Waridi wa BBC: Je wajua kwamba kuishi na hali ya ulemavu wa ngozi ni tishio karne hii ya kizazi kipya

Grace Maria Nzomo aliye na ulemavu wa ngozi ni mwanamitindo

Chanzo cha picha, Maria Nzomo

    • Author, Anne Ngugi
    • Nafasi, BBC Swahili
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Grace Maria Nzomo ni Mwanamke wa miaka 26 kutoka Nairobi Kenya, anayejivunia mengi katika maisha yake hususan kwa kuwa yeye alizaliwa na ulemavu wa ngozi .

Ulemavu huu wa ngozi husababishwa na ngozi kushindwa kutengeneza viini vya melanin vinavyohusika kwa kiasi kikubwa na utengenezaji wa rangi ya ngozi ya kila binadamu

Licha ya kuwa baba na mama yake Grace Nzomo ni watu wenye rangi nyeusi , Grace alizaliwa akiwa na ngozi nyeupe , lakini sio weupe wa kawaida , ila ni ule wa ulemavu wa ngozi .

Kuishi na hali hii kulingana na Grace kumekuwa na changamoto kubwa sana , mojawapo wa changamoto hizi ni unyanyapaa na mtazamo ambao jamii inawapa watu kama Grace; kuna jamii hadi leo zinatazama albino kama soko tayari la kafara inayoleta 'bahati nzuri' katika maisha ya watu.

Ruka Facebook ujumbe

Haipatikani tena

Tazama zaidi katika FacebookBBC haihusiki na taarifa za kutoka mitandao ya nje.

Mwisho wa Facebook ujumbe

Grace alisema " Imani potofu zinaendelea kutiliwa mkazo na itikadi za kitamaduni , zinazosababisha binadamu wanaoishi na ulemavu wa ngozi kuwa kwenye hatari ya dhuluma na unyanyapaa , inaonekana kana kwamba sisi wenye ualbino tunadhamana kuu tukiwa wafu kwa sababu tunapozaliwa tunafichwa , na tunapofika utu uzima tunawindwa ili sehemu za mwili wetu ziuzwe "

Grace Nzomo na dadake Martha nzomo wote walizaliwa wakiwa na ulemavu wa ngozi

Chanzo cha picha, Grace Nzomo

Matamshi ya Grace yaliibuka pale alipoanza kufikiria kuhusiana na upeo au mtizamo ambao jamii imewapatia watu kama yeye , kwa kiasi kuwa kila siku katika maisha ya mtu mwenye kuishi na ulemavu wa ngozi anapambana kuishi kwa kuwa mwangalifu zaidi kuliko mtu mwingine.

"kuishi katika sehemu nyingi barani Afrika , kuna hatari chungu nzima , lakini kila siku watu kama sisi tunapigana kudhihirishia ulimwengu urembo na nguvu tulionayo katika maisha haya "Grace aliongezea kusema

Grace Nzomo alizaliwa miaka 26 iliyopita, yeye ni mtoto wa kwanza katika jamii yake, ana dada yake kwa jina Martha Nzomo mwenye miaka 22 ambaye anamfuata, ambaye pia alizaliwa na hali hiyo hiyo , haikuwa rahisi kwa jamii yake Grace kuwa wazazi wake walijifungua watoto wawili waliofuatana wakiwa na ugonjwa ambao unatizamwa na jamii kwa njia tofauti kabisa .

Ila kwa wazazi wake Grace walipambana kwa hali na mali kuwalea mabinti wao kwa mapenzi na pia kwa kuwafahamisha kuwa walikuwa ni watu tofauti na watoto wengine kutokana na ulemavu wao wa ngozi.

Njee Wangoi anaishi na hali ya vitiligo

Chanzo cha picha, Njee Wangoi

"Nilipozaliwa na nikafikisha wakati wa kwenda shuleni , waalimu na wanafunzi hawakuwa na ufahamu wa hali kama yangu , kwa hiyo hawakujua hata jinsi ya kunichukulia , lakini kwa kuwa mamangu mzazi alikuwa mwalimu alisaidia sana kuhamasisha waalimu na pia wanafunzi kuhusu hali yangu wakati huo mambo yalikuwa mepesi kwangu " Grace alisema

