Uchaguzi Marekani 2020: Donald Trump amependekeza uchaguzi wa urais uahirishwe

Muda wa kusoma: Dakika 3

Donald Trump amependekeza uchaguzi wa urais uahirishwe.

US President Donald Trump (file pic)

Chanzo cha picha, Reuters

Donald Trump ametoa wito kuwa uchaguzi wa rais utakaofanyika Novemba uahirishwe akidai kuongezeka kwa upigaji kura kwa njia ya posta kunaweza kusababisha udanganyifu na matokeo yasiyo sahihi.

Kuna ushahidi mdogo wa madai ya Bwana Trump lakini kwa kipindi kirefu amekuwa akipinga upigaji kura kwa njia ya posta ambao anadai unaweza kusababisha udanganyifu.

Majimbo ya Marekani yanataka upigaji kura kwa njia ya posta kufanywa kuwa rahisi zaidi kwasababu ya wasiwasi wa matatizo ya kiafya kutokana na janga la corona.

Trump alisema nini?

Katika ujumbe wake kwa njia ya Tweeter, Bwana Trump amesema kupiga kura kwa njia ya posta kutafanya uchaguzi wa Novemba kuwa usio sahihi na wenye udanganyifu mkubwa katika historia ya nchi hiyo na aibu kubwa kwa Marekani.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Alisema hivyo bila kutoa ushahidi wowote kwamba kupiga kuta kwa njia ya posta kama inavyofahamika Marekani, kutahatarisha uchaguzi kuingiliwa na nchi za kigeni.

"Wanazungumza kuhusu uchaguzi kuingiliwa na nchi za kigeni lakini wanajua kwamba upigaji kura kwa njia ya posta ni njia rahisi ya nchi za kigeni kuuingilia," amesema.

Bwana Trump alisema njia hiyo tayari unadhihirisha kwamba hilo litakuwa matatizo tu katika maeneo ambayo imejaribiwa.

Mapema mwezi huu, majimbo sita ya Marekani yalikuwa yanapanga kufanya uchaguzi wa Novemba kwa njia ya posta: California, Utah, Hawaii, Colorado, Oregon naWashington.

Majimbo hayo yatatuma kura moja kwa moja kwa njia ya posta kwa wapiga kura wote waliosajiliwa, na baada ya hapo zitarejeshwa tena au kuwasilishwa siku ya kupiga kura - ingawa kupiga kura moja kwa moja bado kutakuwepo kwa wachache ambao hali italazimu kufanya hivyo.

Chini ya uchaguzi wa urais, Bwana Trump hana mamlaka yoyote ya kuahirisha uchaguzi yeye binafsi na tukio kama hilo ni lazima liidhinishwe na bunge.

Juni, New York iliruhusu raia kupiga kura kwa njia ya posta katika uchaguzi wa awali wa chama cha Democratic kumtafuta mgombea wa kupeperusha bendera ya chama. Lakini kuhesabiwa kwa kura kulicheleweshwa na hadi kufikia sasa matokeo bado hayajulikani.

Vyombo vya habari vya eneo vimesema kwamba pia kuna wasiwasi kuwa wapiga kura wengi hawatahesabiwa kwasababu hawakujazwa vizuri au pengine hawana alama zinazoonesha kwamba kura zao zilitumwa kabla ya siku ya upigaji kura kufikia ukomo wake rasmi.

Hata hivyo kuna majimbo mengi ambayo kwa muda mrefu sasa yamekuwa yakipiga kura kwa njia ya posta.

Uchaguzi na Anthony Zurcher, Mwanahabari wa BBC

Donald Trump hawezi kuchelewesha uchaguzi wa urais wa Novemba bila idhini ya bunge, ambalo kwa kiasi fulani linaongozwa na Democrats. Ikiwa pengine wakati anasema hivyo hakujua hilo bila shaka sasa hivi taarifa ameipata.

Rais pia anastahili kujua kwamba kwa kuandika ujumbe kwenye Twitter kuhusu uchaguzi uahirishwe au hata kama atasema "Nauliza tu!" - ana uhakika kwamba atasababisha cheche za kisiasa hasa baada ya kukataa mara kadhaa kusema ikiwa atakubali matokeo kama mambo yatamwendea mrama kwenye uchaguzi.

Trump anaonekana kufanya kila analoweza ndani ya uwezo wake kushusha uaminifu wa uchaguzi wa Novemba ambapo raia kadhaa wa Marekani inatarajiwa kwamba watategemea kupiga kura kwa njia ya posta kama hatua ya kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.

Mara kadhaa amekuwa akisema madai ya uongo na yenye kupotosha kuhusu kutegemewa kwa njia ya posta na kusema kwamba kutakuwa na ulaghai kutoka mataifa ya nje.

Wakosoaji wake wameonya kwamba huenda anatengeneza mazingira ya kupinga matokeo - ingawa pengine nia yake ni kuwa ni kisingizio iwapo atashindwa kwenye uchaguzi huo.

Ujumbe wa Trump wa Twitter Alhamisi asubuhi pia unaweza kuwa dhamira yake ni kutaka kubadilisha angalizo la watu kutoka kwa takwimu za uchumi za robo ya pili ya mwaka zilizotolewa hivi punde.

Amekuwa akitegemea sana uchumi kupata nafasi ya kuwika kwenye kampeni zake lakini jinsi takwimu hizo zilivyo, mambo huenda yamembadilikia.

Hata awe na sababu gani, kuandika ujumbe kuhusu uchaguzi sio njia ya mgombea yeyote ambaye ana imani kwamba atashinda kuitumia na huenda ikawa ishara ya njia zingine za ajabu ajabu zitakazofuata.