Makazi duni Nigeria: Makazi duni Lagos yako juu ya maji

Wakati Umoja wa mataifa ulipotoa ripoti wa kukemea makazi duni nchini Nigeria,mwandishi wa BBC Mayeni Jones alitembelea baadhi ya maeneo hatari wanamoishi watu maskini katika mji mkuu wa kibiashara nchini humo, Lagos.
Hapo juu ni maeneo ya karibu ya mtaa wa Oko-Agbon ambao unajulikana kama mtaa duni uliojaa maji kila kona Makoko kama unavyoonekana katika picha.
Kuna ngalawa au boti za mbao ambazo zinawasaidia kutoka eneo moja mpaka lingine kutokana na eneo hilo kujaa mifereji ya maji taka kila kona.
Baadhi ya watu ambao wanaishi nje hapo wanalielezea eneo hilo kama Venice ya Afrika.
Ingawa ukikaribia eneo hilo ni picha tofauti kabisa.
Maji yamejaa taka za kila aina na harufu inayotoka katika katika eneo hillo ni mbaya na hewa pia nzito.

Mamia ya watu wanaishi katika nyumba za eneo hilo ambapo kuna usiri mdogo sana.
Pamoja na hali hii bado kuna watu ambao hawana makazi.
Dosu Francis ambaye ni mvuvi alihamia hapo miaka mitatu iliyopita, baada ya kuondolewa kutoka Otodo Gbame, eneo lingine la makazi duni ya maji ambayo yako umbali wa kilomita 25 kutoka anapoishi sasa.
Amekuwa akilala na mke wake na mtoto katika kibanda ambacho huwa kilikuwa kinatumika kuchoma samaki.
Kibanda hiko kinamilikiwa na kaka zake, hivyo inamaanisha kuwa yeye anaishi hapo kwa muda tu ingawa miaka mitatu imepita sasa na hajafanikiwa kupata maeneo mengine ya kuishi.
'Kuwaondoa wanangu'
"Tangu nilipoondolewa, maisha hayajawa rahisi kwangu," alisema bwana Francis kwa sauti ya upole.
"Nina watoto watatu ambao wako katika umri wa kwenda shule, lakini sina uwezo wa kulipa ada yao na sina uwezo wa kuwalisha, hivyo ilinibidi niwahamishe watoto wangu wawili kwenda kuishi na binti yangu wa kwanza ambaye ameolewa.
"Ninaishi hapa na mtoto wangu mmoja tu wa kiume."

Wakati alipokuwa anaonyesha kibanda anachoishi kilichoezekwa kwa makuti na plastiki, ameeleza kuwa bado huwa wanaoka samaki muda wa mchana.
Na usiku, wanapasafisha na kulala.
Kuna sehemu za wazi ambazo wakati wa mvua lazima ni changamoto.
"Huwa tunatandaza mifuko ya plastiki katika kibanda hicho wakati wa mvua," alijibu.

Bwana Francis alisema kuwa makazi mengine ya Otodo Gbame ambayo waliondolewa mwaka 2017 baada ya majirani kunaka ardhi yao, waliita polisi kutufukuza.
"Walianza kutufukuza kwa vitisho na tulidhani tungeweza kumalizana na polisi na kutusamehe lakini siku moja walikuja na kuondoa kila mmoja nje ya eneo hilo."
Nilimuuliza kama alipata fidia tangu alipoondolewa.
"Hakuna kitu tulichopewa,alieleza, "hakuna ambaye alipewa pesa, hakuna aliyetupa nyumba yaani hatukupewa chochote, zaidi ya kutuambia tuondoke."

Simulizi ya Bwana Francis si ya kipekee sana katika eneo hilo.
Mamilioni ya watu waliondolewa katika makazi duni miaka 20 iliyopita huku wakiwa wamepewa muda mfupi wa kujiandaa na bila kupewa nyumba nyingine kuwa mbadala.
Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International,kati ya mwaka 2000 na 2009, mamlaka ya Nigeria iliwalazimisha watu zaidi ya milioni mbili kuondoka katika makazi duni.
Kumekuwa na utumiaji wa nguvu katika kuwaondoa watu katika mji wa Lagos.
Mwezi Februari 2013, mamlaka ya nchi hiyo iliwaondoa watu 9,000 kutoka Badia iliyopo mashariki ya kati ya Lagos, ili kupisha serikali kujenga mradi wake.
Mwezi septemba 2015, watu wengine 10,000 waliondolewa katika eneo hilo.
Mwanzoni mwa mwaka huu, watu wapatao 10,000 walipewa muda wa saa moja kufungasha mizigo yao na kuondoka katika fukwe za bahari inayojulikana kama 'Tarkwa Bay', maarufu kwa watu wa Lagos kwenda kupumzika.
Pamoja na kelele nyingi zilizopigwa katika mitandao ya kijamii, nyumba nyingi ambazo eneo hilo askari wa majini ndio wamepewa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwishoni mwa mwezi Januari , nilikutana na baadhi yao nje ya mahakama ya Ikoyi, ambao walikuja kupinga ujenzi ambao unaendelea katika sehemu waliokuwa wanaishi.
Wanasema kijiji chao kiliharibiwa ili kupisha ujenzi wa maeneo ya burudani.
"Tunaamini kuwa ni kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi," mkazi wa zamani wa eneo hilo alisema. "Kihistoria , maeneo hayo dunitunayoondolewa huwa yanajengwa na kuwa nyumba au mali za watu binafsi"
Mamlaka inakanusha madai ya jumuiya ya watu hawa walioondolewa na kusema kuwa sababu baadhi walikuwa wanafungua mabomba ya mafuta kinyume na sheria.

Lakini nilipoenda Tarkwa Bay kujionea mwenyewe, wanajeshi walinitaka kuondoka katika eneo hilo.
Walisema kuwa hawana cha kuficha lakini nilipaswa kufuata utaratibu ili kutembelea eneo hilo.
Ni rahisi kuelewa kwa nini wakazi wa eneo hilo wana wasiwasi wa kile kinachoendelea.

Baada ya makazi ya jirani ya bwana Francis' Otodo Gbame, kuondolewa miaka mitatu iliyopita, nyumba za gharama na starehe zilianza kujengwa katika eneo hilo.
Lakini wengi wanasema kuwa maendeleo mara nyingi huwa ghali sana na wengine wanabaki bila kitu.
"Utashangaa kujua kuwa baadhi ya majengo yako wazi mjini Lagos, huku maelfu ya watu wanalala katika makazi duni au hawana makazi kabisa," alisema Dkt Muyiwa Agunbiade,mwalimu wa chuo kikuu cha agos anayefundisha masomo ya mipango ya miji.

"Nchini Nigeria hatujasahau hatua ya kutoa makazi. Jambo la muhimu, ninahisi serikali haina uwezo wa kutoa huduma hiyo."
Anaamini kuwa njia ambayo inaweza kusaidia ni kutoa idhini ya umiliki ardhi. Bila hivyo watu wanaoishi katika makazi ambayo sio rasmi wataendelea kuondolewa kila kukicha, alisema.
"Lakini kama serikali itafanikiwa kuwasajili katika ardhi hizo , wenyewe watakuwa na imani ya kujenga nyumba nzuri na serikali haitahitaji kuwaondoa."
Kwa sasa wanaishi hivyo kwa kuwa hawana uhakika wa kesho yao.












