Mbunge wa Tanzania Zitto Kabwe atishiwa kuuawa baada ya kushinikiza kusitishwa kwa mkopo wa benki ya Dunia

Muda wa kusoma: Dakika 2

Chama cha upinzani cha ACT Wazalendo nchini Tanzania kimetoa shutuma kuwa kiongozi wake amepokea vitisho vya kuuliwa baada ya kuiambia benki ya dunia kuzuia mkopo kwa serikali ya Tanzania kutokana na wasiwasi wa haki za kibinadamu nchini humo.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kwamba Zitto kabwe alipokea na kulengwa kuuawa.

Spika wa bunge aliitaja barua ya bwana Kabwe kuwa ni uhaini mkubwa huku mwanachama mmoja wa chama tawala akitaka auwawe.

Makundi ya haki za kibinadamu yameonya kuhusu ukandamizaji nchini Tanzania.

Wiki iliopita benki ya dunia ilidaiwa kuahirisha uamuzi wake kuhusu iwapo kuendelea na mpango wake wa kuipatia Tanzania mkopo wa $500m ili kufadhili elimu nchini Tanzania kutokana na shinikizo kutoka kwa wanaharakati .

Benki hiyo ilikuwa imezuia fedha hizo 2018 kufutia wasiwasi kuhusu sera za taifa hilo kuwafurusha shule wanafunzi wajawazito.

Muungano wa wanaharakati ambao waliandikia benki hiyo walihoji kwamba kuidhinishwa kwa mkopo huo kutakuwa kunaunga sera ya kibaguzi ya kuwafurusha wasichana wajawazito mashuleni.

Sheria hiyo ya kikoloni ina kifungu kinachoruhusu mamlaka kuwafukuza wasichana wajawazito mashuleni.

Wanaharakati wanasema kwamba sheria hiyo imepatiwa uhai na serikali ya rais John Pombe Magufuli na maafisa wamekuwa tayari kuidhinisha .

Je vitisho hivyo vilitolewa vipi?

Katika kikao cha bunge siku ya Ijumaa, spika Job Ndugai alitaja barua ya bwana Kabwe kuwa uhaini mkubwa na kuifananisha na vitendo vilivyopelekea rais Donald Trump kushtakiwa bungeni , makossa anayokana.

''Yeye Bwana Trump ameshtakiwa kwa sababu alikuwa anakula njama na mataifa ya kigeni ili kuingilia maswala ya ndani ya Marekani . Tuna mbunge ambaye amekuwa akifanya vitendo kama vya bwana Trump - kuna swala la uhani hapo'' , alisema.

Abdallah Bulembo, kutoka chama chs mapinduzi CCM alitoa wito wa kuuawa kwa bwana .

''Kuna mtu mmoja aliyechukua maswala yetu ya ndani na kuyapeleka nje ya taifa , hafai kuruhusiwa kurudi na anafaa kuuawa pale alipo .Uhaini! kile ambacho bwana Zitto Kabwe amekuwa akilifanyia taifa hili ni uhaini''.

Wanachama wenzake walimuunga mkono na kumpongeza baada ya matamshi yake.

Akizungumza baada ya mkutano wa chama wikendi iliopita, afisa wa chama tawala cha CCM kitengo cha vijana Kenani Kihongosi alisema watu 'walioichafulia' jina Tanzania walifaa kuuawa.

''Tumechoka na watu wachache wasio na maana ambao wanalichafulia jina taifa letu lakini pia tumechoka na wale wanaotumiwa na wakoloni'', alisema.

''Natoa wito kwa vijana kuandika kuhusu mambo mazuri ambayo serikali inafanya lakini pia kutochoka kukosoa wale wanaokandamiza taifa letu , wao ndio maadui wetu wa kwanza na wanastahili kuuawa''.

Je Kabwe anasema nini?

Chama cha ACT Wazalendo kilisema kwamba CCM imekuwa ikiendesha kampeni inayomlenga bwana Kabwe , lakini kampeni hiyo ikachukua mwelekea mbaya na hatari mnamo tarehe 31 mwezi Januari 2020.

Wiki iliopita , bwana Kabwe aliwajibu wakosoaji wake katika mahojiano na runinga ya BBC ya Dira mjini London wiki iliopita akisema : Wanafaa kujua kwamba kuwa wazalendo hakumaanishi kuwa watiifu kwa serikali bali kwa taifa. Na hakuna njia kubwa ya kuonyesha uzalendo zaidi ya kukosoa serikali wakati inapofanya makossa.

Kulingana na benki ya Dunia stakhabadhi zilizokuwa zikielezea kuhusu mkopo huo, zilisema kwamba takriban wanafunzi wa kike 5,500 walizuiliwa kuendelea na masomo yao ya shule ya upili baada ya kuwa wajawazito 2017.

Wiki iliopita rais Magufuli aliwataka maafisa wa serikali kuwapuuza wakosoaji wa sera hiyo akisema : Makamu wa rais wa Benki ya Dunia alizuru nchini mwaka uliopita - watatupatia fedha wakijua msimamo wa Tanzania na kile tunachofanya. Waliosalia ni wapiga kelele musiwajibu hata kidogo.