China na India: Kwanini hofu imerudi kati ya majeshi ya mataifa haya yenye idadi kubwa ya watu duniani

Chanzo cha picha, Getty
Majeshi ya China na India yamejikuta katika makabiliano makali kwenye eneo la Himalayas, ambayo yanaweza kuongezeka zaidi wakati ambapo pande zote mbii zinajitahidi kuendeleza malego yake ya kimkakati.
Vyombo vya habari vya India vimenukuu maafisa wakisema maelfu ya wanajeshi wa China wameingia kwa lazima eneo la bonde la Galwan huko Ladakh, katika eneo lenye kuzozaniwa la Kashmir.
Ni wazi kwamba viongozi wa jeshi la India wanaopanga mikakati wameduwaza na hali hiyo
Taarifa zinaonesha kwamba mapema Mei, vikosi vya China viliweka vyandarua na kuchimba mahandaki pamoja na kuweka vifaa vya kivita kilomita kadhaa ndani ya kile ambacho India inakichukulia kama eneo lake.
Hatua hiyo inawadia wakati India inajenga barabara kuu ya kilomita mia kadhaa amayo inaunganisha kambi ya jeshi iliyofunguliwa tena mwaka 2008.

Chanzo cha picha, PRESS INFORMATION BUREAU
"Hali ni tete. China imeingia eneo ambalo wao wenyewe wanakubali kwamba ni la India. Hili limebadili kabisa hali ilivyo," anasema Ajai Shukla, mtaalamu wa masuala ya kijeshi wa India ambaye alihudumu kama kanali jeshini.
China ina maoni tofauti. Inasema kwamba India ndiyo ambayo imebadilisha hali iliyokuwepo awali.
Vyombo vya habari vya India vinadai kwamba wanajeshi kutoka pande zote wamekuwa wakikabiliana katika matukio kama mawili eneo la Ladakh.
Pia makabiliano yameripotiwa katika maeneo karibia matatu: bonde la Galwan, chemichemi za maji moto na ziwa Pangong lililopo kusini.

Chanzo cha picha, AFP
Majeshi yao, ambayo ni miongoni mwa makubwa zaidi duniani, yanakutana ana kwa ana katika maeneo mengi ya eneo hilo.
Kwa sasa hivi eneo hilo la mpakani linatenganishwa kwa mstari tu. Kwa sababu ya mito, maziwa na vilele vyanzo vyenye barafu, mstari unaotenganisha wanajeshi wa nchi hizo mbili unaweza kubadilika na mara nyingi vikosi vimekuwa katika hatari ya kujikuta kwenye makabiliano.

Chanzo cha picha, Reuters
India na China zina mpaka wa zaidi ya kilomita 3,440 na zimekuwa na maeneo ambayo zote zimekuwa zikidai kuyamiliki.
Doria zao mipakani mara nyingi huwa zinaingiliana na matokeo yake ni makabiliano ya mara kwa mara lakini pande zote mbili zinasititiza kwamba hazijawahi kurushiana risasi katika kipindi cha miongo kadhaa.

Chanzo cha picha, AFP
Wasiwasi ambao umetanda kati ya majeshi ya nchi hizo mbili sio tu kwamba ni katika eneo la Ladakh pekee. Wanajeshi kutoka pande zote mbili pia wanakutana ana kwa ana katika mpaka wa China na kaskazini mashariki mwa India jimbo la Sikkim.
Awali mwezi huu ilisemekana kwamba walikabiliana katika mapigano.
Na kuna mzozo juu ya ramani mpya iliyotolewa huko Nepal, ambayo pia inashtumu India kwa kuingilia eneo lake kwa kujenga barabara kuu inayouunganisha nchi hiyo na China.
Kwanini wasiwasi umeongezeka?
Kuna sababu kadhaa, lakini chanzo ni malengo ya kimkakati na pande zote mbili zinataka mwengine achukue jukumu.
"Mto wa Galwan kwa sasa hivi umekuwa angalizo kuu kwasababu uko karibu na barabara mpya iliyojengwa na India katika mto Shyok hadi kambi ya jeshi ya Daulat Beg, eneo la kijijini na lililo katika hatari kubwa ya kuathirika huko Ladakh, "anasema Shukla.

Umauzi wa India wa kuongeza miundo mbinu unaonekana kwamba ulikasirisha China.
Chombo cha habari vya China, Global Times: "Bonde la Galwan Valley ni eneo la China, mamlaka ya eneo inayodhibiti mpaka huo ilikuwa wazi kwa hilo."
"Kulingana na jeshi la China, India ndio ambayo imeingia kwenye eneo hilo kwa nguvu . Kwa hiyo India inabadilisha ile hali iliyokuwepo katika eneo hilo na hilo limekasirisha China" anasema dkt. Long Xingchun, rais wa Taasisi ya Chengdu ya Masuala ya Dunia (CIWA) ambayo ni jopo la ushauri.

Chanzo cha picha, AFP
Je hali inaweza kuwa mbaya kiasi gani?
"Mara nyingi majeshi ya pande zote mbili huwa yanashika doria katika eneo hilo. Na mara nyingi matukio kama hayo huwa yanatatuliwa katika kiwango cha jeshi la eneo.
Lakini safari hii, kumekuwa na wanajeshi wengi, " aliyekuwa mwanadiplomasia Stobdam, mtaalamu eneo la Ladakh katika masuala ya China na India.

Chanzo cha picha, AFP
"Makabiliano yanatokea katika maeneo ambayo ni ya kimkakati ambayo ni muhimu kwa India.."
"Ikiwa watadhibiti ziwa Pangong, eneo la Ladakh haliwezi kulindwa. Ikiwa jeshi la China litaruhusiwa kukita kambi katika eneo la kimkakati la binde la Shyok, basi huenda hata bonde la Nubra na Siachen yakaathirika, anasema.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya India, wanajeshi nchini humo walizidiwa na kuzingirwa pale China ilipojumuisha wanaume na mashine katika zoezi la kijeshi eneo hilo la mpakani.
Hatua hiyo ilizua wasiwasi huko Delhi, na India inanafasi finyu ya kukabiliana na hali hiyo.
Inaweza kushawishi China kupitia majadiliano ya kuondoa wanajeshi wake au kujaribu kuwaondoa kwa lazima.
Kati ya machaguo hayo hakuna ambalo ni rahisi.
"China ni ya pili kwa wanajeshi wengizaidi duniani. Kiteknolojia, inashinda India. Miundo mbinu yake kwa upande mwengine, imeendelea mno," anasema Ajai Shukla.
"Kifedha, China inaweza kugawanya raslimali zake kufikia malengo yake ya kijeshi huku uchumi wa India ukiwa umekuwa ukipitia shinikizo kubwa katika miaka ya hivi karibuni na janga la virusi vya corona limezorotesha kabisa hali hiyo," anaongeza.

Chanzo cha picha, AFP














