Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Xi Jinping: China kufuta mikopo isiokuwa na riba kwa mataifa ya Afrika
China itafuta mikopo isio na riba miongoni mwa mataifa ya Afrika ambayo inakaribia kuanza kulipwa mwisho wa mwaka huu 2020, rais Xi Jinping ametangaza.
Aliambia mkutano wa China na mataifa ya Afrika kuhusu Covid-19 siku ya Jumatano kwamba mataifa ya Afrika yalioathirika pakubwa na virusi vya corona pia yataongezewa muda wa kulipa mikopo hiyo.
Raia huyo wa China pia alizitaka taasisi za kifedha nchini mwake kufanya majadiliano ya kirafiki na mataifa ya Afrika kuweka mipango ya mikopo ya kibiashara kwa kuweka dhamana zilizo huru.
''China itafanya kazi na Umoja wa mataifa UN, Shirika la Afya Duniani WHO na washirika wengine kuisaidia Afrika kukabiliana na janga la Covid-19 , kwa njia ambayo itaheshimu matakwa ya Afrika'' , alisema Rais Xi Jinping.
Kuhusu Suala la virusi vya corona, amesema Afrika itakuwa miongoni mwa mataifa yatakayofaidika na chanjo iliotengenezwa China.
China pia itaendelea kujenga mahospitali barani Afrika.
Pia imesema kwamba itajenga kituo kikuu cha kudhibiti magonjwa CDC katika mji mkuu wa Ethiopia , Addis Ababa.
Jinsi uhasama kati ya Marekani na China ulivyojitokeza katika vita dhidi ya corona Afrika
Huku Afrika ikijiandaa kwa ongezeko la idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona , China na Marekani zinadai kuwa msaidizi mkubwa wa bara hili, lakini kuna mengi ambayo hayajaangaziwa katika uhasama huo zaidi ya kukabiliana na virusi hivyo kulingana na mwandishi wa BBC Andrew Harding.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo alisema kwamba hakuna taifa litakaloshindana na kile ambacho Marekani inakifanya katika kusadia Afrika kukabiliana na Covid-19.
Na aliendelea kusema kwamba hakuna taifa ambalo limesaidia ama litafanya zaidi ya kusaidia Afya duniani.
Bwana Pompeo alikuwa akizungumza katika mkutano na kundi dogo la wanahabari wa Afrika pamoja na wale waliopiga kambi barani Afrika.
Nilikuwa miongoni mwao.
Wakati huo - mwezi uliopita - Nilichukulia tamko lake la 'hakuna taifa litakavyofanya zaidi', sawa na matamshi yanayotumiwa kila siku na utawala wa rais Trump, ambao ulikuwa unajaribu kuimarisha uhusiano wake wa kimataifa kufuatia uamuzi wake wa kukata uhusiano na Shirika la Afya Duniani WHO katikati ya mlipuko mkubwa zaidi duniani.
Inasikitisha kusema kwamba $170m (£134m) za msaada ambazo bwana Pompeo anajigamba kuipatia Afrika zilishindwa na msaada wa bilionea mmoja wa China uliotolewa na Jack Ma.
lakini siku chache zilizopita, niliona habari kuhusu Afrika katika chombo kimoja cha habari kinachodhibitiwa na serikali, The global Times na nilikumbushwa kuhusu matamshi ya bwana Pompeo na kikanishangaza jinsi bara hili lilivyosukumwa katika kona moja ndogo ya vita baridi kati ya Washington na Beijing na kama ilivyokuwa awali katika vita vya baridi vilivyokuwa rasmi- mgogoro wa ghafla, kama ule wa virusi vya corona sasa umebadilishwa na kuwa mzozo fulani.
Shinikiza dhidi ya demokrasia ya vyama vingi
Habari hiyo ya Chombo cha habari cha Global Times ilijigamba kwamba mfumo wa China wa Kisiasa , ulifanikiwa katika kukabiliana na Virusi vya corona.
