Virusi vya corona: Jinsi Covid-19 ilivyoathiri matamasha

    • Author, Na Dinah Gahamanyi
    • Nafasi, BBC News Swahili
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Mlipuko wa virusi vya corona ambao umesambaa katika mataifa mbali mbali duniani umeathiri matukio mbali mbali ya burudani yanayohusisha mikusanyiko ya watu, miongoni mwa mwake yakiwa ni matamasha.

Akizungumza na BBC Swahili kupitia ukurasa wa Facebook Nasib Juma al maarufu Diamond Platnum ameelezea kuwa kwa sasa sekta ya muziki imeathiriwa na mlipuko wa virusi vya corona.

Diamond amesema kuwa wanamuziki wengi akiwemo yeye binafsi wamepoteza mamilioni ya pesa kwa kutoweza kufanya shoo za matamasha ambayo kwa sasa yamezuiwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona:

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Bwana Diamond alitangaza kuahirisha matamasha yake ya Ulaya .

Awali Diamond alikua amewaalika wapenzi wa muziki wake kuhudhuria matamasha yake mkiwemo tamasha ambalo alitarajia kulifanya nchini Uswiss, ambapo akiwahamasisha kununua tiketi za tamasha mapema:

Msanii maarufu wa Nigeria Davido Adeleke pia amelazimika kuahirisha tamasha lake alilotarajiwa kulifanya Marekani kutokana na mlipuko wa Coronavirus. Licha ya kwamba tiketi za tamasha hilo ziliuzwa na kuisha imemlazimu kuwaomba radhi mashabili na wapenzi wa muziki wake:

''Ninasikitishwa na kuvunja kile ambacho kimeshuhudia kuuzwa kwa tiketi zote za safari bora ya kimuziki hadi sasa , lakini kuahirisha ni kitu sahihi kukifanya. Kwa afya na usalama wa mashabiki wangu na wahudumu ni muhimu na hakuna kingine tena cha muhimu. Uwe salama nitawaona hivi karibuni! Mungu awe nanyi nyote!'' ulisema ujumbe wa Davido kupitia mtandao wake wa Instagram

Nchini Kenya pia shughuli mbali mbali zikiwemo zenye mikusanyiko ya watu yakiwemo matamasha zimesitishwa hususan baada ya kuthibitishwa kwa virusi vya corona.

Moja ya burudani kubwa zilizotangaza kuahirishwa ni ile ya vichekesho inayotolewa kupitia televisheni. Mmiliki wa kampuni ya vichekesho Churchill Daniel Ndambuki, al maarufu Mwalimu king'ang'i alifuta maonyesho yake kufuatia mlipuko huo katika taarifa yake aliyoituma kwenye ukurasa wake wa Facebook mara baada ya kutokea kwa mlipuko wa corona:

Mchekeshaji maarufu wa Televisheni nchini Marekani Trevor Noah aliahirisha kuishirikisha hadhira katika kipindi chake kutokana na hofu ya coronavirus.

Mchekeshaji huyo kutoka kutoka Afrika Kusini Trevor Noah huialika hadhira katika kipindi chake cha kila siku ya Alhamisi ambacho awali kilikua kikipeperushwa moja kwa moja ameambua kuwa hatawaalika watu kuja katika studio yake kutokana na janga la virusi vya corona.

Trevor Noah amesema kipindi chake cha Daily Show kililazimika kutekeleza jukumu lake la kukabiliana na virusi vya corona.

'' Kutekeleza sehemu yangu ya kukabiliana na janga, Daily haitakuwa na hadhira ya moja kwa moja studio kuanzia Jumatatu.

Matamasha mengine makuu yamechukua hatua sawa na hiyo huku virusi hivyo vikiripotiwa kusambaa nchini Marekani.

Tangu kutokea kwa virusi nchini Uchina mwaka jana, virusi hivyo vimewauwa watu 230,000 kote duniani 63,000 miongoni mwa vifo hivyo vikitokea Marekani..

Matamasha mengine makuu yalichukua hatua sawa na hiyo huku virusi hivyo vikiripotiwa kusambaa nchini Marekani.

Hakuna safari za matamasha kabisa kote barani Asia na Italia kwa sasa, huku mikusanyiko ya watu zaidi ya 1,000 ya matamasha ikiahirishwa katika mataifa ya Uswis, Ufaransa na katika baadhi ya miji nchini Ujerumani.

Kufutwa kwa mikusanyiko na matamasha mbalimbali kunatarajia kusababisha hasara katika sekta ya burudani kwa watu na makampuni binafsi katika maeneo mbali mbali duniani.

Unaweza pia kusoma: