Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Makala ya Korea Kaskazini inayofichua mipango ya kukwepa vikwazo
Makala mpya iliyo na wahusika wa kushangaza inadai kutoa mwangaza kuhusu juhudi za Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya kimataifa, kwa kuwadanganya washirika wa utawala wa siri wa Kim Jong-un kutia saini mikataba bandia ya silaha.
Filamu hiyo inaonesha mpishi wa Kidenmark aliyeacha kazi kutokana udikteta wa kikomunisti; mtu mashuhuri wa Uhispania na mwenezaji wa propaganda wa Korea Kaskazini na mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa na muuzaji wa cocaine aliyehukumiwa ambaye anacheza kama mtu wa siri wa kimataifa.
Lakini inaweza kuwa kweli? Afisa mmoja wa zamani wa UN aliiambia BBC kuwa aliiona kuwa "ya kuaminika sana".
Filamu hiyo, inayoitwa Mole, ni kazi ya mtengenezaji wa filamu wa Denmark Mads Brügger, ambaye anasema alipanga operesheni ngumu ya miaka mitatu kudhihirisha jinsi Korea Kaskazini inavyopuuza sheria za kimataifa.
Mpishi wa nje ya kazi aliyevutiwa na udikteta wa kikomunisti ni Ulrich Larsen, ambaye, kwa msaada wa Brügger, anaingia katika Chama cha Urafiki cha Korea, kikundi kinachounga mkono serikali nchini Uhispania. Larsen anapanda ngazi na mwishowe anapata uaminifu wa maafisa wa serikali ya Korea Kaskazini.
Uanachama wa KFA unamfanya Larsen kuwasiliana na mwanzilishi mwenza na rais Alejandro Cao de Benós, mtu mashuhuri wa Uhispania anayejulikana ulimwenguni kote kama "Mlinda lango wa Korea Kaskazini".
Wakati wa filamu, ambayo wakati mwingine huonekana katika sare ya jeshi la Korea Kaskazini, Cao de Benós anajivunia ufikiaji na ushawishi wake kwa serikali huko Pyongyang.
Halafu kuna Jim Latrache-Qvortrup, anayeelezewa kama mwanajeshi wa zamani la Ufaransa na aliyeshtakiwa kwa kuwa mfanyabiashara wa dawa za kulevya cocaine. Latrache-Qvortrup ameajiriwa kucheza sehemu ya muuzaji wa silaha wa kimataifa.
Akivuta kamba ni Brügger mwenyewe, ambaye anajiita "bwana kibaraka". Anadai kuwa ametumia miaka 10 kufanya kazi kwenye filamu yake - kwa sasa utengenezaji wa pamoja na watangazaji wa BBC na watangazaji wa Scandinavia.
Filamu hiyo ni ya kuchekesha, ya kutisha na wakati mwingine ni ya kuaminika . "Mimi ni mtengenezaji wa filamu ambaye anatamani hisia," Brügger anakiri katika filamu hiyo.
Lakini Hugh Griffiths, ambaye alikuwa mratibu wa Jopo la Wataalam la Umoja wa mataifa kuhusu Korea Kaskazini kati ya 2014 na 2019, aliita ufunuo huo katika filamu hiyo kuwa "ya kuaminika sana".
"Filamu hii ni aibu kali zaidi kwa Mwenyekiti Kim Jong-un kuwahi kutazamwa," Griffiths alisema. "Kwa sababu tu inaonekana ya kuwa si kamilili haimaanishi kuwa kusudi la kuuza na kupata mapato ya fedha za kigeni haipo. Vipengele vya filamu vinahusiana kweli na kile tunachokijua tayari."
Korea Kaskazini imekuwa chini ya vikwazo vya UN tangu mwaka 2006 kwa sababu ya mipango yake ya nyukilia - maendeleo na majaribio yake yameandikwa katika ripoti za kawaida na Jopo la Wataalam tangu mwaka 2010. Lakini ni jambo la kawaida kuona viongozi wa Korea Kaskazini, kwenye filamu, wakijadili jinsi ya kukwepa vikwazo ili kusafirisha silaha nje.
Katika wakati mmoja muhimu katika filamu, Ulrich Larsen, mpishi wa zamani na "Mole" wa jina hilo, filamu kama Jim Latrache-Qvortrup, au "Bwana James" muuzaji wa silaha, anasaini mkataba na mwakilishi wa kiwanda cha silaha Korea Kaskazini, na maafisa wa serikali walikuwepo. Mkutano huo unafanyika katika eneo la chini la mgahawa wa gaudy katika kitongoji cha Pyongyang.
Sio Wakorea wote waliopo wanaotambuliwa vizuri, na walionekana wakicheka pamoja baadaye, Latrache-Qvortrup anasema ilibidi abuni jina la kampuni wakati akiulizwa maswali magumu na mmoja wa maafisa wa Korea. Inaonekana ni ajabu timu hiyo isingeweza kutoa mawazo yoyote ya hapo awali kuhusu maelezo ya msingi kama hayo, kama vile ilivyodhania kufikiria kwamba maafisa wa kweli wa Kikorea wangeruhusu mkutano huo kupigwa picha na hati zisainiwe na kubadilishwa.
