Osprey: Ndege aliyeruka kutoka Finland hadi Kenya afariki

Chanzo cha picha, KSW
Ndege aliyesafiri zaidi ya kilomita 6000 kutoka Finland hadi Kenya Alhamisi iliopita amefariki.
Ndege huyo alipatikana katika maji ya ziwa Kanyaboli baada ya kuruka kilomita 6,948 na kutua katika kijiji cha Usalu katika eneo la Yimbo eneo la Bondo.
Katika taarifa yake siku ya Jumatatu Mkurugenzi wa KWS bwana Paul Udoto alisema kwamba ndege huyo anayekula samaki alifariki siku ya Jumapili.
''Tunasikitika kutangaza kifo cha ndege huyo licha ya juhudi zetu zote kumhifadhi na baadaye kumrudisha msituni. Tulikuwa tukimlisha na kumtibu ili aweze kupata afya njema tukiwa na mpango wa kumrudisha kule tuliko muokoa katika Ziwa Victoria ili asiweze kupoteza njia aliokuwa akielekea''.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Bwana Udoto alisema kwamba ndege huyo amedhoofika na alikuwa na upungufu wa maji mwilini kufuatia safari yake ndefu wakati alipokuwa akihamishwa kuelekea Nairobi.
Anasema kwamba ndege huyo alipata majeraha kadhaa wakati alipokwama katika wavu wa kuvulia samaki.
''Alikuwa na uzani wa gramu 950 kinyume na uzani wa kawaida wa kati ya kilo 1.3 hadi kilo 1.8 kwa ndege mkubwa wa aina ya Osprey'', alisema.
Bwana Udodo anasema kwamba upasuaji wa kimatibabu umebaini kwamba ndege huyo alifariki baada ya kufeli kiungo cha mwilini kutokana na njaa ya muda mrefu.
''Ndege huyo alikutwa na majeraha miguuni lakini alikuwa mzima wa afya licha ya kwamba alikuwa amekonda'', mamlaka ilisema.

Chanzo cha picha, KWS
Ndege huyo alijulikana asili yake kutokana na ringi aliyokuwa amevalishwa mguuni kuwa na maelezo ya asili yake kuwa makumbusho ya Finland (Museum Zool, Helsinki Finland, www.ring.ac, M-68528)," KWS ilituma maelezo.

Chanzo cha picha, KWS
Ndege huyo anayekula samaki aligunduliwa siku ya Jumatatu na idara ya wanyama pori Kenya.
Alikuwa katika uangalizi kwa siku chache kabla kuachiwa kwenda porini.














