Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Coronavirus: Mapambano ya nyuma ya pazia kati ya Marekani na China baada ya mlipuko wa virusi vya corona
Iko wazi kuwa sasa dunia haiko katika wakati mzuri na uhusiano kati ya Marekani na China.
Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akitoa matamsi ya mara kwa mara kuwa virusi vya corona ni "virusi vya China".
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo naye anaviita "virusi vya Wuhan", jambo ambalo ambalo limeikera sana China.
Rais na waziri wa mambo ya nje wote wanailaumu China kwa kushindwa kukabiliana na mlipuko huu.
Lakini msemaji wa China amekanusha madai yao na kusema kuwa walikuwa China ilikuwa wazi katika tatizo hilo kuanzia mwanzo kabisa.
Kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii kuna tetesi zinazodai kuwa ugonjwa huu umesababishwa na mpango wa wanajeshi wa Marekani.
Wakati wanasayansi wanapinga madai hayo na kusema kuwa ugonjwa huo virusi vyake ni vya asili na hakuna aliyevitengeneza.
Lakini hii si vita ya maneno peke yake, kuna mapambano zaidi yanayoendelea.
Mapema mwezi huu, wakati Marekani ilipotangaza kufunga mipaka yake yote kwa wasafiri wengi wa mataifa ya bara la Ulaya, Italia ikiwemo serikali ya China imetangaza kutuma vifaa tiba Italia, taifa ambalo linaongoza kwa maambuizi mengi ya virusi vya corona.
China imetuma msaada wa kukabiliana na corona kwa nchi za Iran na Serbia pia.
Ni wakati ambao tunaona ishara kubwa .
Hii ni ishara ya mapambano ya taarifa kwa kile ambacho kiko nyuma ya pazia, huku China ikiwa inapata unafuu katika janga hili lakini janga limegeuka kuwa la ulimwengu.
Kiukweli, mapambano haya kwa Marekani, ni wakati ambao inabidi tushushe mikono yetu chini.
Na msaada wa vifaa tiba wa ndege ndogo ya vita ya Marekani nchini Italia ni ngumu kuwa msaada wa kutosha.
Huu ni wakati mgumu ambao mamlaka na mfumo wa kisiasa katika mataifa yote yanakabiliana nao na hawajawahi kukutana na hali kama hii hapo kabla.
Viongozi watauwa katika hali ngumu ya kiuchumi.
Viongozi ambao wako madarakani watalaumiwa kwa kushindwa kuabiliana na tatizo hili , ufanisi wao katika uongozi utahukumiwa na watu kwa kushindwa kukomboa nchi zao kutoka katika ugonjwa huu mpya.
Ugonjwa wa corona umekuja wakati ambao Marekani na China walikuwa tayari katika uhusiano ambao si mzuri.
Tayari mahusiano yao ya kibiashara yalikuwa mashakani kabla ya virusi vya corona kupiga hodi.
Mataifa yote mawili, China na Marekani wanajiandaa kupambana wazi huko Asia-Pacific.
China imejiweka tayari kuwa taifa lenye nguvu za kijeshi kwa upande wake na ina nia ya kupanua wigo wake katika kile ambacho inakiamini kuwa ni kiwango cha kimataifa kinachohitajika.
Ugonjwa huu umetishia uhusiano wa Marekani na China uwa mbaya zaidi.
Ingekuwa muhimu kwa mataifa yote mawili yangeelewana wakati huu ambao dunia iko kwenye janga hili la ugonjwa.
Wakati ambao ugonjwa utaweza kutokomezwa, Uchumi wa China unahitaji kufanya jukumu kubwa la kuweza kusaidia kujenga uchumi wa dunia.
Lakini sasa, China inasaidia maeneo mengi kukabiliana na virusi vya corona. Takwimu za dawa na majaribio kadahaa yanaendelea kushirikishwa kwa watu.
China ina viwanda vingi vya dawa na vifaa tiba vikiwemo viwanda vya barakoa, mavazi ya kujikinga maambukizi na vifaa vyote vya umhudumia mgonjwa aliyepata maambukizi.
China iko mbali katika maduka na viwanda vya madawa duniani, wana uwezo wa kuhudumia mataifa kadhaa.
China inachelewa kutumia fursa nyingi lakini kwa mujibu wa wakosoaji wengi kama rais Trump, ni wao ndo waliosababisha janga hili.
Utawala wa Trump ni kama umekataa kukubali ukubwa wa tatizo, kwa kuona kuwa huu ni wakati mwingine wa kuiweka Marekani kuwa ya kwanza na kujiona kuwa iko juu katika mifumo yote.
Ingawa tatizo lililopo sasa ni tatizo la utawala wa dunia.
Wataalamu wawili wa Asia, Kurt M Campbell - ambaye ni katibu msaidizi wa mataifa ya Mashariki mwa Asia na masuala ya uhusiano wa Pacific na uongozi wa Obama - na Rush Doshi, walituma ujumbe wa maandishi kwenye ofisi za mambo ya nje: "Marekani kama kiongozi wa dunia kwa miongo saba imekuwa haijengi utajiri wake au nguvu za utawala wake pekee lakini pia ilikuwa muhimu kwa nafasi yake kuwiwa kusaidia ulimwengu , na kushirikiana na dunia katika kukabiliana na majanga".
Ugonjwa wa corona , wanasema kuwa ugonjwa huu unapima sifa ya kiongozi, mpaka sasa Marekani inaonekana kushindwa mtihani huu.
Na makosa hayo yanafanya China kuchukua fursa haraka na kuziba ufa ambao Marekani unaonekana kuutengeneza kwa kushindwa kusaidia dunia kukabiliana na janga la ugonjwa huu wa corona.
Wengi wanaweza kushangaa ni namna gani China inachukua fursa hiyo ya kuwa taifa kubwa la usaidizi wakati janga la ugonjwa lilianzia kwao
Taarifa kwa vyombo vya habari nchini Marekani, imeandikwa katika tovuti ya mambo ya nje: Hofu na usimamizi mbovu wa janga hili umekuza tatizo kuwa kubwa zaidi.
China imeweka propaganda nyingi ndani na duniani ya jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huu, jitihada ambazo ni kubwa ukilinganisha na kile ambacho serikali za bara la ulaya na Marekani hawafanyi.
Wachambuzi wengi wa bara la Ulaya wanaona kuwa China inachukua mamlaka makubwa na mataifa mengi yana hofu matokeo ya kiuchumi yatakayosababishwa na ugonjwa huu ambayo tayari yameanza kuonekeana kidogo kidogo.
Utawala wa Trump umeonekana ukikosolewa kwa wazi lakini wengi wanaona ni kwa sababu ya utofauti wa taifa hilo na China, usalama wa teknolojia ya China kwa mataifa kama Iran na mengineyo.
China inajaribu kutumia mlipuko wa ugonjwa huu kujaribu kuanzisha utofauti wa mahusiano yao ya baadae katika teknolojia- inawezekana kuwa China inaweza kuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani kwa kuhusisha kampeni zake na jiirani zake - Japan na Korea Kusini- haswa kwenye upande wa vifaa vya afya kwa ulaya inawezekana kuonekana kuwa kitu kidogo.
Leo watengeneza sera wa Marekani wanapaswa kutambua kuwa mapambano dhidi ya virusi vya corona yanaweza kuibuka kwa wakati mwingine ambao una shujaa mwingine wa dunia.