Na Baadaye likaendelea kusema kwamba huu ndio wakati ambao mataifa ya Afrika yanapaswa kusitisha utumizi wa mfumo wa vyama vingi unaotumiwa na mataifa ya magharibi - mfumo ambao chombo hicho kinasema kwamba umesasabisha ukosefu wa usawa kikabila na kidin, ghasia uharibifu wa maisha na mali. Badala yake Afrika inapaswa kufuata mfumo wa chama kimoja wa China.
Muda mchache baadaye niliona taarifa nyengine katika gazeti jingine linalodhibitiwa na serikali ya China , China Daily , lililosifu mchango wa China kujenga barabara barani Afrika , uwekezaji mkubwa na mkakati ambao ulikuwa unaliponya bara hili kutokana na utumwa wa muda mrefu wa ukoloni mambo leo na sasa janga la virusu vya corona.
Jibu la bwana Pompeo kwa hilo lilikuwa wazi. Chama tawala cha China kilikuwa kinailimbikizia Afrika madeni kwa masharti ya kuvutia hatua ambayo itaathiri raia wa Afrika kwa kipindi cha muda mrefu.
Siku chache baadaye nilipiga simu na kujiunga katika majadiliano ya mtandao wa Zoom kuhusu uhusiano wa Marekani na China barani Afrika -ulioelezewa na wasimamizi wa mkutano huo kama makabiliano hatari - na kumsikiza profesa mmoja wa China akisema kwamba virusi vya corona vilikuwa vinasaidia waandishi wa Afrika kuelewa umuhimu wa waandish wa China waliodhibitiwa.
Vyombo vya habari vya magharibi vinaangazia mabaya, habari hasi, alisema professa Zhang Yanqiu, lakini wasomaji walitaka kupatiwa habari njema zaidi wakati wa mlipuko huu.
Ili kuelewesha , alimaanisha kwamba anataka mfumo wa uandishi wa habari wa China unaongazia mambo mema .
Alisema kwamba hivi karibuni alivutiwa na mfumo wa waandishi wa Ethiopia.
lakini je uandishi wa Afrika unashawishika kwa urahisi?
Nilipomuuliza bwana Pompeo iwapo anadhani kwamba sura ya Marekani barani Afrika imeharibiwa na matamshi ya hivi karibuni ya rais Trump kuhusu matumizi ya dawa za kuuwa vidudu na mwanga wa miale ya UV kutibu corona, waziri huyo wa maswala ya kigeni hakujibu moja kwa moja lakini akasema kwamba matamshi ya bwana Trump hayakueleweka na yalibadilishwa na vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali.
Ulikuwa muda usio wa kawaida katika mkutano huo wa zoom.
Kwa miongo kadhaa diplomasia ya Maredkani imekuwa ikikuza na kulinda uhuru wa wanahabari Afrika dhidi ya uatawala wa kiimla na serikali zinazowadhibiti wanahabari.
Lakini sasa rais wa Marekani amekuwa akiwashutumu waandishi wa taifa lake kuwa feki, maadui wa watu na wasiofata maadili ya uandishi usiopendelea upande wowote.
Nikimsikikliza bwana Pompeo , nilihisi kwamba maoni ya Beijing na Washington kuhusu uandishi unaojenga hayana tofauti kubwa.
Trump 'anaeleweka vibaya'
Ni sawa kusema kwamba Marekani - kupitia mpango wa dharura wa rais wa zamani George Bush kuhusu msaada Pepfar umesaidia pakubwa kukuza afya barani Afrika.
lakini ni wazi kwamba China inatumia mlipuko wa corona na maovu yanayofanywa na Marekani ili kukuza ajenda yake ya kisiasa barani Afrika kwa ujasiri- nashuku na ufanisi.
Hio sio kusema kwamba kwamba mataifa ya Afrika - ama waandishi hutumika na mataifa yenye uwezo mkubwa.
lakini ni serikali ngapi barani Afrika, ambazo zinadaiwa na benki za China mbali na kuwa chini ya shinikizo la virusi vya corona zinaweza kujaribu kuufuta mfumo wa vyama vingi uliofeli na kuanza kutekeleza mfumo wa chama kimoja unaotumika na China?