Nyaraka zilizosainiwa zina saini ya Kim Ryong-chol, rais wa Shirika la Biashara la Narae.
Narae ni jina la kawaida katika Rasi ya Korea, lakini ripoti ya hivi karibuni ya Jopo la Wataalam wa UN, ya tarehe 28 mwezi Agosti 2020, inasema kwamba kampuni inayoitwa Korea Narae Trading Corporation "inahusika katika shughuli zinazohusiana na vikwazo kwa kukwepa mapato ambayo inasaidia shughuli zilizokatazwa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea ".
Griffiths, afisa wa zamani wa UN, amesema kwamba Wakorea waliokuwepo walikuwa wako tayari kushughulika na mfanyabiashara wa binafsi ambaye hawakujua chochote kumhusu.
"Inaonesha kuwa vikwazo vya UN vinafanya kazi. Wakorea wa Kaskazini ni wazi wana hamu ya kuuza silaha zao," alisema.
Wakati wa mkutano huko Kampala mnamo 2017, Latrache-Qvortrup anaulizwa na "Bwana Danny" (anayeelezewa kama "muuzaji wa silaha wa Korea Kaskazini") ikiwa ataweza kupeleka silaha za Korea Kaskazini kwa Syria. Swali hilo linaonyesha ugumu unaozidi kuongezeka wa Korea Kaskazini kufanya jambo hili kwa wenyewe, Griffiths alisema.
"Bwana James" yuko nchini Uganda, akifuatana na maafisa wale wale wa Korea Kaskazini walioonekana Pyongyang, kujadili ununuzi wa kisiwa katika Ziwa Victoria.
Maafisa wa Uganda wameambiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa eneo la kifahari la mapumziko, lakini Bwana James na Wakorea wanapanga kwa siri kujenga kiwanda cha chini ya ardhi ili kutengeneza silaha na dawa za kulevya.
Tena, inaonekana kuwa ya kupendeza, lakini Korea Kaskazini imefanya jambo la aina hii hapo awali.
Utawala huo ulijenga kiwanda cha risasi katika mgodi wa shaba uliokuwa ukitumika katika Bonde la Leopard nchini Namibia. Inaonekana, walikuwa nchini kujenga sanamu na makaburi.
Shughuli za Shirika la Biashara ya Maendeleo ya Madini ya Korea (Komid) zilichunguzwa na Jopo la Wataalamu la UN kati ya 2015 na 2018. Shinikizo la UN kwa Namibia linaweza kusaidia kuelezea ni kwanini Wakorea Kaskazini, ambao katika filamu hapo awali walipendekeza kujenga huko tena, walibadilisha mawazo yao kwenda Uganda, alisema Griffiths.
"Miradi ya Korea Kaskazini nchini Namibia ilifungwa ," afisa huyo wa zamani wa UN alisema.
"Kufikia mwaka wa 2018, Uganda ilikuwa moja ya nchi chache sana za Kiafrika… ambapo madalali wa silaha wa Korea Kaskazini bado wanaweza kusafiri kwa mapenzi yao."
Kipengele kingine cha filamu hiyo inayowavutia waangalizi wa kimataifa ni kuhusika dhahiri kwa wanadiplomasia wa Korea Kaskazini walioidhinishwa katika balozi za nje ya nchi katika kuwezesha juhudi za kukiuka vikwazo vya UN.
Wakati mmoja Ulrich Larsen anatembelea ubalozi wa Korea Kaskazini huko Stockholm, ambapo anapokea bahasha ya mipango ya mradi huo nchini Uganda kutoka kwa mwanadiplomasia aliyeelezewa kama Bw. RI
Kama matukio mengi muhimu ya makala hayo, mkutano huo umepigwa picha kwa siri na Larsen. Wakati akiondoka, Bw Ri anamuonya kuwa awe msiri
"Ikiwa kitu kitatokea, ubalozi haujui chochote juu ya hili, sawa?" Bwana Ri anasema.
"Uchunguzi mwingi wa vikwazo uliofanywa na Jopo la UN uligundua kuwa majengo ya kidiplomasia ya Korea Kaskazini au wamiliki wa pasipoti walihusika katika ukiukaji huo," alisema.
Hakuna biashara yoyote iliyojadiliwa kwenye filamu hiyo iliyofanikiwa.
Hatimaye, washirika wanapoanza kudai pesa, Brügger anamfanya "Bwana James" atoweke. Watengenezaji wa filamu wanasema ushahidi wao umewasilishwa kwa ubalozi wa Korea Kaskazini huko Stockholm, lakini hakukuwa na majibu.
Cao de Benós, mwanzilishi wa KFA, alisema kwamba alikuwa "akiigiza uigizaji" na kwamba filamu hiyo ilikuwa "ya upendeleo,iliyopangwa".