Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Coronavirus: Idadi ya walioambukizwa virusi vya corona yafikia 75 Rwanda
Rwanda imethibitisha kuwa na wagonjwa wapya watano wa maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 siku ya Jumanne na mpaka sasa kufikia 75, Wizara ya afya Rwanda imetangaza.
Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Ijumaa Rais Paul Kagame alisema idadi hiyo itaendelea kuongezeka kwasababu wale waliotangamana na waathirika wanaendelea kutafutwa.
Katika visa vya hivi punde vya maambukizi, watu sita walitokea Dubai, wawili kutoka Afrika Kusini, mmoja kutoka Nigeria na mwigine alikuwa amesafiri maeneo ya Afrika mashariki hivi karibunii, ilisema taarifa ya wizara ya afya nchini humo.
Rwanda kwa sasa in ajumla ya wagonjwa 70 wa corona, 32 kati ya hao waliwasili nchini kutoka Dubai.
Wiki iliyopita waziri wa afya wa Rwanda alikiambia kituo cha televisheni cha Rwanda kwamba hali hiyo ya maambukizi ilitokea baada ya wafanyibishara wengi wa Rwanda kurejea nyumbani kutoka Dubai, serikali ilipotangaza kuwa itafunga mipaka yote ya nchi.
Rwanda inaongoza kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa wa corona katika kanda ya Afrika Mashariki ikiiwa na wagonjwa 70, ikifuatiwa na Kenya 42, Uganda 33, Tanzania 14, huku Burundi na Sudan Kusini zikiwa hazijarekodi visa vyovyote vya maambukizi.
Siku ya Jumapili Rwanda ilianza wiki ya pili ya kukaa nyumbani ili kudhibiti kuenea kwa virusi.
Katika hotuba yake kwa taifa Bw. Kagame alisema serikali inatoa msaada wa chakula kwa kwa familia zisizojiweza na ambazo zimeathiriwa na amri ya kukaa nyumbani.
Mamlaka nchini humo siku ya Jumamaosi alianza shughuli ya kugawa chakula mjini Kigali kwa kuzitambua familia masikini zinazojikimu kutokana na shughuli za kila siku.
Maelfu ya familia zinatarajiwa kupokea vyakula vya msaada kutoka kwa serikali mchakato wa utambuzi utakapokamilika.
Taarifa zaidi kuhusu coronavirus:
Hatua za kudhibiti maambukizi
Mwanzoni mwa juma lililopita, Rwanda ilitangaza kufunga mipaka yote ya nchi hiyo na watu kuamrishwa kusalia majumbani mwao katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
Hatua zingine zilizochukuliwa ni pamoja na watumishi wote wa serikali na wa kibinafsi kufanyia kazi nyumbani na safari za kuenda mikoani kusitishwa kwa wiki mbili kukiwa na uwezekano wa muda huo kuongezwa.
Vilabu vya pombe na, maduka yasio ya chakula pia yamefungwa huku usafiri wa bodabobda ukisitishwa.
Hatua hiyo ilichukuliwa siku moja baada ya wizara ya afya ya Rwanda siku ya Jumamosi kutangaza kuwa watu wengine sita wameambukizwa virusi vya corona miongoni mwao mtoto mchanga wa miezi 10.