Kulinganana Grace mamake alikuwa ni msaada mkubwa kwake kutokana na kuwa alikuwa mwalimu katika shule ya msingi alikokuwa anasoma , mmojawapo wa changamoto zake Grace ni kuwa mcho yake yalianza kuwa na matatizo ya kuona , akiwa mbali na maandishi ya mwalimu Grace alipata matatizo ya kuona kabisa , na ililazimu walimu wke kuandika kwa herifu kubwa zaidi , hii ni hali ambayo inawaa changamoto wau wengi wanaoishi na hali ya albino kuwa na shida ya macho , hususan wanapokuwa katika mazingira ya mwanga au jua

Njee Wangoi akiwa na mwathiriwa mwengine wa hali ya vitiligo

Chanzo cha picha, Njee Wangoi

Changamoto iliwadia alipoingia shule ya sekondari , na waalimu wa somo la Jeografia , chemia walipendekeza kuwa Grace aachishwe masomo kwa kuwa alikuwa na mattaizo ya mcho , na ilipendekezwa kuwa aingie shule ya watu wasiokuwa na uwezo wa kuona ilikusoma , kupitia BRAILE ,

Braile ni maandishi rasmi ya watu vipofu , hali hii Grace anasema ilimpotezea muda mwingi na pia kumkosesha nafsi ya kusomea taaluma za udakitari na kadhalika

Lakini Grace hakukata tamaa licha ya kuwa na changamoto ya kuona , alihitimu n ahata kuingia chuo kikuu kimoja nchini Kenya aliposomea Saikolojia

Grace pia anashiriki sana kama mwanamitindo na maonyesho ya ulimbwende ambapo anachukua nafasi ya hali yake kudhihirishia ulimwengu changamoto zinazoandamana na watu wenye ulemavu wa ngozi

''Mimi hushiriki katika maonesho ya mavazi na urembo , kwa kuwa nina Imani kuwa unapokuwa na ujasiri wa kujitokeza kimsomaso licha ya muonekano wako uwa kimwili , basi unadhihirishia ulimwengu kuwa wewe umejikubali , na hauhitaji mtu mwengine kukueleza wewe ni nani '' Grace alisema

Grace anasema kuwa wakati wake wa ziada yeye hujipumbaza na densi za mtindo wa kilatino, kuogelea .

Njee Wangoi ni mtetezi wa watu wanaoishi na hali ya vitiligo

Chanzo cha picha, Njee Wangoi

Grace ana maono makubwa kwake yeye na kwa watu ambao wanaishi na ulemavu maishani.

Ya kuwa licha ya changamoto nyingi ambazo zinawazunguka wanajizatiti kuyafikia malengo yao kama binadamu wengine duniani

Grace Nzomo hayuko pekee yake katika Kuishi na changamoto za ngozi Wakati Bi Elizabeth Wangui mwenye miaka 26 pia kutokana nchini Kenya alipogundua alama nyeupe usoni , Alikuwa wa haraka Mno kupuuza tu , lakini ikawa hofu kwani alama hiyo haikwisha.

"Nilikuwa kidato cha Pili , nilidhani ni alama ya chaki ya mwalimu nilipoifuta niligundua ilikuwa ndani ya Ngozi yangu " alisema Wangui

Ilibidi niombee ruhusa shuleni kutafuta matibabu , Alipata matibabu na kupona na akarejea shule, punde tu alama nyingine nyeupe ikatokea mgongoni , wakati huu ilienea kwa kasi Mno , na alipotafuta matibabu ndipo aliambiwa kuwa ana ugonjwa wa ngozi wa Vitiligo.

Kila siku alama ile ilipanuka kwenye ngozi yake.

Hali hii ilisababisha muonekano wa sura yake kubadilika Mno.

Hivyo basi maisha yake kukumbwa na changamoto nyingi .

Uso wake uliathirika kwa kiasi kikubwa na kuanza kuwa na madoa meupe na Meusi.

Maria Nzomo anayeishi na tatizo la ulemavu wa ngozi

Chanzo cha picha, Maria Nzomo

Anataja kuwa wengine wamemfananisha na ngozi ya wanyama kama ngombe, na kudhihirisha unyanyapaa mkubwa kutoka kwa jamii kuhusu hali ya Vitiligo

" wengine husema kuwa niliungua na wengine pia kusema kuwa ni ishara ya bahati mbaya maishani , Yaani kila mtu ana maoni yake kuhusu muonekano wangu " alisema Wangui

Wangui anasema kuwa wakati mwingine baadhi ya watu hukataa kumsalimia kwa kuhofia kuwa akiwashika mikono yao au kuwakumbatia wataambukizwa hali anayoishi nayo.

Je wataalamu wa ngozi wanasema nini kuhusu vitiligo?