Virusi vya corona: Hifadhi nyingi barani Afrika zafungwa kuepuka maambukizi kwa nyani

Haijulikani kama nyani hao wanaweza kuambukizwa virusi vya corona, lakini kuna wasiwasi kuwa wanyama hao wanaweza kuwa hatarini sawa na binaadamu.Wiki hii chui aliyekuwa kwenye hifadhi ya Bronx alikutwa na virusi vya corona.

Hatua mpya zimewekwa kwa ajili ya kuzuia maambukizi kwa wanyama hao.Dokta Kirsten Gilardi ofisa wa juu wa madaktari wanaotunza wanyama, taasisi inayowahudumia nyani kwenye msitu wa Rwanda, Uganda na DRC:

''Hatujui kama nyani walioathirika ni wa milimani; hatujaona ushahidi wowote kuhusu hilo,'' alisema. ''lakini kwa sababu nyani wa milimani wanalingana na uwezo wa binaadamu katika kuambukiza na kuambukizwa, tunajua kuwa wanaweza kupata maradhi katika mfumo wa upumuaji.''

Nyani wa milimani (beringei beringei) ni viumbe wanaoweza kuwa hatari wa nyani wengine wanaopatikana kwenye msitu wa Rwanda, Uganda na DRC.Nchi zote tatu zimeshuhudia maambukizi kwa binaadamu,huku utalii wa wanyama hao ukiwa umefungwa kwa sasa.Kutochangamana.

Kazi ya watunza wanyama na maafisa wa nyamapori inaendelea, lakini kwa tahadhari. ''Zaidi tunachokifanya sasa katika suala la kutotengamana, na kujiweka karantini , ni suala muhimu lililo kwenye mapendekezo ya kutunza wanyama hao pia,'' anaeleza dokta Gilardi.

Hata kabla ya mlipuko, watu walitakiwa kukaa umbali wa mita saba mbali na nyani wakati wote.Masharti mapya kutoka kwa Umoja wa hifadhi za asili (IUCN) umetaka watu wakae umbali wa mita 10 kutoka kwa nyani, huku idadi ya wanaotembelea wanyama hao ikiwa imepunguzwa kwa ajili ya kuhakikisha usalama wao na afya.

Hakuna mtu mgonjwa, au aliyekuwa karibu na mtu aliyeathirika katika kipindi cha siku 14, anayeruhusiwa kuwasogelea nyani hao.Kuharibiwa kwa makazi yao na ujangili ni matishio kwa uhai wa nyani hawa, lakini virusi pia ni suala linalotazamwa kwa karibu. Maradhi ya kuambukiza pia yameorodheshwa kuwa miongoni.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:

Serge Wich, ni profesa wa baiolojia ya viumbe wa jamii ya nyani Chuo cha John Moores Liverpool nchini Uingereza, anasema serikali nyingi zimefunga utalii wa nyani, wakati watafiti na watu wa hifadhi wakichukua hatua zaidi.

Alisema: ''Hatujui, kama wameathirika, athari za kiafya ni zipi, lakini kwa kuangalia athari zake kwa watu, ni hatari ambayo haiwezi kutazamwa kwa juu juu, hivyo tahadhari hizia mbazo zinachukuliwa na mmoja ni muhimuili kupunguza hatari ya maambukizi.

Kituo cha kubadili tabia Sepilok Orangutan kwenye kisiwa cha Borneo ni moja ya hifadhi za nyani wakubwa ambacho kimefungwa.

Susan Sheward, mwanzilishi na mwenyekiti wa Orrangutan Appeal UK, amesema kwenye taarifa yake: ''ugonjwa unaweza kuua viumbe aina ya orangutan ambavyo tayari viko hatarini, ni hatari ambayo hatuwezi kuichukua, hivyo taasisi ya OAUK itafanya kila inachoweza kuhakikisha nyani hao wanakuwa na afya njema na salama.''

Unaweza pia kutazama:

Kuna aina nne za nyani wanaoishi mpaka sasa: Gorilla (Africa)Orang-utans(Kusini mnwa bara la Asia) bna chimpanzee(Afrika). Binaadamu wana mahusiano ya karibu na nyani wakubwa, wakihusishwa na kiumbe wa zamani aliyekuwepo miaka milioni kadhaa iliyopita.