Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Amiba: Tahadhari yatolewa Marekani baada ya kubainika kwa ugonjwa usio wa kawaida
Ugonjwa wa amiba unaoathiri ubongo umethibitishwa huko Florida, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa jimbo hilo la Marekani.
Idara ya Afya Florida imesema kwamba mtu mmoja huko kaunti ya Hillsborough amepata maambukizi ya ugonjwa wa 'Naegleria fowleri' kwa kiingereza.
Maambukizi hayo ya amiba yanapoingia kwenye ubongo kupitia maji machafu yanayoingia kwa njia ya pua kawaida husababisha kifo.
Idara ya Afya haikusema maambukizi hayo yamepatikana wapi au hali ya mgonjwa.
Pia ugonjwa huu wa maambukizi ya kimelea ya amiba hauwezi kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
Maambukizi yamebainika katika majimbo ya kusini mwa Marekani na ni nadra sana kujitokeza huko Florida ambapo maambukizi 37 pekee ndio ambayo yamewahi kuripotiwa tangu 1962.
Maafisa wa Afya waliwataka wenyeji kuepuka kugusisha pua kwenye maji yanayotoka mferejini moja kwa moja au kupitia vyanzo vyingine.
Vyanzo hivyo ni pamoja na maji ya mtoni, kwenye ziwa, mifereji na vidimbwi ambapo maambukizi yana hatari zaidi ya kutokea msimu wa joto, Julai, Agosti na Septemba.
Waliopata maambukizi ya ugonjwa huu wa amiba wa 'Naegleria fowleri 'wana dalili za homa, kuhisi kuzinguzungu na kuhisi kutapika pamoja na shingo kukakamaa na kuumwa kichwa.
Wengi wao hufa ndani ya wiki mo
Wizaya ya Afya imetaka watu wenye dalili kama hizo kufika kwenye kituo cha afya mapema iwezekanavyo kwa sababu ugonjwa huo unaonekana kudhohofisha mtu haraka.
"Ugonjwa huu ni nadra na mikakati ya kuuzuia kutasaidia watu kuwa salama msimu wa joto," wizara ya afya imesema.
Maambukizi ya ugonjwa wa Naegleria fowleri ni nadra sana Marekani kulingana na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa na Kuzuia Maambukizi Marekani (CDC).
Lakini kati ya 2009 na 2018, maambukizi 34 yaliripotiwa nchini humo huku kati ya idadi hiyo, watu 30 inasemekana waliambukizwa kupitia maji.
Pia unaweza kutazama: