya kura ya maoni itakuwa kweli basi Joe Biden ataibuka mshindi usiku wa Jumanne.

Nimefanya kura ya maoni msimu huu wa uchaguzi huu na imekuwa rahisi sana kupata maoni ya watu kwasababu unaweza kubashiri jibu litakuwa nini kama vile utabiri wa hali ya hewa: "Leo kutakuwa hali ya joto jingi na jua kali, na kesho pia tunatazamia kutakuwa na joto na jua vile vile."

Kwa mara ya kwanza katika kampeni hii- kura ya kitaifa ya maonei ambayo ni muhimu kwa taifa hili imekuwa ikitabirika moja kwa moja. Hakuna kilichofanyika. Hakuna kilichobadilika. Biden ameongoza katika kura ya maoni kote nchini, akapata ushindi mdogo katika majimbo ya Florida, Arizona na North Carolina, na kupata viwango sawa katika maeneo ya kaskazini ya viwandani - Wisconsin, Michigan na Pennsylvania.

Ukienda kwenye blogi ya FiveThirtyEight blog, ambapo wanaweka wastani wa kura zote za kawaida, wanasema kumekuwa na uimarishaji katika kinyang'anyiro hiki kwa aslimia 0.1.

Tunaporipoti kura za maoni kawaida tunasema kuna dosari cha 3% +/-. Na mabadiliko 0.1% tu kwa wiki kadhaa hayawezekani. Kwa hivyo ikiwa Jumanne usiku hii itakuwa matokeo, sitashangaa hata kidogo.

2. Ushindi wa kushutua kwa Trump

Hoja hiyo inanileta katika mazingira ya pili ambayo huenda ikaamua matokeo ya uchaguzi wa Marekani. Ni kama mwaka 2016 kura za maoni hazipo sahihi kuhusu ushindi Donald Trump katika muhula wa pili. Kitakachoamua ufanisi wake ni kile kitakachofanyika Pennsylvania na Florida.

Hakuna mtu anayeamini kura ya maoni inayomuonesha Biden akiwa na kifua mbele kwa alama tatu au nne katika jimbo la Sunshine - na ushindani ni wa hali ya juu zaidi ya Florida. Na mwaka 2020 Trump anafanya vyema zaidi katika uungwaji mkono wake na jamii ya walatino s ikilinganisjhwa na mwaka 2016.

Sawa na Pennsylvania, ambako katik amajimbo ya magharibi yaliyo na wazungu wengi, wapiga kura wanaofanya kazi huenda wakamtosa.

Katika uchaguzi huu uliodhibitiwa na Covid, nimekuwa Florida, Ohio, Tennessee, Pennsylvania, North Carolina, Georgia na Virginia. Kila nilipoenda unapatana na wafuasi wa Trump ambao wanampenda rais wa 45 wa Marekani kupita maelezo.

Mpango wa kampeni ya Trump ni sawa na ule wa mwaka 2016 - wa kuwashawishi watu kujitokeza kwa wingi kupiga kura "wengine hawakushiriki kura ya maoni ", kwa hivyo hawakuangaziwa - wanapanga kufanya hivyo tena.

Pia nataka kusema kitu kimoja kuhusu mikutano ya kampeni ambayo Rais amekuwa akifanya wakati wa janga la corona.

Wapinzani wake wa chama cha Democratic wamekuwa wakimkosoa kwa kutojali maisha ya watu anapoamua kuwaleta pamoja maelfu ya watu bila kuzingatia kanuni ya kutokaribiana wakati huu wa janga la corona. Sitaki kujiingiza katika mjadala huo. Lakini ni vyema ifahamike kuwa kampeni yake imetumia ujanja wa hali ya juu.

Kuhudhutria mkutano huo watu walihitajika kujiandikisha mtandaoni, baada ya hapo oparesheni ya kupata maelezo ya kina kuwahusu ilifanywa ili kubaini ikiwa wamejiandikisha kupiga kura kutokana na mkutano huo au la, na kwa kufanya hivyo wanatafuta mbinu ya kuhakikisha malalamiko yatashughulikiwa endapo watapiga kura ambayo italeta mabadiliko.

Sababu nyingine ambayo huenda isinishangaze Trump akishinda ni kwamba Joe Biden mzungumzaji ambayo anawavutia watu katika kampeni zake.

Ikiwa kuna mtu anayewawakilisha wazee, basi yeye ni mfano mzuri. Uzee ni hali inayomkabili kila mtu, lakini rais anaonekani kuwa mchangamfu kuliko Biden, japo wameachana kwa miaka mitatu tu. Sio kwamba Biden hana "matumaini" aliyopata kutoka kwa kauli mbiu ya Obama mwaka 2008. Neno analotoa ni "nope", mimi Donald Trump.

Lakini "nope" ni neno lenye nguvu sana mwaka 2020.

Sio kwamba watu wanamtaka Biden, lakini wamechoshwa na utawala huu wa makelele ambao umegawanya vibaya Wamarekani

3. Biden- kupara ushindi wa kishindo

Mazingira ya tatu ambayo huweenda yakaamua matokeo ya uchaguzi wa wa marekani ni sawa na ya pili -kura ya maoni kutokuwa sahihi. Tofauti ni kwamba mara hii kura hizo sio sahihi kuelekea upande mwingine. Sio ya uwezekano wa Biden kushinda tu, bali kushinda kwa kishindo; utakuwa ushindi wa ajabu, kama ule wa Ronald Reagan dhidi ya Jimmy Carter mwaka 1980. Au ushindi wa George HW Bush dhidi ya Michael Dukakis mwaka 1988.

Rais amefanya kampeni ya mwisho katika wiki ambayo umeshuhudia ongezeko la juu la viwango vya maambukizi ya virusi vya corona, huku idadi ya watu waliolazwa hispitali ikiongezeka, vifo vikongezeka hadi elfu moja kwa siku. Pia soko la hisa limekabiliwa na hali mbaya zaidi ya uuzaji wiki hii tangu mwezi Machi - kipimo cha hali kiuchumi kinachoangaziwa na rais kwa dhati.

Tofauti na mwaka 2016, ambapo Donald Trump alikuwa na ujumbe wa wazi kwa watu wa Marekani - alitaka kujenga ukuta, kuwafungia nje Waislamu, alitaka kujadili tena mikataba ya biashara, alitaka kurudisha shughuli ya utengenezaji- mwaka 2020 alijikakamua kujieleza katika muhula wa pili atawafanyia nini.