Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
China yafanya mazoezi ya kijeshi karibu na mlango wa bahari wa Taiwan ''kulinda mamlaka yake''
China imesema kuwa inafanya mazoezi ya kijeshi karibu na mlango wa bahari wa Taiwan ili ''kulinda mamlaka yake'' wakati maafisa wa Marekani wakitembelea Taiwan.
Mazoezi ya kijeshi yanafanyika wakati kukiwa na mvutano kati ya Beijing na Washington, na wakati Marekani ikihimiza masaada wake kwa kisiwa hicho.
China inaichukulia Taiwan inayojitawala kama jimbo lililojitenga.
Keith Krach ni afisa wa Juu kutoka Wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuzuru kisiwa hicho kwa miongo kadhaa.
Siku ya Ijumaa, Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini China Ren Guoqiang ameishutumu Marekani na Taiwan kwa ''ushirika wao wenye hila na kusababisha migongano'', ingawa hakuzungumzia ziara hiyo.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa ''kuitumia Taiwan kuidhibiti China'' au ''kutegemea nchi za kigeni kujiimariha'' ni mawazo ya kufikirika.
Mazoezi ya kijeshi yalikuwa ''halali na muhimu kwa eneo la bara kwa ajili ya kulinda himaya na uaminifu '', alisema.
Bwana Krach, ambaye, yuko chini ya Waziri wa Marekani anayeshughulikia masuala ya uchumi, atakutana na rais wa Taiwan Tsai Ing-wen baadae Ijumaa.
Ingawa Marekani haina mahusiano rasmi ya kidiplomasia na Taiwan, sheria ya mahusiano ya mwaka 1978 inaruhusu Marekani kuuza silaha kwenye kisiwa hicho, na kufanya kuwa ''mahusiano ya karibu''