Uchaguzi Marekani 2020: Trump amesema Biden atamkasirisha Mungu
Raia wa Marekani Donald Trump amesema kuwa "Joe Biden anakwenda kinyume na Mungu", akiongeza matamshi ya kumvamia mpinzani wake wa chama cha Democratic na kutabiri uchaguzi utakuwa na mapambano makali ya kisiasa.
Matamshi ya Trump aliyoyatoa wakati wa ziara yake Ohio, yanawadia wakati akijaribu kuingia katika eneo muhimu la majimbo ya Midwestern ambako kulikuwa na mchango mkubwa katika kupata ushindi wake 2016.
"Anampinga Mungu. Anapinga bunduki," amesema rais mwanachama wa Republican.
Bwana Biden, mwenye imani kubwa ya Kikatoliki, atakuwa anakabiliana na Bwana Trump katika uchaguzi wa Novemba.
Kura za maoni zinaashiria kwamba sasa hivi chama cha Democratic kiko kifua mbele.
Aliyekuwa makamu rais wa Marekani amezungumza mara kadhaa kuhusu vile imani yake ilivyomsaidia kukabiliana na vifo vya mke wake wa kwanza na binti yake katika ajali ya gari 1972.
Msemaji wa kampeni yake Andrew Bates amesema katika taarifa Alhamisi: "Imani ya Joe Biden ndio msingi wa vile alivyo yeye; ameishi kwa heshima na taadhima katika maisha yake yote, na imekuwa chanzo chake kinachomfariji kipindi anachopitia magumu."

Chanzo cha picha, Getty Images
Awali akiwa Cleveland, Ohio rais alisema Bwana Biden: "Anafuata ajenda za wanasiasa wenye misimamo mikali wa mrengo wa kushoto.
Chukueni bunduki zenu, haribuni kufungu cha pili cha marekebisho. Hakuna dini, hakuna kitu chochote, ukidhuru biblia unamdhuru mungu.
"Atamkasirisha mungu, kampeni chafu za uchaguzi."
Bwana Trump ameshutumiwa kwa kutumia mtindo wa siasa za kurusha maneno katika mjadala uliofadhiliwa na fedha za walipa ushuru unaolenga kuzungumzia sera za serikali ya Maarekani.
Akiwa katika kiwanda cha kutengeneza mashine za kufua Alhamisi, rais aliendelea tu kumshambulia mpinzani wake kwa maneno makali.
"Siwezi kusema kuwa anafanya vizuri sana kwa kampeni," rais amesema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kampeni za Bwana Trump na Biden zimekuwa za kushutumiana kwamba mgombea wao ana matatizo ya akili.
Bwana Trump, 74 na Bwana Biden 77.
Katika tangazo lililotolewa na kampeni ya Bwana Trump wiki hii, mgombea wa Democrat alioneshwa kama "aliyejificha" peke yake eneo la chini ya ardhi, kwa kutumia picha ambayo imebatilishwa na watu wengine kuondolewa.
Dini ni suala ambalo liliwahi kujitokeza katika kampeni hii.
Bwana Biden alimshutumu rais kwa kufanya dhihaka kwa kutumia Bibilia katika picha iliyopangwa nje ya kanisa mapema Juni baada ya waandamanaji - walioelezewa na wanahabari.













