Coronavirus: Mamilioni ya watu watabaki masikini, Benki ya dunia yaonya

Watu zaidi ya milioni 24 wataathirika kiuchumi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona huko mashariki ya Asia na Pacific, kwa mujibu wa benki ya dunia.

Aidha ripoti hiyo inasema kuwa athari za kiuchumi zinaonekana kutoepukika katika mataifa yote duniani.

Benki hiyo imetoa angalizo la athari kubwa ambayo itajitokeza hasa katika mataifa yanayoendelea.

Athari hizo ni pamoja na utalii kushuka Thailand na visiwa cha Pasific, Vilevile kwenye viwanda vya Vietnam na Cambodia.

Benki ya dunia imetaka ukanda huo kuwekeza katika sekta ya afya na viwanda vya vifaa tiba ili kuwezesha bara hilo kuwa na hali ya ahueni wakijumlisha msaada wanaopata.

Katika hali hiyo ,watu wapatao milioni 24 au pungufu ya watu hao hawataweza kuepuka umasikini katika ukanda huo kwa mwaka 2020 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Kama hali ikiwa mbaya zaidi, benki ya dunia imeweka makisio kuwa watu wapatao milioni 35 ,wanatarajiwa kubaki katika ufukara, wakiwemo raia milioni 25 wa China.

Kiwango cha umasikini kilichopimwa ni chini ya dola 5.5 kwa siku.

Benki ya dunia imesema pia uchumi katika upande wa mashariki mwa Asia unakua polepole sana kiwango cha 2.1% ukilinganisha na 2019 ulikuwa unakuwa kwa 5.8%.

Benki ya dunia imeeleza kuwa si rahisi katika hali hii ya mlipuko wa ugonjwa ,uchumi kukua.

"Habari njema ni kwamba ukanda huo umeweza kukabiliana na janga hilo ingawa mataifa yake wanapaswa kuchangamka kurejesha uchumi katika mstari kama ilivyokuwa hapo awali".

Takwimu za uchumi wa China zilizotolewa siku ya Jumanne, zinaleta matumaini wakati wakiona namna ya kuwa na viwanda katika majengo waliyojenga mwezi Februari.

Maafisa wa China wameonesha namna walivyoibuka kwa kasi mwezi huu na kuvunja rekodi ya 35.7 kwa mwezi Februari.

Huku takwimu za juu ya 50 kuonekana kukua.

Hii inamaanisha kuwa shughuli za kiuchumi zimekuwa licha ya kwamba bado ziko chini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Matokeo ya sasa ni jambo ambalo haliwezi kuzuilika katika mataifa yote duniani kwa mwaka 2020.

Masikini watazidi kuwa masikini na wataongezeka-wakati mataifa tajiri pia watahangaika kuimarisha biashara zao na maendeleo yao.