Jinsi Paka walivyochukua nafasi ya binadamu Syria

Baada ya miezi kadhaa ya mapigano ya Syria na Urusi, mji wa Kafr Nabl ulioko Syria ambao sasa umegeuka kuwa makazi ya paka zaidi ya wanadamu.
Binadamu sasa wanapata faraja kutoka kwa paka hao katika wakati huu mgumu wa upweke, ameandika mwandishi wa BBC Mike Thomson.
Makazi ya ya watu pia yaliharibiwa na mabomu .Lakini kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 anayeitwa Salah Jaar (katika picha hapo juu) yeye hayupo peke yake.
Amezungukwa na paka wengi ambao wamekuwa sehemu ya maisha yake.
"Huwa ninajisikia vizuri sana wakati ambapo paka wakiwa karibu yangu," aliniambia. "'Paka hawa huwa wananiondolea majonzi na upweke na kujiona afadhali kidogo."
Nyumbani kwa Salah, huko Kafr Nabl, kulikuwa na watu zaidi ya 40,000 lakini sasa wamebaki chini ya watu 100 . Si rahisi kufahamu idadi kamili ya paka wengi waliopo katika mji huo lakini wapo mamia au hata maelfu.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Watu wengi waliondoka Kafr Nabl hivyo kufanya idadi ya watu kuwa ndogo. Paka wanahitaji mtu wa kuwajali kwa kuwapa chakula na maji, hivyo nimeamua kuwachukua wengi ili nifanye kazi hiyo.
Kila nyumba sasa ina paka wasiopungua 15 au zaidi ya 15," Salah alisema.
Salah bado anafanya kazi ya uandishi wa habari katika kituo cha redio nchini humo kinachoitwa, Fresh FM.
Licha ya kwamba kituo cha matangazo ya redio hiyo kimehamishwa katika mji ambao ni salama zaidi.

Kitu hicho cha redio ambacho kilituwa kinatangaza habari juu ya tahadhari ya mabomu yatakayolipuliwa, vichekesho na matangazo ya kupokea simu za wasikilizaji lakini sasa matangazo mengi yanahusu paka zaidi.
Watu wengi katika mji huo waliuliwa na wanamgambo wa kiislamu mnamo Novemba 2018,
Sasa kuna posho inayotolewa kwa ajili ya kununua maziwa na jibini ya paka.
"Paka wengi walizaliwa katika majengo hayo yaliyolipuliwa, wengine wamezoea kuongozana nami kila sehemu ma hata kulala pembeni yangu," Salah alisema.
Salah anasema kuwa huwa anatembea barabarani akiwa na paka 20 a 30 kila siku.

Kwa sababu kulikuwa na milipuko mingi, baadhi ya paka ni walemavu kwa sababu walijeruhiwa wakati wa vita.
Hivyo Salah anasema kuwa jukumu lake kubwa ni kutafuta namna ya kuwapa matibabu ingawa kuna uhaba wa madawa katika mji huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Tuko pamoja na paka hawa kwa shida na raha, wakati wa furaha na majonzi pamoja na hofu.
Paka wamekuwa wenza wetu katika maisha," alisema.














