Nzige: Wadudu waharibifu wafanywa kuwa kitoweo Uganda na Somalia

Chanzo cha picha, Reuters
Raia wa Uganda wanaoishi kaskazini mwa wilya ya Kitgum wanakula nzige wa jangwani ambao wameharibu mimea yao kulingana na kituo cha habari cha Uganda radio Nnetwork URN.
Hatua hiyo inajiri baada ya ripoti nyengine kwamba raia wa Somali pia wamekuwa wakibadilisha jangwa hilo la uvamizi wa nzige na kuwafanya kitowe wadudu hao
Ripoti za vyombo vya habari nchini humo zinasema kwamba raia wa mji wa Adado katikati mwa Somalia wamekuwa wakiwakamata wadudu hao na kuwafanya kitoweo.
Raia mmoja amesema kwamba wadudu hao ni watamu kushinda samaki.
Haipatikani tena
Tazama zaidi katika FacebookBBC haihusiki na taarifa za kutoka mitandao ya nje.Mwisho wa Facebook ujumbe
Mwengine aliambia runinga ya Somali ya Universal kwamba anaamini kwamba wadudu hao wana manufaa ya kimatibabu na kwamba anawafanya kitoweo kwa matumaini ya kupunguza uchungu uliopo mgongoni mwake pamoja na shinikizo la damu.
Baadhi ya wakaazi wameitaka mikahawa kuanzisha chakula cha nzige hao.
Uvamizi wa nzige hao katika baadhi ya maeneo mnchini Somalia na Ethiopia umeharibu mimea na kutishia baa la njaa katika eneo hilo kulingana na shirika la chakula duniani FAO.
Wakati huohuo vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kwamba mavuno duni yamewafanya baadhi ya wakulima kuwafanya nzige hao kuwa chakula chao.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Lakini wengine wana wasiwasi kuhusu matatizo ya kiafya kwa sababu serikali ya Uganda imekuwa ikiwanyunyizia dawa ili kujaribu kupunguza idadi yao.
Raia wamedai kwamba wamekuwa wakiwashika wadudu hao , kuwachemsha na baadaye kuwakausha kabla ya kuwakaanga.
Picha zilizosambazwa na gazeti la The Observer zilionyesha raia wakiandaa wadudu hao kwa mlo.
Bwana John Bosco Komakech afisa wa kilimo anayekabiliana na wadudu katika wilaya ya Kitgum alisema kwamba matumiz ya nzige kama mlo hayana athari zozote huku akisema kwamba wale wanaopatikana na raia hawajanyunyuziwa dawa.
Nzige wa jangwani wameharibu mimea nchini Somalia, Kenya Uganda , Ethiopia na Suda Kusini katika kile kilichoelezewa kuwa uavamizi mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 25.














