Siri ya makaburi ya zamani yaliyozikiwa watu wa familia moja yagundulika

Wanaakiolojia wametumia uchambuzi wa vinasaba kugundua siri ya eneo la maziko yaliyokuwepo kwa karne kadhaa iliyopewa jina ''Chifu wa vichwa sita'' iliyokuwepo kwa karne.

Kaburi lililokuwa kwenye eneo la Portmahomack eneo la nyanda za juu lina mtu mwenye jeraha la kupigwa panga kwenye fuvu lake.

Alizikwa na mafuvu manne kabla kaburi lake kufukuliwa baadae ili kumzika mtu wa pili, huku mtu mwingine wa tatunakiwa amezikwa katika kaburi la karibu.

Uchambuzi umebaini kuwa baadhi ya mabaki ni vizazi vya familia moja.

Mabaki yote yanaanzia tarehe moja hadi mwishoni mwa karne ya 13 hadi mwanzoni mwa karne ya 15.

Eneo la maziko la Chifu wa vichwa sita lilikuwa miongoni mwa makaburi kadhaa yaliyochimbwa na wanaakiolojia katika eneo la Kanisa la kati la Mtakatifu Colman, Tarbat Ness , nyanda za juu za Easter Ross.

Mazishi yalifanyika wakati wa vita kati ya koo zinazopingana.

Tangu uchimbaji mnamo 1997, wanaakiolojia kutoka Chuo Kikuu cha York na Urithi wa FAS wamekuwa wakijaribu kutoa mwanga kuhusu mabaki kama sehemu ya Programu ya Ugunduzi wa Tarbat.

Chombo kinachochunguza Mazingira ya kihistoria ya Scotland kinaunga mkono uchambuzi wa vinasaba vipya vya eneo la Chifu wa vichwa sita.

Wanaume wawili ambao walizikwa kwenye kaburi moja ni ndugu na wanaakiolojia wanaamini kuwa wanaweza kuwa mabinamu wa kwanza watakapoondolewa.

Mafuvu manne ''zaidi'' ni ya mwanamke na wanaume watatu, mmoja kati ya wanaume hao anaaminika kuwa mtawa ambaye fuvu lake lilikuwa limetoka katika eneo la makaburi ya watu wa kidini.

Mafuvu mengine ya wanaume yalikuwa ya baba na mtoto, kwa upande mwingine Babu na baba wa mtu wa pili kuzikwa kwenye kaburi na mtu wa kwanza. Mwanamke alikuwa mama wa mtu wa pili.

Mtu wa tatu kuzikwa kaburi la karibu yao anadhaniwa kuwa mtoto wa kiume wa mwanaume wa pili .

Dkt Lisa Brown, wa taasisi ya Historic Environment Scotland, amesema uchambuzi umesaidia kutoa mwanga kuhusu mahusiano ya watu hao waliozikwa katika mazingira hayo.